Wednesday, July 17, 2013

WANAHABARI WALIYORIPOTI AJALI ILIYOTOKEA KWENYE MSAFALA WA WAZIRI MKUU JANA ENEO LA NAMTUMBO WATIMULIWA KWENYE MSAFARA HUO, NA AJALI NYINGINE YATOKEA MBINGA GARI LA POLISI

WAKATI mwandishi wa Waziri Mkuu kuwatoa waandishi wawili wa mkoani Ruvuma  kwa kuripoti ajali iliyotokea kwenye msafara wa Waziri Mkuu jana katika eneo la Nantumbo , leo tena ajali nyingine imetokea kwenye ziara ya wilaya Mpya ya Nyasa na Mbinga ya gari la polisi.Hakuna aliyetangaza hiyo.

Kumbe ajali Zinapotokea za Waziri Mkuu hazitakiwi kutangazwa, Na waandishi wa habari ambao si wa Waziri Mkuu? Na waandishi wa Mawaziri wakuu wamepata mafunzo ya kuwakataza waandishi wengine wasitangaze matukio yanayotokeayawe  mazuri au mabaya katika Ziara ya Waziri Mkuu,na watangaze wao na wasipo tangaza basi, sasa nini maana ya uandishi wa habari?

No comments:

Post a Comment