Tuesday, July 8, 2014

BRAZIL WAISHANGAZA DUNIA KWA KUKUBALI KUFUNGWA MAGOLI MENGI YA MFULULIZO KWAO,NA KUWAFANYA UJERUMANI IANDIKE HISTORIA YA MVUA YA MAGOLI KATIKA KOMBE LA DUNIA

Haijawahi kutokea katika mashindano ya kombe la Dunia na kama ilitokea basi ni miaka kadhaa ya nyuma huko timu kufungwa magoli mengi ya mfulululizo na kufanya timu nyingine wachanganyikiwe uwanjani kama ilivyo tokea Jana kwenye uwanja wa Estadio Minarao ulioko Beto Horizente mechi kati ya Brazil na Ujerumani ,wakati Ujerumani ilivyo ifunga Brazil magoli 7 - 1 yaliyosababisha vilio uwanjani humo.

Pamoja na Jitihada za goli kipa wa Brazil Julio Cesar kudaka mashuti makali kiasi kile lakini hazikuzaa matunda anabakia akidaka hewa kama unavyoona pichani.

 Jitihada za Julio Casar jana haziku zaa matunda pale alipo zitiwa na mashuti ya Ujerumani katika uwanja wa Estadio Minarao jana.
 Hizo ndizo heka heka za mvua za magoli kwa wanasoka hao wakongwe Duniani,walio waacha wapenzi wa wanasoka hoa midomo wazi.Na mbaya zaidi mvua hiyo ya magoli imewanyeshea kwao na sio ugenini ambako wangeweza kuficha aibu hizo.
 Baadhi ya wachezaji wa Brazil wakiteta jambo na Kocha wao lakini wapi, mwaka wa balaa ni wa balaa tu.Ukipanda mchicha zinaota mbigili.
Ni siku ya uzinduzi wa Kombe la Dunia Brazil,ambapo Timu hiyo ilisimama kwa stahili hiyo mbele ya macho ya umati wa watazamaji uwanjani humo siku hiyo.Lakini hatima yake na shamrashamra zote zimeishia mabao 7 - 1.

No comments:

Post a Comment