Wednesday, October 31, 2012

TAASISI YA MASHEIKH NA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA WATOA TAMKO LAO KUHUSU GHASIA ZILIZIJITOKEZA


                                   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO la jopo la Masheikh na  Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania lililotolewa tarehe 19/01/ 2011,Jijini Dar es Salaam liliwakumbusha watanzania umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria na kutii  amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.
     Jopo la Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania limesikitishwa sana na kitendo cha kunajisiwa Qur’aan Tukufu, Surat Al Waaqia’h (56) Aya ya 76.
Jopo hilo limehuzunishwa na kitendo cha polisi cha kuchelewesha kuchukua hatua za haraka baada ya kitendo hicho kutokea, ambapo kumechangia kuamsha hamasa mbaya na hasira za Waislam.
     Isitoshe Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imesikitishwa na mihemko  hasi na ghadhabu za baadhi ya Waislamu kufanya vitendo mbalimbali vya uhalifu vikiwemo vya uchomaji wa Makanisa na kuharibu mali za watu kwani Uislam hauluhusu mlalamikaji  kujipa haki ya kuhukumu na kuadhibu.
      Aidha Taasisi hiyo imestushwa na baadhi ya matamko ya viongozi wenzao wa Dini ya Kikristo kuitumia kadhia hiyo kuitia doa Uislam na Waislam kitu kitakacho tikisa misingi ya udugu wao na utanzania wao kiasi cha kutamani kuzaliwa ‘ Tanzania mpya’ iliyo fumbo kubwa,na hivyo kuzua hofu juu ya mustakbal wao kama taifa.
       Vilevile Taasisi hiyo haikupendezwa na baadhi ya Waislam kutumia mikusanyiko isiyo halali kupingana na Jeshi la polisi la kutaka kuachiliwa huru wenzao watuhumiwa ambao wako mikononi mwa chombo cha dola.
     Kadhalika Taasisi hiyo imepongea Jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kutuliza ghasia zilizojitokeza bila ya kutoa uhai wa mtanzania yeyote,pia kwa Masheikh na Maimamu na waislam wote waliyonyesha utulivu mkubwa katika kipindi kile kigumu.( Source  Sheikh Khamis Mataka katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania – Gazeti la Tazama Tanzania )

No comments:

Post a Comment