Tuesday, September 11, 2012

WAKATI MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI NCHI NZIMA YAMEFANYIKA ,VIONGOZI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI RUVUMA WAINGIA MITINI/MAFICHONI ILI WASIHUSIKE NA MAANDAMANO HAYO

Hiyo ndiyo timu ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma ambao viongozi wao waliiingia mafichoni ili wasijulikane kuwa wamesababisha maandamano hayo kwa lengo la kujisafisha kwa watu wanaowatambua wao.
lakini siwezi kuwalaumu ,ni waandishi wenyewe mkoani hapo wajilaumu binafsi,kwa kawida kuwa kiongozi wa Club uwe mwandishi na siyo kuwa na chama ndani yake huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.Ni lazima kuchagua moja kuwa mwandishi wa habari au kuwa mwanasiasa.
Tuiko hili linamgusa kila raia wa nchi hii na Dunia,kwa huwa hakuna mtu mwenye kuwa na uwezo wa kucheza na uhai wa mtu isipokuwa Mungu peke yake.
Ninani anayeweza kuvumilia ukatili huu uliyofanywa na Askari mkoani Iringa

Ukweli picha kama hizi hatupendi kuzitoa lakini kwa hili ,imetulazimu kuitoa ili wano sikia maandamano ya waandishi hao siyo ya kutaka ila ni kilio cha mwenzao huyo hapo juu ,huo ndio mwili wa Marehemu David Mwangozi wa Iringa.
Hivyo ni nani mwenye moyo mwepesi wa kuvumilia mauaji kama hayo? Hivyo watoto wa marehemu mwangosi waone baba yao alivyo ,hatambuliki,kinacho onekana hapo ni mkono ambao alishikia Camera ,ambayo imechukuliwa na Jeshi hilo.Kilio cha waandishi ni kwa Serikali na Jeshi la polisi,wakimtaka IGP amwajibishe kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa.Tamlo la waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera.
Bomu hilo lilikuwa kubwa na siyo bomu la ,achozi,toka lini bomu la machozi linamchakaza mtu hivyo.E Mungu iweke roho ya Marehemu huyo Mwangosi mahali pema peponi Amina.Kafa kazini maskini wa Mungu,

1 comment:

  1. kWA KWELI INASIKITISHA NA INAGOPESHA KUONA TANZANIA YETU IMEKUWA HIVI..CHUKI ZIMEZAGAA MIOYONI MWETU. pOLENI SANA WANA FAMILIA NA WAANDISHI WOTE WA HABARI ..HAPA INAONYESHA HATUWEZI KUWAAMINI POLISI. WENGI TUNADHANI POLISI KAZI YAO NI KUWATETEA WANANCHI SIO KUWAUA..

    ReplyDelete