Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aongea na wananchi kupitia vyombo vya habari ,kama kaida yake kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa kuhesabiwa katika Sensa iliyoanza saa 6 usiku kwa wasafiri na wenye mazingira magumu.
RAIS wa Jamhuri ya Tanzania Dr.Jakaya Kikwete amewaasa
wananchi kujitokeza katika sensa iliyoanza jana usiku kwa wasafiri na watu walioko katika mazingira
magumu,kuhesabiwa na kuwapa ushirikiano wa kutosha Makarani wa Sena,na kwamba
madai ya kurudishwa mifupa ya Mjunsi iliyoko Ujerumani,na madai ya viongozi na
wanaharakati wa Dini ya kiislamu ya Takwimu zilizotolewa na mashirika visiwe
vigezo vya kususia Sensa.
Alisema kuwa kususia sensa kwa sababu hizo ni kutoitendea
haki serikali,kwa kuwa taarifa za Takwimu zinatolewa na ofisi ya Taifa ya Sensa
na siyo ya mashirika.na katika sensa hakuna masuala ya udini au rangi,Sera yetu
haiusiki na sera za ubaguzi wa rangi au udini kama ilivyo wakati wa Ukoloni,kwa
kuwa wakoloni walikuwa na Sera za ubaguzi.
Hivyo Rais amewataka wananchi kushiriki katika Sensa kwa
maendeleo ya Taifa letu na si vingine,Aidha amewataka viongozi wa
vyama,Serikali kusimamia zoezi hili lifanikiwe katika maeneo yao.
Katika Mkoa wa Ruvuma zoezi hilo limeanza ,ambapo makarani
wa Sensa wameshapata vifaa vyote vinavyo husiana na zoezi hili na hivi sapo
katika kuhesabu watu katika kata zao.Ikiwemo Mtaa wa Sabasaba na nje ya uwanja
wa sabasaba Matarawe manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Katani wa Sensa Bi. Maria
Kibumu na Mjumbe wake Razalo Luambano
wamesha pitia zaidi ya kaya 5 na wanasema hawaja kumbana na matatizo yoyote
hadi muda tuna kwenda mitamboni.
No comments:
Post a Comment