Sunday, August 26, 2012

ZOEZI LA SENSA KATIKA MANISPAA YA SONGEA LIMEANZA VIZURI - KATIKA MTAA WA SABASABA MATARAWE NA MARIA KIBUMU

 Karani wa Sensa akijaza mambo muhimu kwa mkuu wa kaya katika mtaa wa Sabasaba Matarawe Manispaa ya Songea saa 1.30 leo.
 Karani wa Sensa Bi. Maria Kibumu akiendelea kujaza taarifa muhimu za mkuu wa kaya ndani ya uwanja wa Sabasaba leo.
 Wa kwanza kushoto ni Mjumbe Mzee Razalo Luambano akiwa na Karani wa Sensa Bi. Maria Kibumu kuhakikisha zoezi hilo linaenda vizuri.
 Bi.Maria kibumu alisema kuwa hajapambana na tatizo lolote katika zoezi hilo katika mtaa wake ,ipokuwa siku tatu za nyuma alicheleweshwa kupata idadi ya watoto wa shule ya watoto wadogo ya Charity iliyoko ndani ya uwanja wa Sabasaba.
Sensa ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa na watu wake,hivyo watu ambao wanashabikia watu wasihesabiwe,ni kosa watu kama hao si wema wa Taifa letu linye sifa tele ya Amani na utulivu miongoni mwa wananchi wake.
Sera ya nchi ni Sera isiyokuwa na udini,ukabila, rangi ama Itikadi,ila ni Sera inayo jali maendeleo ya kila mwananchi kwa Itikadi yoyote,Imani yoyote.

No comments:

Post a Comment