Sunday, February 1, 2015

ITOLEWE ELIMU CHANYA KWA UMMA YA KUIPIGIA KURA KATIBA INAYOPENDEKEZWA - KIKWETE

Mwenyekiti wa Chama Tawala Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo kwenye kilele cha maazimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Majimaji Mjini Songea Leo

Wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliyofurika katika Uwanja huo,wageni mbalimbali walihudhuria maazimisho hayo wakiwemo wa kutoka Uganda.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa safari ya ushindi wa Chama  Cha Mapinduzi  ni uwepo wa wapigakura, iwapo wanachama wote watajiandikisha na kupiga kura ushindi ni lazima." Alisema Rais Kikwete."

Alisema kuna Kadi zaidi 2,000,000 zote wakizigawa kwa wanachama wapya , kwa vyovyote idadi itakuwa kubwa ya wapiga kura katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu, katika ngazi mbalimbali za Dola na ushindi utapatikana.

Aidha alisema kuwa jambo lililombele ya atanzania  ni upigaji  wa kura ya Katiba iliyopendekezwa na kwamba katiba hiyo itachapishwa na kusambazwa  na kutoa elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa kujitokeza kupiga kura ya kuikubali ,ingawa inapigwa vita na baadhi ya vyama kuwa wasiipigie kura katiba hiyo basi Katiba ya sasa itaendelea.

Amesema katiba inayopendekezwa ni Katiba iliyobeba maslahi makubwa ya Taifa zima,lakini iwapo haikukubaliwa  kwa kuwa  Serikali tatu hazikuwekwa  katika Katiba Inayopendekezwa ,hivyo Katiba  ya sasa itaendela mpaka hapo Rais mwingine akiwa tayari kuanzisha mchakato  wa Katiba wanayoitaka.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa Uchaguzi wa Oktoba 2015 ni wa kihistoria kwa kuwa Rais atakayechaguliwa ni wa awamu ya tano ( 5 ).Hivyo ni muhimu kupata mombea  bora mwenye sifa kutoka kwenye chama kilicho komaa,Imara, ambacho kitato mgombea  kwa kuzingatia kanuni na maadili ya CCM.

Hatimaye amesema kuwa sh.bilioni 89 za ununuzi wa mazao ya wakulima zimeshaanza kulipwa kwa wakulima,ambapo lengo ni kuanza kuwalipa wakulima wadogo ndipo wakala walipwe baadaye inaonyesha malipo ya hayo melipwa kinyume kama ilivyo elekezwa.Ambapo Bilioni  15 zimesha tolewa kwa ajili ya malipo hayo ,na kwamba malipo hayo yatamalizika kabla ya mwezi Machi 2015.

1 comment:

  1. Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, angefanya jambo jema iwapo angewakumbusha wananchi kuwa suala la katiba mpya halikuwepo katika ilani ya CCM, kwamba CCM walisema katiba iliyopo inafaa, na kwamba CCM wamechakachua mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba na kuandaa hii katiba wanayotaka ipigiwe kura. Angefanya bora iwapo angesema kuwa katika kuelimisha umma, CCM itasaidia katika kusambaza mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba sambamba na hii katiba inayopendekezwa na CCM. Hapo ningekubali kuwa mwenyekiti wa CCM kweli ana nia ya dhati ya kuona umma unapata elimu chanya kuhusu suala hilo.

    ReplyDelete