Tuesday, August 14, 2012

WANAFUNZI 20 WATUNUKIWA ZAWADI KWA UFAULU WA DARAJA LA KWANZA KIDATO CHA SITA MWAKA 2012



WANAFUNZI 20 walifanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita mwaka huu wametunukiwa zawadi na Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,kati yao Wavulana 10 na Wasichana 10 kutoka katika shule kumi bora nchini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Shukuru Kawambwa kuwa zawadi hizo ni pamoja na Cheti, Laptop na shilingi 200,000 kila mmoja kutokana na kufanya vizuri katika masomo ya sayansi,Mhe. Kawambwa alisema kuwa wanafunzi hao wametoka katika shule 8  za Serikali na mbili ( 2 ) kutoka shule binafsi ,amezitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule za sekondari za Kibaha,Mpwapwa,Mzumbe,Kilakala,Ifunda,Fedha,Mariani,Tabora , Minaki na Tabora wasichana.
Aidha shule 10 zilizofanya vizuri katika masomo zimezawadiwa shilingi milioni moja kila shule,ambapo zawadi hizo zitatolewa na Waziri Mkuu Mhe. Pinda kwa wakuu wa shule hizo jioni hii leo.

No comments:

Post a Comment