Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Kayanza Pinda
WARIZRI
Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ameweka jiwe la msingi chuo cha Ualimu Kiuma
Bonite Tunduru ,Chuo kinacho milikiwa na
Mkurugenzi Dkt.Matomola,ikiwa ni Taasisi kubwa inayo unganisha Chuo cha
Waganga,shule msingi na sekondari na
shughuli nyingine za maendeleo.
Mhe.Pinda
alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa shirika hilo la Bonite ambalo
linaliletea maendeli wananchi wa Tunduru, Mkoa wa Ruvuma na majirani pamoja na
Taifa kwa ujumla.na kwamba alimshukuru sana Dkt Matomola kwa moyo wake wa
uzalendo wa kuanzisha taasisi kubwa kama ile kwa manufaa ya taifa, badala ya
kujinufaisha mwenyewe.
Aidha
mhe.Pinda katika mkutano na wananchi mjini
Tunduru leo, alisema ushururu kwa watu wadogo wadogo usitozwe, maana unaleta
kero kwa wananchi wa hali ya chini.
Kuhusu
maendeleo ya elimu wilayani humo, Mhe. Pinda amemwambia Mkuu wa mkoa kuwa asili
30 ya watoto wote waliyo faulu kuingia Kidato cha kwanza, ambao hawaja ripoti
waende shule mara moja.
Ambapo
kuhusu ujenzi kwa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Namtumbo hadi Tunduru utaendelea
kujengwa baada ya wakandarasi wa awali
kufukuzwa kwa kushinda kukamilisha katika muda waliyo pangiwa.
Waziri
Mkuu amesikia kilio cha watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambao
wamekaa kwa miaka mingi bila kupata
uhamisho kama vile ndiyo wamehamia, amewaambia
mara baada ya kufika Songea ataangalia nini cha kufanya. ( Na. Juma Nyumayo
katika Msafara wa Waziri Mkuu mkoani Ruvuma )
No comments:
Post a Comment