Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa akiongea na wahitimu wa Stashahada na Shahada ya Kompyuta Sayansi katika chuo cha St,Joseph Songea leo wanachuo 96 wamehitimu mafunzo hayo.
Picha ya pamoja ya wahitimu wa Shahada ya kwanza katika Kompyuta Sayansi
Picha ya pamoja ya wahitimu wa Stashahada
Picha ya pamoja ya wahitimu wa Stashahada
Wahitimu wakila kiapo kabla hawajatunukiwa Stashahada na Shahada zao.
Mawaziri wakimsikiliza mtoa maelezo kwenye chumba cha Kompyuta sayansi

SERIKALI
imewataka wanafunzi wa elimu ya juu ambao wanakopeshwa fedha na Bodi ya mikopo nchini
kuirejesha mikopo hiyo,mara tu wanapo
malize elimu yao
na kufanikiwa kupata ajira, kwa kulipa mikopo hiyo kuitafanya serikali kuweze
kuwakopesha wanachuo wengine.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru
Kawambwa kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika St, Joseph College of Information Technology
Ruhuwiko nje kidogo ya Mji wa Songea leo.
Alisema
serikali inahitaji kutoa elimu ya juu kwa wanachuo wote wenye sifa na vigezo
vya kujiunga na vyuo vikuu nchini,na itajitahidi kutoa mikopo kwa kadiri ya
uwezo wake ingawa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa ni wengi,kwa hiyo waliyo
kopeshwa wakirejesha mikopo hiyo wanachuo wenye kuhitaji mikopo hiyo watapata.
Aidha
ameto rai kwa waajiri kuonyeshe ushirikiano wao na serikali katika kukusanya fedha hizo kwa wahitimu
ambao wamewaajiri, kurejesha mikopo hiyo kwenye bodi ya mikopo.na wasipo fanya
hivyo hatua kadhaa zitachukuliwa zidi yao.
Alisema
serikali imetengenga shilingi trioni 1.45 kwa wanafunzi wa elimu ya juu,Wizara
kupitia elimu ya juu na bodi ya mikopo imeamua kuongeza kiwango cha mkopo kwa
mwanafunzi wa elimu ya hiyo.
Katika
mahafali hayo wanachuo 96 wamehitimu mafunzo yao na kutunukiwa Stashahada kwa wanachuo
39 katika Fani ya Uhandisi wa Sayansi ya
Kompyuta na 58 shahada ya kwanza katika Uhandisi wa Sayansi ya Kompyuta.