Monday, August 31, 2015
MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA ACT WAZALENDO BIBI ANNA MGHWIRA AHAIDI KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA AKIJUMUISHA VYAMA VYOTE NA MAKUNDI YA KIJAMII
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Bibi Anna Mghwira akitaja misingi ya Utu,Uadilifu na Uzalendo katika Chama chake,Jana katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Kampeni ambapo amesema ataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kujumuisha Vyama vyote mradi wawe na Utu,uadilifu na Uzalendo.
Baadhi ya wananchama waliyo hudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya ACT katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wananchama waliyo hudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya ACT katika Viwanja vya Mbagala Jijini Dar es Salaam jana
Mgombea
Urais huyo alisema hayo wakati
akizungumza na wanachama wa chama hicho katika viwanja vya Mbagala
Jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa iwapo atapa ridhaa ya kuwa Rais wa awamu ya Tano ataunda serikali ya umoja
wa Kitaifa kutoka vyama vyote,wananchi na Sekta mbalimbali kwa msingi wa kujali
Utu,Uadilifu na Uzalendo.
Ametaja
vipaumbele vyake ni pamoja na Hifadhi ya Jamii,Tatizo la ajira kutokana na uwekezaji katika kilimo,Kuimarisha Makao
makuu ya Dodoma kuwa ya Serikali,siyo ya Chama.kwani Dodoma ni katikati ya nchi
makao makuu ya chama yatatafutiwa sehemu nyingine.
Vingine
ni pamoja na hifadhi ya jamii,viwanda vya mazao ya kilimo,uvuvi utalii na
michezo,nakwamba maliasili zote zitakuwa za wananchi na sio za Katiba,pamoja na
kuboresha Elimu kwani watoto wanamaliza Elimu ya Msingi hawawezi kusoma na wale
waliomaliza Elimu ya sekondari hawawezi kusoma barua ambapo wanaomaliza vyuo
vikuu hawawezi kujieleza katika ofisi wanazofanyia kazi.
Aidha
amesema kuwa watoto wengi wenye vipaji
wako mitaani wanaitwa watoto wa mitaani, serikali yake watoto wote hao
watapata elimu.
Alisema
iwapo atapata ridhaa hiyo ya kuwa Rais Mwenye kiti wa Chama hicho Bwana Zitto
Kabwe atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali
Kampeni Meneja wa Chama hicho,ni mkakamavu na shujaa anayesema mambo asiyo na
uhakika nayo yanayo sababisa kuingilia Utu wa mtu,lakini katika Sera zao
wanajali utu,Uadilifi na Uzalindo katika Ilani yao ya Uchaguzi, kutokana na
kauli ile ya kudhalilisha utu wa mtu vinaendana na wanayoyanadi.Kitu kile
hakipendezeshi watu.Anatakiwa kunadi Ilani na Sera ya Chama chake siyo kukosoa kwani
wana uhakika gani kama wakipata ridhaa kutawala watateleza ahadi zote kwa
wananchi. Walizo zisema..
Kwa
Stahili ile Chama cha Mapinduzi CCM kitaendelea kutawala kwa muda mrefu kwa kuwa vyama vya Upinzani
badala ya kusaidiana katika kunadi Sera zao wanazarauliana wao kwa wao.
Lakini
kwanini wanashambuliana wao kwa wao
wakati wanadai kuleta mabadiliko katika Siasa,wakidai CCM imekaa madarakani kwa
muda mrefu bila mabadiliko.Nimeamini kuwa vita vya panzi furaha ya kunguru.
Ukweli
ndoto ya Ukawa kwenda Ikulu kwa Stahili ya msemaji wa ACT Wazalendo ambaye ni Kampeni meneja haipo,kwani
itawachanganya hata wananchi ambao nao walikuwa na ndoto ya madiliko wakachagua
kuendelea na CCM hiyohiyo.kwa inaonyesha kuwa vyama hivyo kila kiongozi anataka
madaraka ya juu.
Ila
Mgombea wao anajua kutetea Sera na Ilani ya Chama chake,amepanga vipaumbele
vyake kwa ufasaha na hakuwa na haja ya kuwalaumu wenzake au viongozi wailiyo
shika madaraka ya juu.
Friday, August 21, 2015
PAMOJA NA USHABIKI KWA WAKEREKETWA ,CHA MSINGI HAPA NI KUWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA
Ushabiki wa kusindikiza viongozi kwenda kuchukua Fomu na kurudisha Fomu,uwe wa amani na nidhamu bila kujali Itikadi za vyama vyao.
Kinachao takiwa kutolewe elimu kwa mashabiki hao, siku ya kupiga kura wasijae kwenye vituo vya kupigia kura na kudai wanamtaka nani,kelele kibao waache. wawaachie mawakala wafanye kazi yao.
Maana mkono wa Dola ni mrefu kupita kawaida,watapigwa bila faida yoyote kwani huyo watakaye mtaka kuwa Diwani, Mbunge au Rais akichaguliwa au hakuchaguliwa watapa faida gani au hasara gani.
Ushabiki usio na tija hauta saidia,Wananchi wengi wanaomba kwa Mungu kuwepo na Upigaji kura wa Amani,Ili Tanzania Ibakie kuwa kisiwa cha Amani.
Wengine wanasema hata viongozi nao waache lugha za kashfa wakati wa Kampeni zao,Matusi,lugha za kejeli,Ubabe na umwamba kwenye Kampeni hazisidii wananchi,Wananchi wanacho hitaji ni maisha nafuu, kumtoa mtanzania mwenye kipato cha chini na kumpeleka kwenye kipato walau hata cha kati na sio wimbo uliyozoeleka kila Awamu.
Tunawatakia Amani,Utulivu,Upendo na kuhasehimiana wakati wa Kampeni zao kwa kila Chama kilichoingia kwenye kinyang'anyilo cha Udiwani,Ubonge na Urais
Tuesday, August 11, 2015
BAADA YA KUINGIA IKULU MHE. LOWASSA ,BODABODA,MAMA NTILIE, NA MACHINGA WATANUFAUKA IWAPO ATACHAGULIWA
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo { CHADEMA} Mheshimiwa Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake walisindikizwa na wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kwenda kuchukua Fomu za Urais.na kusema, iwapo atachaguliwa kuwa Rais hatawangusha,na ataweka kipaumbele kwa Bodaboda,mama ntilie na Wamachinga
Subscribe to:
Posts (Atom)