Sunday, September 2, 2012

HAKUNA VITA KATI YA TANZANIA NA ,MALAWI WANANCHI WAMETAKIWA KUONDOA HOFU – KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete alizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ikiwa ni taratibu yake aliyojiwekea ya kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.Ambapo alizungumzia mafanikio ya zoezi la sensa ya watu na makazi na tamko la suluhisho la mpaka wa Ziwa Nyasa.
Bendera ya taifa.
Rais Kikwete azungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam.



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya MrishoKikwete wamewataka wananchi kuondoa hofu ya kuwepo kwa vita kati ya nchi hizimbili majirani Tanzania na Malawi,kwani ni majirani pia ni marafiki na kwambawananchi wametakiwa kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa bila wasiwasi.
Aidha Rais ameongezea kusema kuwa matatizo hayo yoteyametokana na wakoloni wakati wakigawa mipaka ya kuigawa Afrika,ambapo walidaikuwa mpaka wa Malawi upo katikaufukwe wa Tanzaniakitu ambacho siyo sahihi,mipaka ya kimataifa ni katikati ya ziwa.
Isitoshe alisema maji nizawadi iliyotolewa na Mungu kwa binadamu,hivyo kuwanyima majiwananchi wanaoishi pembezoni mwa maziwa ni kuwanyima haki zao za kimsingi.Nahiyo mazungumzo yanaendelea ya suluhisho la mipaka ya Ziwa Nyaza iliyo fuatiamazungumzo kwa mara tatu kufanyika ya kutafuta suluhisho hilo bila mafanikio.
Ametoa angalizo kwa Vyombo ya Habari na viong0zi wa Vyama vya siasa kuacha kuongeza maneno ambayo yataharibumazungumzo ya kuleta mwafaka wa suluhisho la mgogoro uliyojitokeza hivikaribuni.

No comments:

Post a Comment