Saturday, July 13, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKOANI RUVUMA NA MKUU WA MKOA WA MKOA HUO BWANA SAID THABIT MWAMBUNGU KUWA ,WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. MIZENGO PINDA ATAFANYA ZIARA MKOANI RUVUMA KWA SIKU 8

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe; Said Thabit Mwambungu akizungmza na waandishi wa habari
 Waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma wakifanya kazi zao,tayari kwa kuwapa wananch habari.,Peni/kamera na computer.
Waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa Mkoa


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda taanza ziara ya siku 8 katika mkoa wa Ruvuma kuanzia siku ya Jumatatu kuelekea wilaya ya Tunduru.

Akizungumza na waandishi wa  habari , Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Said Thabiti Mwambungu, kuwa Waziri Mkuu katika ziara hiyo atatembelea wilaya tano zote  za Mkoa huo na kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi, kuzindua miradi na kuongea na wananchi.

Aliwataka wananchi katika Manispaa ya Songea kujitokeze kumlaki katika Ikulu ndogo Mjini Songea kesho Jumapili,na kuanza ziara Wilaya ya Tunduru, Namtumbo, Wilaya ya Nyasa na kuizindua Wilaya mpya ya Nyasa.

Baada ya hapo atakwenda wilaya ya mbinga, Songea Manispaa na Songea Vijijini na kuongea na wananchi na kisha  kurejea nyumbani siku ya Jumapili.


No comments:

Post a Comment