TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
TAMKO la jopo la Masheikh
na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania
lililotolewa tarehe 19/01/ 2011,Jijini Dar es Salaam liliwakumbusha watanzania
umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa
katiba na sheria za nchi.
Jopo la Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania limesikitishwa sana na kitendo cha kunajisiwa Qur’aan
Tukufu, Surat Al Waaqia’h (56) Aya ya 76.
Jopo hilo limehuzunishwa na kitendo cha polisi cha
kuchelewesha kuchukua hatua za haraka baada ya kitendo hicho kutokea, ambapo
kumechangia kuamsha hamasa mbaya na hasira za Waislam.
Isitoshe Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni
wa Kiislamu Tanzania imesikitishwa na mihemko
hasi na ghadhabu za baadhi ya Waislamu kufanya vitendo mbalimbali vya
uhalifu vikiwemo vya uchomaji wa Makanisa na kuharibu mali za watu kwani Uislam
hauluhusu mlalamikaji kujipa haki ya
kuhukumu na kuadhibu.
Aidha Taasisi hiyo imestushwa na baadhi
ya matamko ya viongozi wenzao wa Dini ya Kikristo kuitumia kadhia hiyo kuitia
doa Uislam na Waislam kitu kitakacho tikisa misingi ya udugu wao na utanzania
wao kiasi cha kutamani kuzaliwa ‘ Tanzania
mpya’ iliyo fumbo kubwa,na hivyo kuzua hofu juu ya mustakbal wao kama taifa.
Vilevile Taasisi hiyo haikupendezwa na
baadhi ya Waislam kutumia mikusanyiko isiyo halali kupingana na Jeshi la polisi
la kutaka kuachiliwa huru wenzao watuhumiwa ambao wako mikononi mwa chombo cha
dola.
Kadhalika Taasisi hiyo imepongea Jeshi la
polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kutuliza ghasia zilizojitokeza bila ya
kutoa uhai wa mtanzania yeyote,pia kwa Masheikh na Maimamu na waislam wote
waliyonyesha utulivu mkubwa katika kipindi kile kigumu.( Source Sheikh Khamis Mataka katibu Mkuu wa Taasisi
ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania – Gazeti la Tazama Tanzania )