Sunday, September 2, 2012

KIFO CHA MWANAHABARI NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI HAYATI DAUD MWANGOSI NI KIFO CHA KISHUJAA ,LAKINI PIA POLISI IJIFUNZE MADHARA YA KUTUMIA NGUVU KUBWA KUZUIA VURUGU ZA KISIASA NCHINI

Mwenyekiti wa Press Club Iringa na mwandishi wa Channel Ten Bw.Daud Mwangosi apoteza maisha yake akiwa kazini kufuatia polisi kuzuia vurugu zilizo sababishwa na wafuasi wa Chama cha Chadema katika ofisi yao katika Kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa jana Jioni.Kufuatua vurugu hizo askari mmoja alijeruhiwa kwa risasi.
Hivyo tunapelekwa wapi ,ni uroho wa madaraka au tusemeje, na matumisi ya silaha za moto katika kuzuia vurugu  kunatupa picha gani.Hata mwezi hauja pita mwananchi asiye na hatia amepoteza maisha yake Mkoani Morogoro kwa Wafuasi wa Chama cha Chadema na Polisi,leo Iringa,Hivyo Hawa Chadema wana maswahibu gani.Kwanini wasisubiri mpaka zoezi la sensa ya watu na makazi limalizike ndipo waendelee na maandamano yao.
Hivyo kufanya hivyo hawaoni kuwa wanawatishia  Amani wananchi ambao wanatarajia kuwatawala? kwanini wasiheshimu sheria zilizowekwa ili kutunza uvunjifu wa amani ?.Polisi nao hawoni athari ya kutumia nguvu kubwa mmno katika kutuliza ghasia,Hawajifunzi ,kwanini watu wasiyo na hatia wanapigwa na polisi hao.Ingependeza kusikia wamemuua kiongozi wa chama Chenyewe.
Hivyo wanataka watu wasifanye kazi zao,Hayati Mwangosi kafa kishujaa akishuhudia makundi mawili yasiyojifunza kutokana na kasoro zinazofanywa na makundi hayo ya kusababisha vifo kwa watu wasiyo na hatia.Jamii ya Tasnia ya habari inasikitishwa sana kwa kumpoteza mwenzao kutokana na matumizi makubwa ya vyombo vya dola na Uroho wa madaraka ya wafuasi wa Chama cha Chadema.Mungu aiweke roho ya Hayati Mwangosi mahali pema Peponi ' Amina' ( Source Blogger Michuzi ) 
 Wakari huo huo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Kamanda Kamuhanda amewataka maandamano yaina yoyote yasifanyike mkoani humo hadi zoezi la sensa ya watu na makazi litakapo kwisha tarehe 8/9/2012.wakati akihojiwa na waandishi wa habari kufuatia ,nguvu zilizochukuliwa na jeshi lake kuzuia vurugu ya wafuasi wa Chadema Nyololo Mufindi Iringa Jana.

No comments:

Post a Comment