Sunday, September 9, 2012

PAMOJA NA CHANGAMOTO ZA MKUTANO YA KATIBA WANANCHI WANAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE MIKUTANO NA KUTOA MAONIYAO MKOANI RUVUMA

Profesa Mwesiga L.Baregu wa kwanza kushoto mwenye shati mikono mirefu kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume wa Taifa Jaji Sinde Wariyoba,akiongea na vyombo vya habari mkoani Ruvuma katika Ukumbi wa Seed Far Hotel leo kuhusu mikutani ya Tume ya mabadiliko ya katiba iliyoanza tarehe 27/8/2012 hadi tarehe 28/9/2012 Mkoani Ruvuma.
Waandhishi kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Timu ya tano mkoani Ruvuma Prof. Baregu
Mwandishi wa TBC Songea akiwa kazini.
Prof.Baregu akisoma taarifa ya ukusanyaji wa maoni kutoka Wilaya za Tunduru na Namtumbo Mkoani Ruruma
Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Joseph Mkirikiti wa kwanza mwenye kaunda suti buluu akiandika mambo muhimu kutoka kwa mwenyekiti wa timu hiyo.



Tume imekumbana na changamoto kadhaa katika ukusanyaji wamaoni Mkoani Ruvuma ,tangu ilivyo anza tarehe 27/8/2012 kwamujibu wa taarira ya Tume kwa vyombo vya habari leo.

MWENYEKITI wa Tume ya madiliko ya Katiba Mkoani Ruvuma Prof.Mwesiga L. Baregu alisema hayo kwa vyombo vya habari mkoani humo kuwa Tumeimeanza kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuanzia tarehe 27/8/2012 haditarehe 28/9/2012,ikiwa ni pamoja na kwenda katika mikoa mingie sita yaMbeya,Morogoro,Kigoma,Mwanza,lindi na Katavi.
Prof. Baregu alisema kuwepo kwa Tume hiyo ni kutaka wananchiwaelewe uwepo wao katika mkoa wa Ruvuma, kutoa taarifa ukusanyaji wa maoniMkoani Ruvuma na kuwaomb wananchi uchirikiano wa kutosha katika kufanikishajukumu hilo lakitaifa.
Aidha Pref. baregu alitaja changamoto walizo kutana nazokatika Wilaya za Tunduru na Nmtumbo,kuwa ni pamoja na idadi ndogo ya wanawakewanaojitokeza katika mikutano sambamba na idadi ndogo ya uchangiaji wa kutoamaoni yaokatika mabadiliko ya Katiba. Ikilinganishwa na wanaume.
Alisema kuwa Tume inatarajia kufanya mikutano 72 katikajumla ya kata 72 katika wilaya tano zaTunduru,Namtumbo,Nyasa,Mbinga na SongeaManispaa na Songea Vijijini.Na kwamba Tume imeshakamilisha mikutano 21 katikawilaya za Tunduru na Namtumbo ambapo wananchi 8,915 walihudhuria katikamikutano hiyo.
Alisema kati ya wananchi 8,915 waliyohudhuria katikamikutano hiyo wanawake walikuwa 1,949 sawa na asilimia 22 na wanaume 8,915 sawana asilimia 78.na kwamba wananchi 2,074 ndiyo walitoa maoni yao katika mikutanohiyo 21 ikiwa sawa na asilimia23.3 ya waliyo hudhuria na katika idadi hiyowanawake ni 198 sawa na asilimia 9.5.
Alisema wananchi waliweza kutoa maoni yao moja kwa moja mbele ta Tume na wenginekwa maandishi kutokana na muda usiyotosha kwa kila mwananchi kuchangia maoniyake mbele ya Tume hiyo.
Tume hiyo inaendelea na mikutano yake katika Wilaya yaSongea Halmashauri za Songea Vijijini,Mmanispaa na hatimaye ,Ziwa Nyasa naMbinga.
Tume imebaini kuwepo kwa idadi ndogo ya wanawakewanaohudhuria mikutano ya Tume,idadi ndogo ya wanawake katika kutoa maonikwenye mikutano hiyo,idadi ndogo ya wananchi wanaochangia katika mikutano hiyona wananchi kujiona hawaelewi katiba iliyopo kwa hiyo hawana cha kuchangiakatika katiba mpya.
Hivyo mwenyekiti wa kundi la tano Prof. Mwesiga L.Baregualisema Tume imeshukuru Tasisi mbalimbali za serikali zilizopo mkoani humo na wananchi wote wanaofika katikamikutano hiyo na kutoa maoni yao waendelee hivyobila ya uoga wowote ili kupata katiba yenye maoni ya wananchi wenyewe wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment