Sunday, December 7, 2014

MHE. MBOWE ANGURUMA VIWANJA VYA BARAFU MKABALA NA UWANJA WA JAMHURI DODOMA MANISPAA UKITANGULIWA NA MAANDAMANO YA AMANI KUANZIA VIWANJA VYA DODOMA SEKONDARI WAKIGAWA VIPEPERUSHI VYENYE UJUMBE MZITO " OPERESHENI ONDOA CCM DODOMA " OCD

 Hivyo ndivyo vibwagizo vya UKAWA Kwa njia ya vipeperushi vyenye Ujumbe huo,katika harakati za kupata ushindi ndani ya Vyama vya Upinzani ,Hiyo ndiyo michezo ya Siasa.
 Ni maandamano ya Amani yaliyo anzia viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma kuelekea Viwanja vya Barafu Mkabala na Uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Dodoma leo.
Matukio hayo ni kufuatia Maandalizi ya Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mtaa unaotarajia kufanyika nchi nzima hivi karibuni.
 Gari la Matangazo na pikipiki
 Hao ndiyo Makamanda wakiwa na Mtundiko kuashiria kwamba CCM inaondolewa Madarakani na Upinzani inashika madaraka hasa kwa ujumbe wa vipeperushi  vilivyo sambazwa Mjini hapa,Lakini ni  dalili za kujiamini.
 Hayo ni maandamano ya pikipiki ya wanachama wakiwa na bendera za CHADEMA ,CUF na nyingine kutokana na Vyama vilivyounda UKAWA
 Hapa Makamanda wakiwa wana pasha pasha mvuto kwa wananchi kusogea kwenye tukio hilo la Kihistoria kama mtangazaji alivyo kuwa akitangaza kuwa ni tukio la Kihistoria la kuitoa CCM madarakani kwa kuwapa likizo isiyo na malipo, Siasa Inapendeza masikioni.Haya kazi kwao tunawatakia mafankio mema katika safari yao ya Kuiondoa CCM kama vile imelala fo fofo.
Ni baadhi ya Viongozi.Zaidi utapata kutoka viwanja vya Barafu kwenye Magazeti na Luninga.

1 comment:

  1. Shukrani kwa taarifa na picha. Dodoma ni jikoni. Tafadhali endelea kutuletea habari za yanayotokea huko.

    ReplyDelete