Tuesday, July 8, 2014

BRAZIL WAISHANGAZA DUNIA KWA KUKUBALI KUFUNGWA MAGOLI MENGI YA MFULULIZO KWAO,NA KUWAFANYA UJERUMANI IANDIKE HISTORIA YA MVUA YA MAGOLI KATIKA KOMBE LA DUNIA

Haijawahi kutokea katika mashindano ya kombe la Dunia na kama ilitokea basi ni miaka kadhaa ya nyuma huko timu kufungwa magoli mengi ya mfulululizo na kufanya timu nyingine wachanganyikiwe uwanjani kama ilivyo tokea Jana kwenye uwanja wa Estadio Minarao ulioko Beto Horizente mechi kati ya Brazil na Ujerumani ,wakati Ujerumani ilivyo ifunga Brazil magoli 7 - 1 yaliyosababisha vilio uwanjani humo.

Pamoja na Jitihada za goli kipa wa Brazil Julio Cesar kudaka mashuti makali kiasi kile lakini hazikuzaa matunda anabakia akidaka hewa kama unavyoona pichani.

 Jitihada za Julio Casar jana haziku zaa matunda pale alipo zitiwa na mashuti ya Ujerumani katika uwanja wa Estadio Minarao jana.
 Hizo ndizo heka heka za mvua za magoli kwa wanasoka hao wakongwe Duniani,walio waacha wapenzi wa wanasoka hoa midomo wazi.Na mbaya zaidi mvua hiyo ya magoli imewanyeshea kwao na sio ugenini ambako wangeweza kuficha aibu hizo.
 Baadhi ya wachezaji wa Brazil wakiteta jambo na Kocha wao lakini wapi, mwaka wa balaa ni wa balaa tu.Ukipanda mchicha zinaota mbigili.
Ni siku ya uzinduzi wa Kombe la Dunia Brazil,ambapo Timu hiyo ilisimama kwa stahili hiyo mbele ya macho ya umati wa watazamaji uwanjani humo siku hiyo.Lakini hatima yake na shamrashamra zote zimeishia mabao 7 - 1.

Monday, July 7, 2014

MAAJABU YA TANZANIA NI VIVUTIO KWA WATALII

 Mbuga za wanyama nchini ni muhimu kwa kuingiza Taifa mapato yake ,ili kinacho sababisha vivutio hivyo visichangie kwa kiwango kikubwa ni ujangili unaofanyika katika hifadhi hizo za Taifa.
Kuna watu wanaotaka utajiri wa harakaharaka wanaoingia katika mbuga hizo ka kuanza kuwa ua tembo kwa lengo la kupata pembe za wanyama hao kitendo ambacho kinasababisha wanyama hao kupungua kwa kiwango kikubwa.
Lakini je Serikali na wananchi wanaoishi katika maeneo ya mbuga hizo wanasaidiaje kupunguza uhalifu huo ili idadi ya tembo isizidi kutokomea.Ni vizuri kila mmoja awe askari wa kuzuia ujangili nchini.

SABABA MJINI DODOMA WANANCHI WASHEHEREKEA KWA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI

Wakati siku za nyuma siku kama ya leo ya sikukuu ya sabasaba ilikuwa ikionekana kuwa kweli sikukuu ya sabasaba.Lakini kwa kipindi  hiki sikukuu hiyo inafanikwa sana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya maonyesho ya Biashara kuanzia tarehe moja hadi tarehe saba.

 kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho  ya biashara, wananchi wakitembelea mabanda  na kununua bidhaa mbalimbali, Ambapo mikoani maonesho kama hayo hayapo,na hakuna ndoto ya kufanyika maonesho hayo katika mikoa yote ili wananchi wa mikoa hiyo nao wanufauke na bidhaa hizo.