Tuesday, October 30, 2012

BAADA YA KUADIMIKA KWA SIKU KADHAA SASA NAJA NA UHABA WA MAJI ,PETROL NA DIZELI WAIKUMBA MANISPAA YA SONGEA KWA MUDA MREFU SASA

 Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma mwaka huu imekumbwa na uhaba wa maji baada ya vyanzo vya maji katika msitu wa Matogoro kukauka,kabisa lakini wataalamu wa mazingira wanadai kuwa kuna miti ambayo siyo rafiki wa maji  iliyopandwa katika msitu huo sasa imekuwa mikubwa na inanyonya maji yote yaliyopo ardhini.
kutokana na hilo maji yamekauka.hivyo wananchi wa Manispaa hiyo wanatumia maji yanayo uzwa na vijana wa yeboyebo na mikokoteni,bila ya kuelewa kuwa na maji salama ama la,yote ni kumwachia Mungu.
Wakati maji yame adimika katika Manispaa ya Songea , tatizo jingine limejitokeza la uhaba wa mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa.yanapo patikana ni foleni kwenda mbele Blog hii kesho itakuletea foleni hizo.

No comments:

Post a Comment