Monday, May 25, 2015

BAJETI YA WIZARA YA MAENDELEO JINSIA NA WATOTO YALETA ZOGO NDANI YA BUNGE,BAADA YA MHE.ESTER MATIKO KUTAKA KUJUA KWA NINI INGO KUFUTWA.

Akilalamikia WAMA ni ya Chama Tawala.
Waziri wa Wizra hiyo Mhe,Sophia Simba alijitahidi kuelezea kuhusu INGO na WAMA,Lakini ikawa nidhamu hakuna, sauti zinasikika kutoka kwa baadhi ya wabunge, Kaachini au simama,sasa hawaheshimu kiti cha mwenyekiti.Hebu wafika mahali wajue kuwa Bunge lile si mahala pa malumbano ya utofauti wa Vyama.Wasubili kwenye Kampeni,Ni aibu watu wengine wanavyo liona Bunge letu.

Friday, May 22, 2015

VIFAA VYA CERAGEM ,PAMOJA NA KUPONYA MAGONJWA NA UBORESHA AFYA,LAKINI PIA HUPUNGUZA MAFUTA YALIYO JAZANA MWILINI,KAMA NILIVYO VAA SLIM BELT KUPUNGUZA TUMBO

 Mkanda huu hupunguza mafuta yaliyo jazana tumboni na ufanya tumbo lipungue.CERAGEM hii ina toa huduma ya upima uzito, urefu na uwingi wa mafuta mwilini.Huyo ni mie  Blogger TUJIFUNZE KUSINI CHRISTIAN SIKAPUNDWA, Hunikosi kwenye Mazoezi Tiba ya CERAGEM kila siku,Wewe Je, Unangoja Nini.
Waati wengine wako kwenye mazoezi ,na baadhi yao hulala wenye mashine hizo kwa dakika 40,kama hiyo haitoshi, walimu wa kituo hicho wanatoa mafunzo kila siku kuhusu mwili wa binadamu ulivyo na jinsi unavyo fanya kazi, Aliye kaa ni mwalimi Bi. Lilian Mushi ili kuwasaidia wanao lala katika mashine hizo
Hilo ni jengo la Kituo cha CERAGEM Uhindini Mjini Dodoma

VIJANA TUACHE KUKAA VIJIWENI,TUJISHUGHULISHE NA BIASHARA NDOGO NDOGO KUFANYA HIVYO TUTAPATIWA MIKOPO YA KUENDESHA BIASHARA

Hayo yamesemwa na majasilia mali Bwana Mmas Iramba anayeuza viatu vya mitumba ndani ya soko la Sabasaba  katika manispaa ya Dodoma.
  Mmasi alisema kuwa vijana waachane na magenge vijiweni, bila ya kujishughulisha kwani kuna fursa nyingi zinazoweza kumtoa kijana pale alipo na kusonga mbele kwa kufanya biashara.
Amesema alianza na viatu vichache lakini baada ya kupata mkopo ameweza kununua viatu vya mitumba vingi vinavyo mpatia faida na kulipa deni alilokopa.

Thursday, May 21, 2015

USAFIRI WA MAJINI ,UWEKEWE VIFAA VYA TAHADHARI,LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUTIMIZA MIAKA 19 YA MELI MV BUKOBA

Hapa ni eneo la Igoma Mwanza walipozikwa wahanga 391 waliokosa ndigu zao kutokana na ajali ya kupindika na kuzama kwa meli ya MV Bukoba Mei 1996.
Basi keo waombolezaji na wananchi wlioguswa na tukio hilo waliweka maua na kufanyia usafi katika makaburi hayo.Lakini pamoja na ajali hiyo bado usafiri katika Ziwa Victoria hali ni tete,sio salama sana.Zaidi ya watu mia nane walipoteza maisha.yao ,Mungu zilaze  roho za marehemu hao mahali pema peponi Amein.

DODOMA, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BAJETI YAKE ZAIDI YA BILIONI 200 IMEPITA BILA KUPINGWA

Waziri wa KATIBA  na SHERIA Mheshimiwa Rose Migiro amewahimiza wananchi kusoma katiba,ili waielewe wakati wa kuipigia kura katiba hiyo.
Amesema kuwa katiba 2,400,000 zimichapishwa na kusambazwa, nakala 2,000,000 ni za  maandishi ya kawaida ,Nakala 200 na  maandishi ya nundu kwa ajili ya wale wasioona  na nyingine 200 ni kwa maansidhi makubwa kwa ajili ya wenye uono hafifu ,naka 1,443,000 zimepelkwa kwenye kata zote nchini.
Aidha mahakama imepata bajeti kubwa ikilinganishwa na bajeti ya miaka iliyopita,ambapo imetengewa 40 Bilion.

Wednesday, May 20, 2015

HIVI VIONGOZI KUSHINDWA KUHAMIA MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA NA KUWAFANYA WABAKI DAR ES SALAAM ,NI KWA SABABU

Dodoma hakuna bahari  au Uwanja wa ndege wa Kimataifa.Au kwa sababu Dodoma kuna vumbi jingi ikilinganishwa na Dar es Salaam ,Au Mchana jua usiku Baridi kali. Au vipi  kwa hiyo Dodoma ya leo siyo ile ya miaka miwili iliyo pita. Nahii ndiyo Dodoma yenye wenyeji wakarimu sana.

 Ni moja ya majengo mapya ambalo litakuwa ofisi mbalimbali lililop mkabala na Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, na ofisi za Fire
 Nihayo  majengo mawili amabyo yapo katika hatua za mwisho wa kukamilisha ujenzi
 Katikati ya miti hiyo ni Maktaba ya Mkoa wa Dodoma mkabala na Hospitali ya Makole na Ofisi za Manispaa ya Dodoma
Kulia kwenye mtu aliyekaa na anyetembea ni SIDO HAPA Dodoma barabara kuelekea Tenesco Dodoma

Tuesday, May 19, 2015

RAIS PHILIP NYUSI WA MSUMBIJI AMEKUWA RAIS WA KWANZA WA NCHI HIYO KULIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 Rais Philip Nyusi akilihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mjini Dodoma leo,amesema ziara yake hapa nchini ina lengo la kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji kuhusu Demokrasi,siasa na utamaduni, ushirikiano katika biashara na elimu.
Aidha ziara hiyo ni mafunzo kwake ya uongozi na kudumisha ushirikiano wa waasisi wa vyama vya nchi hizo mbili.Pia amesema wafanya biashara wanakaribishwa Msumbiji ,na Viza hakuna.
Baada ya Ziara yake bungeni amerejea nyumbani kwake nchini Msumbiji.
Baada ya Hotuba fupi alipewa zawadi ya picha ya Jengo la Bunge na Mhe. Spika Anne Makinda.