Thursday, September 20, 2012

JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA MANISPAA YA SONGEA KUFANYIKA MWEZI UJAO BADALA YA MWEZI SEPTEMBA KWA SABABU YA ZOEZI LA SENSA KITAIFA.

Afisaelimu Watu Wazima Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Faraja Yonas.


AFISAELIMU Watu Wazima  Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Faraja Yonas amesema kuwa Maazimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima huazimishwa kila mwaka kuanzia tarehe moja mwezi wa tisa hadi tarehe 8 mwezi wa tisa ambapo ni kilele Duniani.
Bw, Yonas alisema sherehe hizo zimepelekwa mbele kuanzia tarehe 29/9/2012 hadi tarehe 4/10 2012 ambayo ndiyo kilele,sherehe hizo zitafanyika katika Kata ya Seed Farm Manispaa Songea.
Alisema siku hiyo kikundi cha MUKEJA cha Mtazamo kinachojishughulisha na kilimo na ufugaji kitasheherekea kutimiza miaka 10 ya ufugaji wa ng’ombe wa naziwa.
Aidha alisema kutakuwepo na maonyesho ya vikundi darasa vya kilimo na ufugaji ambapo vizizi vitano ( 5 ) vya ng’ombe wa maziwa vitaonyeshwa,vikundi vitano ( 5 ) wageni waalikwa pamoja na ngonjera ya watoto wenye umri wa miaka 10 ,ambapo kikundi hicho kitatoa lita moja  kwa kila mtoto kwa watoto 100 wenye umri huo wa shule ya msingi Ruhila Seko.
Baadaye kutakuwepo na ligi ya mpira kwa timu 20 ya kushindania mbuzi washiriki watapata vyeti sambamba na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa nao watapata vyeti.Nakwamba kikundi hicho kimeanda T – Shirt  250.
Siku hiyo pia kutatolewa mafunzo ya UKIMWI na Kuzuia Rushwa kwa wana vikundi wa MUKEJA wa Seed Farm.

Wednesday, September 19, 2012

TUKO PAMOJA KATIKA MTANDAO HUU,WALA SIKO LIKIZO BALI NI KUJIPUMZISHA KWANZA TUKIWA NA WAGENI WA IDARA YA ELIMU YA WATU ZAIMA MANISPAA YA SONGEA

Mhariri msaidizi  wa TUJIFUNZE Bwana Juma Nyumayo mwenye suti nyeusi akiongea na Timu nzima ya Idara ya Elimu ya Watu Wazimak atika ofisi ya  TUJIFUNZE walipotembelea ofisi hiyo hivi karibuni,kwa lengo la kuelezea maandalizi ya Juma la Elimu ya Watu Wazima litakalofanyika mapema mwezi ujao katika kata ya Seed farm katika Manispaa ya Songea.Ambapo kikundi cha MUKEJA cha Ufugaji ng'ombe wa maziwa kinatimiza miaka 10.
 Afisa Elimu Vielelezo Bw.Mpangala akiandika mambo muhimu ambayo yatafanyika katika wiki hilo,ikiwemo michezo na burudani mbalimbali.
 Picha ya Pamoja ya Maafisa hao ndani wakiwa na Mhariri msaidizi Bw.Nyumayo ndani.( Picha na Bw.Juma Nyumayo)
Picha ya pamoja nje ya Ofisi  ya Maafisa Elimu Idara  ya Elimu ya Watu Wazima ( Adult of Education Section Songea Municipal }
Aidha katika Juma hilo kikundi cha wafugajimng'omge wa maziwa watawapatia matoto  wasiopungua 100 wa darasa la Tatu lita mojamoja za maziwa wenye umri wa miaka 10 katika shule ya msingi Luhira Seko katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.( Picha na Christian Sikapundwa ).

Tuesday, September 11, 2012

WAKATI MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI NCHI NZIMA YAMEFANYIKA ,VIONGOZI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI RUVUMA WAINGIA MITINI/MAFICHONI ILI WASIHUSIKE NA MAANDAMANO HAYO

Hiyo ndiyo timu ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma ambao viongozi wao waliiingia mafichoni ili wasijulikane kuwa wamesababisha maandamano hayo kwa lengo la kujisafisha kwa watu wanaowatambua wao.
lakini siwezi kuwalaumu ,ni waandishi wenyewe mkoani hapo wajilaumu binafsi,kwa kawida kuwa kiongozi wa Club uwe mwandishi na siyo kuwa na chama ndani yake huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.Ni lazima kuchagua moja kuwa mwandishi wa habari au kuwa mwanasiasa.
Tuiko hili linamgusa kila raia wa nchi hii na Dunia,kwa huwa hakuna mtu mwenye kuwa na uwezo wa kucheza na uhai wa mtu isipokuwa Mungu peke yake.
Ninani anayeweza kuvumilia ukatili huu uliyofanywa na Askari mkoani Iringa

Ukweli picha kama hizi hatupendi kuzitoa lakini kwa hili ,imetulazimu kuitoa ili wano sikia maandamano ya waandishi hao siyo ya kutaka ila ni kilio cha mwenzao huyo hapo juu ,huo ndio mwili wa Marehemu David Mwangozi wa Iringa.
Hivyo ni nani mwenye moyo mwepesi wa kuvumilia mauaji kama hayo? Hivyo watoto wa marehemu mwangosi waone baba yao alivyo ,hatambuliki,kinacho onekana hapo ni mkono ambao alishikia Camera ,ambayo imechukuliwa na Jeshi hilo.Kilio cha waandishi ni kwa Serikali na Jeshi la polisi,wakimtaka IGP amwajibishe kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa.Tamlo la waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera.
Bomu hilo lilikuwa kubwa na siyo bomu la ,achozi,toka lini bomu la machozi linamchakaza mtu hivyo.E Mungu iweke roho ya Marehemu huyo Mwangosi mahali pema peponi Amina.Kafa kazini maskini wa Mungu,

MAANDAMANO YA AMANI YA WAANDISHI WA HABARI NCHINI ,KAGERA WAMTAKA KAMUHANDA KAMANDA WA IRINGA KUJIUZURU

 Maandamano ya waandishi wa habari ya amani kufuatia kifo cha mwandishi mwenzao wa Channel Ten na mwenyekiti wa Iringa Press Club David Mwangosi aliye uliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humi mbele ya kamanda wa Polisi wa mkoa huo Michael Kamuhanda.Wandishi wa habari wa mkoa wa Kagera wanitaka serikali kumwajibisha kanda huyo,na nafasi yake akaimishwa RTO wakati taratibu za kishria zikifanyika.
 Nako mkoani Kilimanjaro waandishi wanalaani vikali mauaji ya kinyama yaliyofanyika Mkoani Iringa ya mwandishi mwenzao,wanasema askari wanakiuka viapo walivyo apa wakiwa katika mafunzo yao kuwa watalinda raia na mali zao,badala yake wanaua raia.wameomba serikali kufuatila mauaji hayo.
Dar es Salaam wandishi uzalendo uliwashinda pale waziri mwenye dhamana alipo taka kwenda kuwasikiliza kumkataa na kutimua kwa kuwa hakuhusika.Dr.Emanuel Nchimbi.wakati amevalia suti nyeupe kwenye msiba wa wanahabari hao,wengine waliwaponda askari kwa maneno makali.
 Lakini je Jeshi la polisi kwa nini wanatumia silaha kubwa kubwa kutuliza ghasia? hivyo bom lililotumika kumlipulia mwandishi huyo ,ilikuwa ni mahali pake? isitoshe mwandishi anasulubiwa na kutekezwa mbele ya Kamanda wa polisi wa mkoa bila ya kukemea,au jeshi hilo mkoani humo walikuwa wanamtafutia kosa la kummaliza.Wanahabari na kalamu zao waliuliza Jeshi la polisi linamchukuliaje kamanda wa polisi wa mkoa huo na muuwaji wake.Familia ya marehemu Mwangosi serikali itawatunza? au la.
Wananchi na waandishi wa habari watashindwa kufanya kazi zao kwa kuwaogopa polisi,Inatisha kusikia kuwa Mwanshi wa Iringa ndiye iliyetoa siri ya askari polisi wetu kwa mauaji ya waandishi wa habari kisirisiri,wapatao 46.Kama ilikuwa ni kutuliza maandamano ya Chama kwanini Bomu hilo wange walipua viongozi wa chama chenyewe,na badala yake kumua mwandishi inasikitisha.Ukweli IGP asema kitu kwa waandishi kuhusu hatima ya matumizi nguvu kubwa katika kutuliza ghasia nchini na viongozi wazembe katika Jeshi lake.Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mwangosi mahali pema peponi Amin.

Sunday, September 9, 2012

PAMOJA NA CHANGAMOTO ZA MKUTANO YA KATIBA WANANCHI WANAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE MIKUTANO NA KUTOA MAONIYAO MKOANI RUVUMA

Profesa Mwesiga L.Baregu wa kwanza kushoto mwenye shati mikono mirefu kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume wa Taifa Jaji Sinde Wariyoba,akiongea na vyombo vya habari mkoani Ruvuma katika Ukumbi wa Seed Far Hotel leo kuhusu mikutani ya Tume ya mabadiliko ya katiba iliyoanza tarehe 27/8/2012 hadi tarehe 28/9/2012 Mkoani Ruvuma.
Waandhishi kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Timu ya tano mkoani Ruvuma Prof. Baregu
Mwandishi wa TBC Songea akiwa kazini.
Prof.Baregu akisoma taarifa ya ukusanyaji wa maoni kutoka Wilaya za Tunduru na Namtumbo Mkoani Ruruma
Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Joseph Mkirikiti wa kwanza mwenye kaunda suti buluu akiandika mambo muhimu kutoka kwa mwenyekiti wa timu hiyo.



Tume imekumbana na changamoto kadhaa katika ukusanyaji wamaoni Mkoani Ruvuma ,tangu ilivyo anza tarehe 27/8/2012 kwamujibu wa taarira ya Tume kwa vyombo vya habari leo.

MWENYEKITI wa Tume ya madiliko ya Katiba Mkoani Ruvuma Prof.Mwesiga L. Baregu alisema hayo kwa vyombo vya habari mkoani humo kuwa Tumeimeanza kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuanzia tarehe 27/8/2012 haditarehe 28/9/2012,ikiwa ni pamoja na kwenda katika mikoa mingie sita yaMbeya,Morogoro,Kigoma,Mwanza,lindi na Katavi.
Prof. Baregu alisema kuwepo kwa Tume hiyo ni kutaka wananchiwaelewe uwepo wao katika mkoa wa Ruvuma, kutoa taarifa ukusanyaji wa maoniMkoani Ruvuma na kuwaomb wananchi uchirikiano wa kutosha katika kufanikishajukumu hilo lakitaifa.
Aidha Pref. baregu alitaja changamoto walizo kutana nazokatika Wilaya za Tunduru na Nmtumbo,kuwa ni pamoja na idadi ndogo ya wanawakewanaojitokeza katika mikutano sambamba na idadi ndogo ya uchangiaji wa kutoamaoni yaokatika mabadiliko ya Katiba. Ikilinganishwa na wanaume.
Alisema kuwa Tume inatarajia kufanya mikutano 72 katikajumla ya kata 72 katika wilaya tano zaTunduru,Namtumbo,Nyasa,Mbinga na SongeaManispaa na Songea Vijijini.Na kwamba Tume imeshakamilisha mikutano 21 katikawilaya za Tunduru na Namtumbo ambapo wananchi 8,915 walihudhuria katikamikutano hiyo.
Alisema kati ya wananchi 8,915 waliyohudhuria katikamikutano hiyo wanawake walikuwa 1,949 sawa na asilimia 22 na wanaume 8,915 sawana asilimia 78.na kwamba wananchi 2,074 ndiyo walitoa maoni yao katika mikutanohiyo 21 ikiwa sawa na asilimia23.3 ya waliyo hudhuria na katika idadi hiyowanawake ni 198 sawa na asilimia 9.5.
Alisema wananchi waliweza kutoa maoni yao moja kwa moja mbele ta Tume na wenginekwa maandishi kutokana na muda usiyotosha kwa kila mwananchi kuchangia maoniyake mbele ya Tume hiyo.
Tume hiyo inaendelea na mikutano yake katika Wilaya yaSongea Halmashauri za Songea Vijijini,Mmanispaa na hatimaye ,Ziwa Nyasa naMbinga.
Tume imebaini kuwepo kwa idadi ndogo ya wanawakewanaohudhuria mikutano ya Tume,idadi ndogo ya wanawake katika kutoa maonikwenye mikutano hiyo,idadi ndogo ya wananchi wanaochangia katika mikutano hiyona wananchi kujiona hawaelewi katiba iliyopo kwa hiyo hawana cha kuchangiakatika katiba mpya.
Hivyo mwenyekiti wa kundi la tano Prof. Mwesiga L.Baregualisema Tume imeshukuru Tasisi mbalimbali za serikali zilizopo mkoani humo na wananchi wote wanaofika katikamikutano hiyo na kutoa maoni yao waendelee hivyobila ya uoga wowote ili kupata katiba yenye maoni ya wananchi wenyewe wa Tanzania.

Sunday, September 2, 2012

KIFO CHA MWANAHABARI NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI HAYATI DAUD MWANGOSI NI KIFO CHA KISHUJAA ,LAKINI PIA POLISI IJIFUNZE MADHARA YA KUTUMIA NGUVU KUBWA KUZUIA VURUGU ZA KISIASA NCHINI

Mwenyekiti wa Press Club Iringa na mwandishi wa Channel Ten Bw.Daud Mwangosi apoteza maisha yake akiwa kazini kufuatia polisi kuzuia vurugu zilizo sababishwa na wafuasi wa Chama cha Chadema katika ofisi yao katika Kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa jana Jioni.Kufuatua vurugu hizo askari mmoja alijeruhiwa kwa risasi.
Hivyo tunapelekwa wapi ,ni uroho wa madaraka au tusemeje, na matumisi ya silaha za moto katika kuzuia vurugu  kunatupa picha gani.Hata mwezi hauja pita mwananchi asiye na hatia amepoteza maisha yake Mkoani Morogoro kwa Wafuasi wa Chama cha Chadema na Polisi,leo Iringa,Hivyo Hawa Chadema wana maswahibu gani.Kwanini wasisubiri mpaka zoezi la sensa ya watu na makazi limalizike ndipo waendelee na maandamano yao.
Hivyo kufanya hivyo hawaoni kuwa wanawatishia  Amani wananchi ambao wanatarajia kuwatawala? kwanini wasiheshimu sheria zilizowekwa ili kutunza uvunjifu wa amani ?.Polisi nao hawoni athari ya kutumia nguvu kubwa mmno katika kutuliza ghasia,Hawajifunzi ,kwanini watu wasiyo na hatia wanapigwa na polisi hao.Ingependeza kusikia wamemuua kiongozi wa chama Chenyewe.
Hivyo wanataka watu wasifanye kazi zao,Hayati Mwangosi kafa kishujaa akishuhudia makundi mawili yasiyojifunza kutokana na kasoro zinazofanywa na makundi hayo ya kusababisha vifo kwa watu wasiyo na hatia.Jamii ya Tasnia ya habari inasikitishwa sana kwa kumpoteza mwenzao kutokana na matumizi makubwa ya vyombo vya dola na Uroho wa madaraka ya wafuasi wa Chama cha Chadema.Mungu aiweke roho ya Hayati Mwangosi mahali pema Peponi ' Amina' ( Source Blogger Michuzi ) 
 Wakari huo huo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Kamanda Kamuhanda amewataka maandamano yaina yoyote yasifanyike mkoani humo hadi zoezi la sensa ya watu na makazi litakapo kwisha tarehe 8/9/2012.wakati akihojiwa na waandishi wa habari kufuatia ,nguvu zilizochukuliwa na jeshi lake kuzuia vurugu ya wafuasi wa Chadema Nyololo Mufindi Iringa Jana.

HAKUNA VITA KATI YA TANZANIA NA ,MALAWI WANANCHI WAMETAKIWA KUONDOA HOFU – KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete alizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ikiwa ni taratibu yake aliyojiwekea ya kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.Ambapo alizungumzia mafanikio ya zoezi la sensa ya watu na makazi na tamko la suluhisho la mpaka wa Ziwa Nyasa.
Bendera ya taifa.
Rais Kikwete azungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam.



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya MrishoKikwete wamewataka wananchi kuondoa hofu ya kuwepo kwa vita kati ya nchi hizimbili majirani Tanzania na Malawi,kwani ni majirani pia ni marafiki na kwambawananchi wametakiwa kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa bila wasiwasi.
Aidha Rais ameongezea kusema kuwa matatizo hayo yoteyametokana na wakoloni wakati wakigawa mipaka ya kuigawa Afrika,ambapo walidaikuwa mpaka wa Malawi upo katikaufukwe wa Tanzaniakitu ambacho siyo sahihi,mipaka ya kimataifa ni katikati ya ziwa.
Isitoshe alisema maji nizawadi iliyotolewa na Mungu kwa binadamu,hivyo kuwanyima majiwananchi wanaoishi pembezoni mwa maziwa ni kuwanyima haki zao za kimsingi.Nahiyo mazungumzo yanaendelea ya suluhisho la mipaka ya Ziwa Nyaza iliyo fuatiamazungumzo kwa mara tatu kufanyika ya kutafuta suluhisho hilo bila mafanikio.
Ametoa angalizo kwa Vyombo ya Habari na viong0zi wa Vyama vya siasa kuacha kuongeza maneno ambayo yataharibumazungumzo ya kuleta mwafaka wa suluhisho la mgogoro uliyojitokeza hivikaribuni.