Thursday, August 30, 2012

BWANA JUMA NYUMAYO AKARIBISHA WAFANYA KAZI WENZAKE NA WAGENI ENGINE NYUMBANI KWAO KWENYE MSIBA WA MKE WA MDOGOWAKE ASKARI WA JWTZ MSHANGANO JANA

 Bwana Juma Nyumayo akiwaonyesha sehamu ya kukaa,wageni na wafanyakazi wenzake wa ofisi ya TUJIFUNZE jana kwenye mazishi ya mpendwa shemeji yake mke wa mdogowake ambaye ni askari wa JWTZ yaliyo fanyika kwenye makaburi ya nyumbani kwao Mshangano.
 Ili kuwa na ulinzi wa kutosha Bw.Nyumayo alikuwa akimwelekeza kitu mbwa wake nje ya kibanda chake hapo jana baada ya mazishi.
Hapa viongozi wa Dini pamoja na Bw.Nyumayoa wakiandaa Sanda kwa ajili ya kwenda kuuvesha mwili wa marehemu.
Ndani ya chumba ambamo baadhi ya akina mama wafiwa walikuwa akimfariji mama mfiwa hapo jana kabla ya mazishi.
 Hapo ni eneo la makaburi ambapo vijana hao wanaonekana wakiandaa mahali ambapo marehemu atakapo hifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele.Na roho ya Marehemu Mama Juma ipunzike kwa amani mahali pema peponi Amen.


Chumba ambapa baadhi ya akina mama wafiwa wakimfariji mama mzazi wa marehemu Mama Juma watatu kutoka kulia aliyefunga kitambaa kichwani na shuka jekundu.Mama Malika.

1 comment:

  1. Poleni sana kwa msiba.tupo pamoja katika maombi na mwenyezi Mungu awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete