Tuesday, November 4, 2014

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE,AHIMIZA VIJANA KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KWA SERIKALI ZA MITAA,KWA KUWA NI SAFARI YA UWEKEZAJI WA UONGOZI KWA VIJANA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wazee wa Mji wa Dodoma leo,baada ya kukabidhiwa Risala iliyo somwa na Katibu wa Baraza  la wazee Shekhe Abdalah Makubeli.kisha ilikabdhiwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Balozi Job Lusinde.
Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa mji wa Dodoma Balozi Job Lusinde amkabidhi Rais Jakaya Kikwete risala ya wazee hao iliyo mpongeza kwa ufanikishaji wa shughuli alizozifanya za maendeleo katika Awamu ya nne ya uongozi wake.


Katibu wa Baraza  la  wazee mkoa wa Dodoma Abdalah Makubeli alisoma Risala  kwa niaba yao wazee hao.
I .Walishukuru kwa kukubaliwa kuongea nao ,Aidha Risala hiyo ilielezea ( Suala la kukua kwa uchumi, kuinua uchumi Mkoani Dodoma na  taifa  kwa ujulma ,Kutuwezesha katika kilimo cha zabibu, viwanda ili kutoa ajira kwa vijana wetu.

Katika usindikaji wa mafuta ya kula na vya  nyama.  Pia walilisemea Suala la Makao makuu lipewe Msukumo  pamoja na kuiomba kuangalia Bodi ya SDA ili kusaidie ustawisishiji wa mji wa Dodoma.

Walisemea kuhusu ,muundo wa kusimamia Ardhi na makazi, na kuweka wazi ratiba ya utekelezaji na ustawisishaji wa Makao Makuu. Hivi sasa mkoa  unakuwa kwa kwasi. Mf kujengwa vyuo vikuu vikubwa katika Afrika mashariki na hivyo wameomba kuipa  Hadhi kuwa mji wa Dodoma na kwa wa  kimataifa.napia liwe  jiji.

Wamesema kwa kuwa miundombinu yake ni bora inayo kidhi mahitaji ya kuwa Jiji kama Majiji mengine nchini.

Sisi wazee tumeona upo umuhimu wa kushukuru maisha ya mama na watoto tunaomba kukamilisha ujenzi wa jingo katika Hospitali ya mkoa lililo jengwa kwa miaka 9 bila kukamilika,kwa ajili ya mama na watoto kwenye hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa.na kwamba wazee hao wameomba kupatiwa huduma ya afya jirani.

Sambamba na   hayo hawakusaha Kumpongeza kwa  kuanzisha mchakato wa Katiba pamoja na vikwazo vingi.vilivyojitokeza na hatimaye Katiba iliyopendekezwa akakabidhiwa,hivyo wameomba akamilishe kabla ya kuachia ngazi na kuongezea wananchi   wajitokeze kwa wingi katika kuipigia kura ya ndiyo katiba iliyopendekezwa.

 Na hatimaye Balozi Lusinde Mweyekiti wa Baraza la wazee Dodoma  alimkaribisha Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.kuongea na wazee wa Dodoma.

Na Rais anasema.wazee mkutano huu wameitisha wenyewe.,ningekutana nanyi lakini nilikuwa na mambo mengi.Katika kujibia Risala ya wazee hao alisema atayashughulikia na kuyafuatilia yote waliyo yaomba. Yajiwemo kwa uwekezaji  wa Hoteli,Viwanda, ili kuongeza ajira kwa vijana wao. ,Ujenzi wa jingo la hospitali ya Mkoa wa Dodoma na huduma za afya kwa wazee.na uwezekano wa kuwa Dodoma kuwa Jiji.

.Ndipo alipozungumzia mambo manne muhimu

 Alisema kuwa mahusiano yetu na China ni mazuri ambapo alipokelewa vizuri sana kwa hafla maalumu ya kutimiza miaka 50 ya mahusiano ya Serikali ya Tanzania na.Serikali ya China  ambayo iliwakilishwa na  na Makamu wa Rais na hatimaya kukutana na Rais.alisema nusu karne ya mahusiano yetu yamekuwa na mafanikioa makuwa sana.

Rais aliwahimiza wananchi kujiandaa katika  uchaguzi wa Serikali za Mitaa.TAMISEMI wamesha anza    maandalizi ya kuandaa Ratiba ambazo zimeshatolewa.kwa majina ya mitaa,na Vitongiji.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, aidha wakati wa kupigia kura Katiba iliyopendekezwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga ya ndiyo . kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.
Aidha amewataka wenye sifa kujitokeza kugombea uongozi kwenye Serikali za Mitaa watu wazima,Vijana na wanawake wasibaki nyuma kujitokeze kugombea afasi hizo.

Alisema vijana wajitokeze kugombea uongozi kwa kuwa jimo wapo ya uwekezaji katika uongzi “ ni lazima tuanze safari ya uwekezaji katika uongozi” alisema Rais.

Jingine alizungumzia Katiba iliyopendekezwa,” ni Katiba iliyo kidhi  viwango vyote,ingekuwa kwenye mpira tungesema imekamilika katika Idara zote,Katiba ni nzuri” alisema.

.






No comments:

Post a Comment