Thursday, September 20, 2012

JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA MANISPAA YA SONGEA KUFANYIKA MWEZI UJAO BADALA YA MWEZI SEPTEMBA KWA SABABU YA ZOEZI LA SENSA KITAIFA.

Afisaelimu Watu Wazima Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Faraja Yonas.


AFISAELIMU Watu Wazima  Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Faraja Yonas amesema kuwa Maazimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima huazimishwa kila mwaka kuanzia tarehe moja mwezi wa tisa hadi tarehe 8 mwezi wa tisa ambapo ni kilele Duniani.
Bw, Yonas alisema sherehe hizo zimepelekwa mbele kuanzia tarehe 29/9/2012 hadi tarehe 4/10 2012 ambayo ndiyo kilele,sherehe hizo zitafanyika katika Kata ya Seed Farm Manispaa Songea.
Alisema siku hiyo kikundi cha MUKEJA cha Mtazamo kinachojishughulisha na kilimo na ufugaji kitasheherekea kutimiza miaka 10 ya ufugaji wa ng’ombe wa naziwa.
Aidha alisema kutakuwepo na maonyesho ya vikundi darasa vya kilimo na ufugaji ambapo vizizi vitano ( 5 ) vya ng’ombe wa maziwa vitaonyeshwa,vikundi vitano ( 5 ) wageni waalikwa pamoja na ngonjera ya watoto wenye umri wa miaka 10 ,ambapo kikundi hicho kitatoa lita moja  kwa kila mtoto kwa watoto 100 wenye umri huo wa shule ya msingi Ruhila Seko.
Baadaye kutakuwepo na ligi ya mpira kwa timu 20 ya kushindania mbuzi washiriki watapata vyeti sambamba na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa nao watapata vyeti.Nakwamba kikundi hicho kimeanda T – Shirt  250.
Siku hiyo pia kutatolewa mafunzo ya UKIMWI na Kuzuia Rushwa kwa wana vikundi wa MUKEJA wa Seed Farm.

No comments:

Post a Comment