Friday, December 19, 2014

438,960 KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015,KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI KWA AWAMU MBILI AMBAPO AWAMU YA KWANZA ASILIMIA 97.23 NA 12,432 WAKOSA NAFASI

Naibu Waziri wa Elimu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Kassim Majaliwa alisema hayo mbele ya vyombo vya Habari hivi karibuni Jijini Dar es Saam ,na kwamba wanafunzi hao ni wale waliyopata daraja la A hadi C.
Alisema wanafunzi waliyokosa nafani katika mikoa ya Dodoma wanafunzi 9,824,Dar es Salaam wanafunzi ,1,414,Morogoro 752,Mtwara 281 na Katavi 161 kwa upungufu wa vyumba vya madarasa.
Aidha alisema kuwa wanafunzi 10,331 wamepata alama za daraja A ambapo wanafunzi 98,789 wamepata alama za daraja B,342,272 wamepata daraja C,321,939 daraja D wakati wanafunzi 18,787 daraja E.
Hatimaye Naibu Waziri huyo ameaasa wanafunzi wote kutumia fursa hiyo kwa kutumia muda wao katika kusoma,pia katoa pongezi kwa wadau wote wa elimu walio fanikisha ufanisi katika matokeo hayo kwakuonyesha alama za juu kwa wavulana ilikuwa 243 na wasichana alama  240 kati ya alama 250 kwa mwaka huu tofauti na mwaka 2013 ilikuwa alama 244.

No comments:

Post a Comment