Saturday, February 28, 2015

BREAKING NEWS!!!!! KIONGOZI WA TOTI NA MBNGE WA MBINGA AFARIKI KUTOKANA NA KUSHUKA KWA SUKARI GHAFLA LEO SAA 1O JIJINI DAR ES SALAAM

 Mshe. Captain John Komba akiwa katika sughuli zake wakati wa hai wake.
Mhe.Capten John Komba Mungu ailaze maali pema peponi Amina

WAANDIHI WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA USAHII,UFASAHA NA MAADILI KATIKA UTOAJI WA TAARIFA ZAO

 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Mhe. Valerie Msoka akiongea na wahitimbu wa Chuo cha Uandishi wa habari ( Morogoro School of Journalism MSJ ) Mgeni Rasmi katika mahafali wahitimu 144.
 Picha ya pamoja ya wanachuo wahitimu Cheti na Mgeni Rasmi
 Picha ya pamoja na wahitimu wa Stashahada ya uandisi wa Habari na Mgeni Rasmi
 Womaji wa Risala ya wahitimu wa Stashada ya Uandishi wa Habari kwa Mgeni Rami ayupo katika Picha
 Mheshimiwa  Valerie Msoka Mkuruenzi Mtendaji wa TAMWA
Mhitimu Michael C.  Sikapundwa akipokea cheti cha Stashahada ya Uandishi wa Habari
Mstaafu wa MSJ Bwana S.Dogoli mwenye kaunda suti nyeusi wakibadilisa mawazo
M
 picha  ya pamoja na wahitimu viongozi na mgeni Rasmii
 Mwakilishi wa Abood Media Mtangazaji Mkongwe Bw.Samadu Hassan akipokea cheti kama zawadi ya mchango wao katika Chuo hicho.
Picha ya pamoja Mgeni Rasmi Mkuu wa Chuo kulia, Mkuruenzi kushoto,na Bw. Said Dogoli kushoto kwa mkurugenzi.

WAANDIHI WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA USAHII,UFASAHA NA MAADILI KATIKA KURIPOTI  TAARIFA ZAO


Mkurugenza Mtendaji wa TAMWA Mhe. Valerie Msoka kwenye mahafali ya wahitmu 144 wakiwemo Walmu wa Awali,Cheti  cha Uandishi wa Habari na Stashahada ya Uandishi wa Habari katika viwanja vya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro School of Journalism MSJ  Nanenane katika Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Msoka aliwaambia wahitimu hao kuwa kazi yao ni ngumu na inachangamoto nyingi katika upatikanaji wa habari,hivyo wanatakiwa kuzingatia ufasha na usahihi katika utoaji wa habari,na kwamba kwaende wakaandike masuala ya Unyanyasaji wa Kijinsia na mambo yote  ya ukatili unaofanywa kwa watoto wa kike na wanawake.
Aidha alisema waandike habari bila upendeleo na kuwa na usiri wa habari walizo pewa na watoa habari hizo wala waiwe na upendeleo katika undikaji wa habari kwa uaminifu na haki pamoja na kuusoma zaidi masuuala ya kisiasa,Kijamii na Kiuchumi.
Hatima yake aliawa vyeti kwa wahitimu  144 wakiwemo  Walimu wa Awali,Cheti  Cha Uandishi wa Habari na Stashahada ya Uandishi wa Habari.
Awali Mkuu wa chuo hicho Bwana Augustine S. Nongwe alisema kuwa chuo chake kina mafanikio makubwa kufuatia wahitimu wa chuo hicho wamepata ajira katika vyombo mbalimbali vya Habari nchini na wengine elimu ya juu.
Ambapo katika mafanikio hapakosi changamoto alitaja changamoto hizo  ni pamoja na upunufu wa vfaa vya kufundishia na kujifunzia,Upungufu wa wakufunzi wenye sifa,uhaba wa fedha za kendeshea chuo kufuatia ulipwaji hafifu wa ada kutika kwa wanafunzi.
Vilevile  amewshari wenye vyombo vya habari kuajiri wahitimu wanaotoka katika chuo hicho,kwani vyombo vingi vinaajiri bia kuzingatia ubora wa elimu ya uandishi wa habari.
Isitoshe ameimba Bodi ya mikopoo ya elimu ya juu,kuona uwezekano wa kuwapatia mikopo wanachuo wanaojiunga na vyu ivyo nchini ili waweze kufikia ndoto zao.

Sunday, February 1, 2015

ITOLEWE ELIMU CHANYA KWA UMMA YA KUIPIGIA KURA KATIBA INAYOPENDEKEZWA - KIKWETE

Mwenyekiti wa Chama Tawala Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo kwenye kilele cha maazimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Majimaji Mjini Songea Leo

Wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliyofurika katika Uwanja huo,wageni mbalimbali walihudhuria maazimisho hayo wakiwemo wa kutoka Uganda.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa safari ya ushindi wa Chama  Cha Mapinduzi  ni uwepo wa wapigakura, iwapo wanachama wote watajiandikisha na kupiga kura ushindi ni lazima." Alisema Rais Kikwete."

Alisema kuna Kadi zaidi 2,000,000 zote wakizigawa kwa wanachama wapya , kwa vyovyote idadi itakuwa kubwa ya wapiga kura katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu, katika ngazi mbalimbali za Dola na ushindi utapatikana.

Aidha alisema kuwa jambo lililombele ya atanzania  ni upigaji  wa kura ya Katiba iliyopendekezwa na kwamba katiba hiyo itachapishwa na kusambazwa  na kutoa elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa kujitokeza kupiga kura ya kuikubali ,ingawa inapigwa vita na baadhi ya vyama kuwa wasiipigie kura katiba hiyo basi Katiba ya sasa itaendelea.

Amesema katiba inayopendekezwa ni Katiba iliyobeba maslahi makubwa ya Taifa zima,lakini iwapo haikukubaliwa  kwa kuwa  Serikali tatu hazikuwekwa  katika Katiba Inayopendekezwa ,hivyo Katiba  ya sasa itaendela mpaka hapo Rais mwingine akiwa tayari kuanzisha mchakato  wa Katiba wanayoitaka.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa Uchaguzi wa Oktoba 2015 ni wa kihistoria kwa kuwa Rais atakayechaguliwa ni wa awamu ya tano ( 5 ).Hivyo ni muhimu kupata mombea  bora mwenye sifa kutoka kwenye chama kilicho komaa,Imara, ambacho kitato mgombea  kwa kuzingatia kanuni na maadili ya CCM.

Hatimaye amesema kuwa sh.bilioni 89 za ununuzi wa mazao ya wakulima zimeshaanza kulipwa kwa wakulima,ambapo lengo ni kuanza kuwalipa wakulima wadogo ndipo wakala walipwe baadaye inaonyesha malipo ya hayo melipwa kinyume kama ilivyo elekezwa.Ambapo Bilioni  15 zimesha tolewa kwa ajili ya malipo hayo ,na kwamba malipo hayo yatamalizika kabla ya mwezi Machi 2015.