Sunday, December 7, 2014

WAJUMBE WA BODI YA "MUTUAL GENERATION OF TANZANIA ( MGT) " IMEWAKILISHA MIRADI YAO MBELE YA WALEZI WAO MIRADI ILIYOFANYIKA NA INAYOTARAJIWA KUFANYWA KATIKA UKUMBI WA 56 KATIKA MANISPAA YA DODOMA NA MWENYEKITI WA MGT BWANA FERDINAND EMILY

 Wajumbe wa BODI ya Mutual Generation of Tanzania ( MGT ) Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao chao kifupi cha kuwakilisha Mirada iliyofanyiwa kazi na inayotarajia kufanyiwa kazi.












Mwanyekiti wa MGT Bw. Ferdinand Emily akilezea malengo ya Mutual Generation of Tanzania ( MGT ) mbele ya walezi  na wajumbe wa Shirika hilo lililoundwa na wanafunzi wa vyuo vikuu vinane Tanzania ambavyo ni Dodoma UDOM, Dar es Salaam UDSM,Chuo cha Elimu ya Biashara CBE, Makumira, Usimamizi wa Fedha  ( IFM), Mipango ( IRDP ) ,SUA na Chuo kikuu cha Jordan
 Walezi wa MGT aliyesimama na kusifu na kuelekeza juhudi za MGT ni Mkurugenzi wa AFNET Sarah D. Mwaga,wa kulia kwake ni Prof. Kalafunja Osaki wa UDOM ,wakatikati ni mwenyekiti wa MGT Bw. Ferdinand Emily , wa kushoto wake ni Bw. Christian Sikapundwa Stationery mkabala na Bohari ya Mkoa wa Dodoma na wanyuma Bi.Zaituni Said Ngwanga Kaimu Mwenyekiti MGT.
 Aliyesimama ni miongoni mwa walezi wa MGT Bi Mirium Zablon wa Sahara Media Group akiwapa moyo wa kujitoa katika kuanzisha Shirika hilo lisilo la Kiserikali la Wasomi waliohitu masomo yao na wale ambao bado wapo masomoni,akito wito kuwa wale ambao hawajajiunga na MGT wajiunge ili wajenge dhana Kujiajiri baada ya masomo yao. Ambapo mpaka sasa wajumbe waliyondani ya MGT ni zaidi ya 1000 idadi ambayo ni ndogo kulingana na idaidi ya wanafunzi wote walioko katika vyuo hivyo vinane nchini.
Wajumbe wa MGT wakisiliza kwa makini ushauri na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na walezi hao moja baada ya mwingine.

MGT imeandaa mradi wa shule ya Sekondari ambayo itawapa fursa kubwa ya kufanya sekodari hiyo iweza kujiendesha yenyewe .Aidha imeanzisha mradi wa ufugaji wa kuku ambao uko tayari kinacho hitajika hapo ninamna ya kupata mtaji. Pia wameandaa miradi mingine itakayo kidhi  mahitaji ya watanzani ikiwemo ufugaji wa nyuki.


No comments:

Post a Comment