Thursday, December 25, 2014

IBADA ZA CHRISTMASS MJINI DODOMA ZIMEFANA SANA NA ZIMETAWALIWA NA MAHUBILI YALIYOSHEHENI AMANI,UPANDO NA MSHIKAMANO PAMOJA NA KUWAKUMBUSHA WAUMINI HAO KUJITOKEZA KWA WINGI WAKATI WA UCHAGUZI WA WABUNGE NA URAIS,BAADA YA IBADA NI KUWA PAMOJA NA FAMILIA NYUMANI KWA VYAKULA NA VINYWAJI NA WATOTO

Wajukuu wa kwanza kushoto ni  Karen Michael Sikapundwa  na wapili ni Ester Emanuel Sikapundwa wakisheherekea Christmass kwa soda na chakula .Hivyo ndivyo ilivyo kama picha zote zinavyo someka.
Bibi Chris Baby Boy Emanuel akiwa na Mjukuu wake
Karen & Ester
Bwana Emanuel Sikapundwa Na Mtarajiwa wake na watoto wao Ester & Chris Baby Boy na Karen Michael Sikapundwa
Mr& Mrs Neson Mwakyusa na Familia yake siku ya Christmass tarehe 25/12/204 Dodoma


Mr.Mwakyusa Watoto na Wajukuu siku ya Christmass Mjini Dodoma






















Wednesday, December 24, 2014

BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI INAWATAKIWA WAUMINI WA KIKRISTO KOTE DUNIANI MKESHA WA CHRISTMASS NA HERI YA MWAKA MPYA WA 2015.PIA KUSHEREHEKEA KWA AMANI NA UTULIVU.NI MATUMAINI YANGU VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI HAUTA KUWEPO.

Nina mshukuru Mungu kwa kunilinda pamoja na Familia yangu ya Sikapundwa kuwa na afya njema.Bloggers wote heri ya Christmass na Mwaka Mpya wa 2015.
Tusheherekee kwa amani na Utulivu wanaokwenda kwenye Ibada ya Usiku wasiondoke wote nyumbani maana wengie hutumia mwanya wa sikukuu hizi kufanya uhalifu.

Friday, December 19, 2014

438,960 KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015,KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI KWA AWAMU MBILI AMBAPO AWAMU YA KWANZA ASILIMIA 97.23 NA 12,432 WAKOSA NAFASI

Naibu Waziri wa Elimu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Kassim Majaliwa alisema hayo mbele ya vyombo vya Habari hivi karibuni Jijini Dar es Saam ,na kwamba wanafunzi hao ni wale waliyopata daraja la A hadi C.
Alisema wanafunzi waliyokosa nafani katika mikoa ya Dodoma wanafunzi 9,824,Dar es Salaam wanafunzi ,1,414,Morogoro 752,Mtwara 281 na Katavi 161 kwa upungufu wa vyumba vya madarasa.
Aidha alisema kuwa wanafunzi 10,331 wamepata alama za daraja A ambapo wanafunzi 98,789 wamepata alama za daraja B,342,272 wamepata daraja C,321,939 daraja D wakati wanafunzi 18,787 daraja E.
Hatimaye Naibu Waziri huyo ameaasa wanafunzi wote kutumia fursa hiyo kwa kutumia muda wao katika kusoma,pia katoa pongezi kwa wadau wote wa elimu walio fanikisha ufanisi katika matokeo hayo kwakuonyesha alama za juu kwa wavulana ilikuwa 243 na wasichana alama  240 kati ya alama 250 kwa mwaka huu tofauti na mwaka 2013 ilikuwa alama 244.

Sunday, December 7, 2014

MHE. MBOWE ANGURUMA VIWANJA VYA BARAFU MKABALA NA UWANJA WA JAMHURI DODOMA MANISPAA UKITANGULIWA NA MAANDAMANO YA AMANI KUANZIA VIWANJA VYA DODOMA SEKONDARI WAKIGAWA VIPEPERUSHI VYENYE UJUMBE MZITO " OPERESHENI ONDOA CCM DODOMA " OCD

 Hivyo ndivyo vibwagizo vya UKAWA Kwa njia ya vipeperushi vyenye Ujumbe huo,katika harakati za kupata ushindi ndani ya Vyama vya Upinzani ,Hiyo ndiyo michezo ya Siasa.
 Ni maandamano ya Amani yaliyo anzia viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma kuelekea Viwanja vya Barafu Mkabala na Uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Dodoma leo.
Matukio hayo ni kufuatia Maandalizi ya Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mtaa unaotarajia kufanyika nchi nzima hivi karibuni.
 Gari la Matangazo na pikipiki
 Hao ndiyo Makamanda wakiwa na Mtundiko kuashiria kwamba CCM inaondolewa Madarakani na Upinzani inashika madaraka hasa kwa ujumbe wa vipeperushi  vilivyo sambazwa Mjini hapa,Lakini ni  dalili za kujiamini.
 Hayo ni maandamano ya pikipiki ya wanachama wakiwa na bendera za CHADEMA ,CUF na nyingine kutokana na Vyama vilivyounda UKAWA
 Hapa Makamanda wakiwa wana pasha pasha mvuto kwa wananchi kusogea kwenye tukio hilo la Kihistoria kama mtangazaji alivyo kuwa akitangaza kuwa ni tukio la Kihistoria la kuitoa CCM madarakani kwa kuwapa likizo isiyo na malipo, Siasa Inapendeza masikioni.Haya kazi kwao tunawatakia mafankio mema katika safari yao ya Kuiondoa CCM kama vile imelala fo fofo.
Ni baadhi ya Viongozi.Zaidi utapata kutoka viwanja vya Barafu kwenye Magazeti na Luninga.

WAJUMBE WA BODI YA "MUTUAL GENERATION OF TANZANIA ( MGT) " IMEWAKILISHA MIRADI YAO MBELE YA WALEZI WAO MIRADI ILIYOFANYIKA NA INAYOTARAJIWA KUFANYWA KATIKA UKUMBI WA 56 KATIKA MANISPAA YA DODOMA NA MWENYEKITI WA MGT BWANA FERDINAND EMILY

 Wajumbe wa BODI ya Mutual Generation of Tanzania ( MGT ) Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao chao kifupi cha kuwakilisha Mirada iliyofanyiwa kazi na inayotarajia kufanyiwa kazi.












Mwanyekiti wa MGT Bw. Ferdinand Emily akilezea malengo ya Mutual Generation of Tanzania ( MGT ) mbele ya walezi  na wajumbe wa Shirika hilo lililoundwa na wanafunzi wa vyuo vikuu vinane Tanzania ambavyo ni Dodoma UDOM, Dar es Salaam UDSM,Chuo cha Elimu ya Biashara CBE, Makumira, Usimamizi wa Fedha  ( IFM), Mipango ( IRDP ) ,SUA na Chuo kikuu cha Jordan
 Walezi wa MGT aliyesimama na kusifu na kuelekeza juhudi za MGT ni Mkurugenzi wa AFNET Sarah D. Mwaga,wa kulia kwake ni Prof. Kalafunja Osaki wa UDOM ,wakatikati ni mwenyekiti wa MGT Bw. Ferdinand Emily , wa kushoto wake ni Bw. Christian Sikapundwa Stationery mkabala na Bohari ya Mkoa wa Dodoma na wanyuma Bi.Zaituni Said Ngwanga Kaimu Mwenyekiti MGT.
 Aliyesimama ni miongoni mwa walezi wa MGT Bi Mirium Zablon wa Sahara Media Group akiwapa moyo wa kujitoa katika kuanzisha Shirika hilo lisilo la Kiserikali la Wasomi waliohitu masomo yao na wale ambao bado wapo masomoni,akito wito kuwa wale ambao hawajajiunga na MGT wajiunge ili wajenge dhana Kujiajiri baada ya masomo yao. Ambapo mpaka sasa wajumbe waliyondani ya MGT ni zaidi ya 1000 idadi ambayo ni ndogo kulingana na idaidi ya wanafunzi wote walioko katika vyuo hivyo vinane nchini.
Wajumbe wa MGT wakisiliza kwa makini ushauri na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na walezi hao moja baada ya mwingine.

MGT imeandaa mradi wa shule ya Sekondari ambayo itawapa fursa kubwa ya kufanya sekodari hiyo iweza kujiendesha yenyewe .Aidha imeanzisha mradi wa ufugaji wa kuku ambao uko tayari kinacho hitajika hapo ninamna ya kupata mtaji. Pia wameandaa miradi mingine itakayo kidhi  mahitaji ya watanzani ikiwemo ufugaji wa nyuki.