Wednesday, October 8, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE ,DR. SHEN WAKABIDHIWA KATIBA INAYOPENDEKEZWA MJINI DODOMA MBELE YA MABALOZI MBALIMBALI WALIYO HUDHURIA SHEREHE HIZO

 Rais Jakaya Kikwete na Dr. Shein waonyesha Katiba inayopendekezwa baada ya kukaidhiwa na mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba Mhe.Samweli Sitta katika sherehe ya kukabidhi Katiba katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba Mhe. Samweli Sitta ,kielezea mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa kujadili Rasimu ya Katiba hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete asema Katiba inayopendekezwa ni halali, nzuri na hana wasiwasi nayo.Alisema Katiba ni nzuri haina mfano wake,amesema Katiba iliyomgusa kila mmoja na hali yake.
Aidha alisema Katiba imependekeza mambo megi ya Muugano ya kuwa na Serikali mbili,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka kamili ya kupata mikopo bila Serikali ya Muungano,Kujiunga na Taasisi za kimataifa na kuondoa migogoro ya Muungano.
Kawataka watanzania kuisoma vizuri Katiba hiyo na kuielewa na hatimaye kupiga kura ya ndio.
 Naye mawkilishi wa Kundi la walemavu Mhe. Mpanju amempongeza Rais Kikwete kwa uadilifu wake aliyouonyesha kipindi cha majadiliano ya Ibara mbali mabli kuliko sababisha sintofahamu kadhaa ,kwa baadhi ya wajumbe na kususia lakini aliona kazi itaendelea kwa mujibu wa sheria iliyopangwa.
Alisema katiba hiyo imayajali makundi yote yakiwemo ,walemavu,wakulima,wanawake,wafugaji ,wavuvi,wasanii, na wachimbaji wadogo wadogo.
Baadhi ya wananchi waliyokuwa wakiingia ndani ya uwanja wa Jamhuri kushuhudia  tukio hilo la Kihistoria

No comments:

Post a Comment