Saturday, October 18, 2014

"MTOTO HATUMWI DUKANI LEO, NA AKITUMWA ATASAHAU CHENJI" HAYO NI YA LEO BADO MASAA MACHACHE TU WAPENZI,WASHABIKI WA YANGA NA SIMBA WATASHUHUDIA MTANANGE BAINA YA WATANI HAO WA JADI UWANJA WA TAIFA KUPITIA TBC 1

Wapenzi hao wameonekana wakijigamba kwa aina tofauti tofauti ya kila mmoja kumshinda mwenzake,lakini wanasema msema kweli ni dakika 90. Na kiingilio ni poa kabisa kisingizio kisiwepo tena kwa mashabiki wa soka.

BREAKING NEWS, MTIA AINA YA MSUFI ULIYOANGUKA KWA UPEPO MIAKA MITATU ILIYO PITA WILAYAI UYUI MKOA WA TABORA UMEINUKA NA KUSIMAMA KAMA ZAMANI, WANANCHI WAUVAMIA KUBANDUA MAGOME YA MTI HUO KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

 Kwa mujibu wa TBC 1 kwamba mti huo aina ya msufi ulianguka kwa upepo mika mitatu iliyopita ikiwa na baadhi ya mabome ya mti huo pamoja na mti kwenye matawi ulishambuliwa na mchwa.Lakini majuzi tu mti huo ulionekana ukinyanyuka polepole kama vile kuna watu wana unyanyua hadi ukasimama kama awali.

Shuhuda mmoja Bi Saada yeye alisema aliuona na kusikia aina fulani ya sauti wakati mti huo ukisimama,watu waliojumuika kushangaa maajabu hayo wilayani Uyui Mkoa wa Tabora hivi karibuni  walionekana wakibandua magome ya mti huo,pamoja na udongo uliolalia mti wenyewe. ( Waswahili husema ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni. ).


DODOMA YETU LEO






UZINDUZI WA CHANJO YA SURUA, MINYOO,NGIRI MAJI KITAIFA MKOANI DODOMA KUFANYIKA NYERERE SQUARE ( VIWANJA VYA MWALIMU NYERER ) KWA MAANDAMANO YALIYO ANZIA BOHARI MKOA

 Brass Bend ya Jishi la Wananchi wa Tanzania
 Brass Bend hiyo ndiyo iliyoongoza maandamano kuelekea Nyerere Square yakianzia Bohari Mkoa Dodoma jirani na stendi kuu ya mabasi.
 Baadhi ya wanafunzi wauguzi kutoka Mirembe Mkoani Dodoma
 Wauguzi wanafunzi
 Wanafunzi wa shule za msingi za Manispaa ya Dodoma
Brass Bendi ya wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa ya Dodoma
 Maandamano
 Wanafunzi wa shule za English Medium katika Manispaa ya Dodoma
 Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari katika Manispaa ya Dodoma

Pamoja na hao pia ni wanafunzi wa sekondari,Cha ajabu walengwa ambao ni Wanawake na Wanaume ambao ndiyo wanakuswa na  Uzinduzi wa Chanjo hiyo Kitaifa kwenye maandamano hawapo.

Aidha imekuwa ni mazoea katika baadhi ya mikoa kujiunga kwenye maandamano yanayo walenga wananchi moja kwa moja.Sana sana ni wanafunzi na wahusika wanaokuwa na wanafunzi hao.

Swali kama wanafunzi ,wanavyuo hawapo hayo maandamano hayatakuwepo?,kwanini maadamano ambayo hayawaletei tija wa faida wananchi wanakuwa wengi.Uzuri wake maandamano ya aina huyo wanafunzi hawa husishwi.

Hivyo kwakuwa hatuna utamaduni wa kuwa kwenye maadamano kama hayo au ni vipi ,bali tumekuwa wepesi wakwenda kwenye sehemu ya tukio kusubiri maandamano yaingie ambayo ni ya wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo.na kwamba mgeni Rasmi anayapokea maandamano hayo ya wanafunzi, na katika hutuba yake hagusii kuhushu wananchi kujihusisha na maandamano yenye manufafaa kwa jamii zao,kuliko kuwaachia wanafunzi peke yao.

Tuesday, October 14, 2014

JAMII YA BLOG YA TJIFUNZE KUSINI NA FAMILIA YA SIKAPUNDWA WANAUNGANA NA WANANCHI WA TABORA KWENYE SHEREHE YA KUZIMA MWENGE NA KUTIMIZA MIAKA 15 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE



Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo ni mika 15 tangu atagulie mbele za haki.Mwaka ambao Tanzania inaanza safari ya Kihistoria ya kutuga Katiba itakayo wapeleka watanzania kwa miaka 50 ijayo.
Aidha siku yaleo ni siku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipozimwa Mwenge baada ya kukamilisha mbio zake nchi nzima na kuzindua na kuwekea mawe ya msigi miradi kadhaa ya miradi kadhaa ya maendeleo.

Wednesday, October 8, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE ,DR. SHEN WAKABIDHIWA KATIBA INAYOPENDEKEZWA MJINI DODOMA MBELE YA MABALOZI MBALIMBALI WALIYO HUDHURIA SHEREHE HIZO

 Rais Jakaya Kikwete na Dr. Shein waonyesha Katiba inayopendekezwa baada ya kukaidhiwa na mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba Mhe.Samweli Sitta katika sherehe ya kukabidhi Katiba katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba Mhe. Samweli Sitta ,kielezea mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa kujadili Rasimu ya Katiba hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete asema Katiba inayopendekezwa ni halali, nzuri na hana wasiwasi nayo.Alisema Katiba ni nzuri haina mfano wake,amesema Katiba iliyomgusa kila mmoja na hali yake.
Aidha alisema Katiba imependekeza mambo megi ya Muugano ya kuwa na Serikali mbili,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka kamili ya kupata mikopo bila Serikali ya Muungano,Kujiunga na Taasisi za kimataifa na kuondoa migogoro ya Muungano.
Kawataka watanzania kuisoma vizuri Katiba hiyo na kuielewa na hatimaye kupiga kura ya ndio.
 Naye mawkilishi wa Kundi la walemavu Mhe. Mpanju amempongeza Rais Kikwete kwa uadilifu wake aliyouonyesha kipindi cha majadiliano ya Ibara mbali mabli kuliko sababisha sintofahamu kadhaa ,kwa baadhi ya wajumbe na kususia lakini aliona kazi itaendelea kwa mujibu wa sheria iliyopangwa.
Alisema katiba hiyo imayajali makundi yote yakiwemo ,walemavu,wakulima,wanawake,wafugaji ,wavuvi,wasanii, na wachimbaji wadogo wadogo.
Baadhi ya wananchi waliyokuwa wakiingia ndani ya uwanja wa Jamhuri kushuhudia  tukio hilo la Kihistoria