Thursday, May 29, 2014

PAMOJA NA KUMKABA KOO PRFOF. ANNA TIBAIJUKA, LAKINI BAJETI YA WIZARA YAKE IKAPITA

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka baada ya kuwakilisha bajeti ya Wizara yake ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2014- 2015 Bungeni,ndipo palipotokea waheshimiwa Wabunge wakaanza kuchangia ,ikwa mshikemshike kwa Mhe. Tibaijuka.

Wizara hiyo ni nyeti na  ina mambo mengi na yote yalikuwa na lawama. Wabunge hao walitaja migogoro kibao ikiwemo  wakulima na wafugaji,upimwaji wa viwanja,upatikanaji wa Milki za Ardhi na mengine mengi.

Lakini mwisho wa lawama  kwa waziri huyo Bajeti yake ilipita.Pamoja na lawama kuhusu migogoro inayotokea kila kona ya nchi hii, ifike mahali tusema Prof. Tibaijuka amejitahidi sana katika kuyatatua matatizo ya migogoro ingawa haiwezi kumalizika maana kila kukicha inajitokeza.

Kilichopo ni kwenda kujipanga sawa sasa na watendaji wake,hasa katika utoaji wa Hati milki za Ardhi na Viwanja, wateja wanasumbuliwa kupata hati hizo mtu anaweza kuzungushwa njoo mwezi ujao ,akienda  naambiwa tena njoo baada ya siku 30, basi mradi lugha inabadilishwa hadi kero.Yeye kama yeye hausiki na majaribu hayo yanayo wapata wateja wake.
                                           Prof. Anna Tibaijuka akiwakilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014 - 2015 Bungeni Mjini Dodoma juzi na kukamilisha jana.

BLOG HUWA JINA, HIVYO BODO NIPO NANINAENDELEA NA KUWASILIANA NA WASOMAJI WA BLOG HII TUPO PAMOJA

Samahani wasomaji wa Blog yanga niliadimika kidogo katika kuwasiliana kwa blog na kupeana habari,Kwa  sasa nipo Dodoma.

Sunday, January 5, 2014

IWAPO KUMEIBUKA HOJA YA KUWEPO KWA SERIKALI MBILI ,AMBAPO WANANCHI WENGI WANATAKA KUWEPO NA SERIKALI TATU NA HASA VIJANA WALIYOKO KWENYE VYUO MBALIMBALI, JE SERIKALI IMEJIANDAAJE KUWAELIMISHA UZURI WA KUWA NA SERIKALI MBILI NA UBAYA WA KUWA NA SERIKALI TATU?




Maswali kadhaa yanaulizwa na watu kuhusu masuala ya kuwepo   kwa Serikali mbili au tatu,na kuna vuta ni kuvute katika hoja hiyo kwa wananchi , ambapo wengi wao hasa vijana wengi wanataka kuwepo kwa Serikali tatu na ni kitu ambacho kinatarajiwa kuwepo kwenye Katiba ya Nchi.

 Sasa iwapo inatokea  kutoka kwa baadhi ya wananchi wachache wenye hoja ya kuwepo kwa Serikali mbili,wakati wengi wao wanahitaji kuwepo na Serikali tatu na hasa wasomi vijana katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
   Ni nini unadhani kitatokea baada ya kutangaziwa hivyo? Na je iwapo itatokea hivyo Serikali imejiandaaje kutuliza au kuwaelimisha watu hao ambao wengi wao wamechoka kuwa na Serikali mbili na wanadai Serikali tatu bila kujali athari zake baadaye “ liwalo na liwe itajulikana mbele kwa mbele”
   Jambo hilo siyo la mzaha wala si la kulichukulia juu juu,kwa kuwa vijana wetu wengi bila kujali wasomi ama si wasomi,wavijijini au wa mjini wote wamekuwa na kauli moja.Hivyo Tume ya katiba iliangalie kwa macho mawili matokeo ya Hoja hiyo,na namna gani watalikabili suala hilo iwapo litatokea.Hatupendi litokee.


Friday, January 3, 2014

FAMILIA YA BWANA SIKAPUNDWA KUFANYA HAFLA FUPI YA KUMPOKEA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUTIMIZA MIAKA 60 TAREHE 25/13/2013 ,ILIYOFANYIKA NYUMBANI KWAKE MJINI DODOMA JANA

 Bwana Sikapundwa analishwa keki na mkewe Mrs Sikapundwa
BwSikapundwa anamkabidhi keki mkewe
 Gw.Sikapundwa anamlisha mkewe keki
 Bw. Sikapundwa anamlisha Baba Mkwe wake Mzee Bickson Bilali wa miaka 100 na siku 2
 Mr & Mrs Sikapundwa
 Bw.na Bibi Sikapundwa kushika kisu kukata keki haipo pichani
 Mama Mdogo Yunesi Mwakyusa akikata vipande vidogo keki na ndiye mtengenezaji wa keki na bingwa wa upambaji kumbi za sherehe.anapatikana karibu na majengo ya Bunge Mjini Dodoma.
 Wanamlisha keki binti yao wa Kwana Anna Sikapundwa Mwanafunzi chuo cha Biashara ASEK  Dodoma.
 Wanamlisha keki mtoto wao wa tatu mwalimu Michael Sikapundwa Manispaa ya Morogoro Mwanafunzi wa Open na Media.
Wanamlisha mtoto wao wa mwisho Bw. Emanuel Sikapundwa Dereva wa nyumbani na nimjasilia mali.
 Wanamlisha keki binti wa kwanza wa mama mdogo Mwl Mwanafunzi Mtwara Magegreth Mwakyusa
 Mama mdogo Yunes Bilal Mwakyua analishwa keki
 Wanamlisha kike mama mkwe wao Mrs Micaheli mwalimu Manispaa ya Morogoro
 Wanamlisha keki mke mtarajiwa wa Emanueli Mama Esta Mwajuma Bushiri
 Wakijiandaa kuwalisha mama wakwe zao
 Kukabidhiwa keki kwa ajili ya baadaye wakati wa mapumziko
 Kumlisha keki mtoto Sarah mwanafunzi Dodoma Seko
 Kumlisha keki mjukuu wa Maico carlen
 Mwalimu Maiko akieleza wasifu wa baba na mama yake kama MS katika hafla hiyo
 Mama Sikapundwa akisema jambo kuhusu safariya maisha yao hadi kufikia hapo wakiwa na watoto watano na wajukuu wanne.
 Picha ya Bw.na Bibi Sikapundwa na wajukuu
 Wajukuu wakisakata rumba waliloandaliwa na DJ wakiwaburudisha babu na bibi na waliyo hudhuria
Mrs,Mama Magreth Nelson Mwakyusa mtaalamu wa kutengeneza keki za ngazi zote kwa bei poa na ni mpambaji wa kumbi za sherehe anapatika kota za makole ,mkabala na majengo ya Bunge mjini Dodoma.kwa wakazi wa Dodoma na mokoa ya jirani mnaweza kupata huduma kutoka kwake.



Bwana Christian Sikapundwa amefikia umri wa miaka 60, ambapo ilipofikia tarehe 25/12/2013 ilikuwa ukomo wa Utumishi wa Umma Serikalini, akiwa mwalimu na Mhariri wa Magazeti vijijini Kanda ya Kusini.
Kwa namna ya pekee familia yake iliamua kufanya hafla fupi ya kumpokea Mstaafu huyo,ili kuungana na familia yake kwa namna moja ama nyingine ni kitendo cha kumshukuru Mungu kwa kumweka salama hadi siku ya mwisho ya kustaafu kwake akiwa na afya njema.
Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa nyumba yake iliyojumuisha watoto wake wakiume na wake zao,watoto wakike pamoja na wajukuu wake.
Aidha pia ilimjumuisha na Baba Mkwe wake Mzee Dickson Bilali mwenye umri wa miaka mia moja na siku tatu,akiwa bado na afya nzuri na mwenye uwezo wa kusoma maandishi ya Biblia bila miwani.
Aidha mzee huyo alisema  kuwa baadhi ya vijana wa siku hizi hawawezi kufikia umri wake kwa sababu ya mabadiliko ya maisha yanayo wafanya vijana wengi kuiga matendo mbalimbali ya nchi za nje,na kwamba vyakula vingi vimekuwa na kemikali nyingi ikilinganishwa na vyakula walivyo vitumia enzi ya ujana wake.
Ili kuwapa picha halisi ya maisha ya Bwana Sikapundwa Mke wake Mrs Sikapunwa alisema neno kuhusu maisha ya Bw. Na Bibi Sikapundwa, alisema kwa niaba ya familia kuwa ili walazimu kufanya hafla hiyo kwa lengo la kumshukuru Mungu kumpa afya njema akiwa kazini hadi siku yake ya mwisho alipokabidhi ofisi.

Tuesday, December 31, 2013

HANDING OVER THE CERTIFICATE OF HAND OVER TO JUMA T, NYUMAYO





Handing over the certificate of hand over to Mr Juma T. Nyumayo as a new Editor of Southern Zone.Ruvuma,Lindi and Mtwara.

Friday, December 27, 2013

KILA CHENYE MWANZO HAKIKOSI KUWA NA MWISHO.HII NI SIKU AMBAYO ILIKUWA YA MWISHO WA UTUMISHI WANGU WA UMMA KANDA YA KUSINI







WATOTO WA SHULE YA AWALI CHARITY UWANJA WA SABASABA SONGEA WAMALIZA ELIMU YA AWALI

Mgeni Rasmi Bwana Bakule bakule maarufu kwa kuwa na timu yake ya miguu Matarawe Songea aliahidi kutoa mchango wake wa shilingi laki mbili.
Aidha alisema kuwa elimu ya Awali ni muhimu sana kwa kuinua taaluma hasa shule za English Medium,na kwamba alisema wakaze uzi wa kuendeleza watoto hao hadi darasa la saba
 Baadhi ya mwanafunzi wa Awali akimkabidhi shairi Mgeni Rasmi siku hiyo ya Awali
 Wanafunzi hao wakisoma shairi bila kubabaika utadhani darasa la saba kumbe ni watoto wa Awali

Baadhi ya wazazi wa watoto waliyo maliza elimu ya Awali siku hiyo