Maswali kadhaa yanaulizwa na watu kuhusu masuala ya
kuwepo kwa Serikali mbili au tatu,na
kuna vuta ni kuvute katika hoja hiyo kwa wananchi , ambapo wengi wao hasa
vijana wengi wanataka kuwepo kwa Serikali tatu na ni kitu ambacho kinatarajiwa
kuwepo kwenye Katiba ya Nchi.
Sasa iwapo
inatokea kutoka kwa baadhi ya wananchi
wachache wenye hoja ya kuwepo kwa Serikali mbili,wakati wengi wao wanahitaji
kuwepo na Serikali tatu na hasa wasomi vijana katika vyuo vya elimu ya juu
nchini.
Ni nini unadhani kitatokea baada ya kutangaziwa hivyo? Na je
iwapo itatokea hivyo Serikali imejiandaaje kutuliza au kuwaelimisha watu hao
ambao wengi wao wamechoka kuwa na Serikali mbili na wanadai Serikali tatu bila
kujali athari zake baadaye “ liwalo na liwe itajulikana mbele kwa mbele”
Jambo hilo siyo la mzaha wala si la kulichukulia juu juu,kwa
kuwa vijana wetu wengi bila kujali wasomi ama si wasomi,wavijijini au wa mjini
wote wamekuwa na kauli moja.Hivyo Tume ya katiba iliangalie kwa macho mawili
matokeo ya Hoja hiyo,na namna gani watalikabili suala hilo iwapo
litatokea.Hatupendi litokee.
No comments:
Post a Comment