Saturday, October 6, 2012

MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM KARIBU UTAPUNGUA KUTOKANA NA UPANUZI WA BARABARA KUTOKA JANGWANI HADI MBEZI

 Ujenzi kutoka Magomeni Mapipa Jijini Dar es Salaam  Manzese Darajani ( na Christian Sikapundwa )
Ujenzi kuelekea Ubungo ukiwa manzese Darajani Jijini Dar es Salaam ,Ni kwa kiasi gani serikali ilivyo pania kupunguza msongamano wa magari Jijini kama unavyo shuhudia.
Barabara zikionekana kutokea Magomeni Mapipa kuelekea Ubungo.


Jitihada za Serikali za kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam zinaanza kuonyesha matunda.
Jitihada hizo zimeonekana katika maneo ya magomeni Mapipa ambapo kampuni inayojenga barabara imeweka kambi yake maeneo ya Jangwani inayo panua barabara hadi  Mbezi,nakwamba barabara hizo zikikamilika foleni ya magari katika Jiji hilo itapungua,hasa wakati wa asubuhi watu wakienda kazini na nyakati za alasiri watu wakitoka kazini kurudi nyumbani kwao.
Hayo ni majibu yanayotokana na ahadi za serikali ya Awamu ya nne wakati wa kunadi sera zake kupitia Chama Tawala.Na mwenye macho haambiwi tazama.

No comments:

Post a Comment