Saturday, October 6, 2012

STENDI YA MABASI YA MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA SASA YA HAMIA VIWANJA VYA NANE NANE,BAADA YA MAMLAKA YA USTAWISHAJI WA MJI CDA KUTIFUA STENDI YA ZAMANI KWA GREDA ILI MABASI YASIENDELEE KUSIMAMA HAPO KWA KUKAIDI AMRI ILIYOTOLEWA NA MAMLAKA HAYO

 Hiyo ndiyo stendi ya mabasi mkoani Dodoma iliyoko maeneo ya Kisasa,katika viwanja vya nanenane,kuelekea Dar es Salaam,kati ya Ihumwa na Kisasa.
Baada ya muda kadhaa makao makuu ya nchi kukosa stendi ya kudumu na kuwa na stendi za muda katika maeneo  ya Reli karibu na Bohari ya Serikali mjini hapo sasa imehamishiwa Kisasa katika viwanja vya nanenane.Iwapo wataijenga kwa hadhi ya Stendi basi  eneo hilo ni zuri maana lipo ndani ya uwanja wa Nane nane.Tunawatakia wenye dhamana kufanikisha azma hiyo ili makao makuu yapate heshima yake.

No comments:

Post a Comment