Thursday, August 22, 2013

ZIMBABWE, RAIS ROBERT MUGABE AAPISHWA KWA AWAMU YA 7 SASA , KULIONGOZA TAIFA HILO .

RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe aapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo kwa awamu ya 7,mbele ya halaiki ya wananchi wa nchi hiyo pamoja na Baadhi ya Viongozi kutoka mataifa ya Afrika.
Sherehe hizo zimefanyika Mjini Harare ambao watu 60 elfu walishuhudia shughuli hizo,ambazo zimewafahya washiriki wa vyama vya upinzani wakikosa raha kwa madai uchaguzi haukuwa wa haki.Lakini mataifa yamekubaliana na matokeo hayo na kuapishwa kwa Mugabe ni kwa halali.Na ndiyo maana ameahidi kuwa atakuwa mwamifu katika kulitumikia Taifa la Zimbabwe.
Lakini Wapinzani wanguwa wanatambua kuwa anayemchagua kiongozi ni mwananchi mwenyewe, mtu akipata kura nyingi inamaana wapiga kura ndiyo wamempenda aliye mpenda.Na kama hukuchaguliwa basi wananchi hawana imani na wewe,kwa nini useme haiwezekani kura zimeibiwa, je una uhakika gani kama kura zimeibiwa? kwani wakati wakupiga kura ulikuwepo kwa kila mpiga kura ukaona wamekuchagua ambapo ilikuwa ni siri yao.na wakati wa kuhesabu zikiwa zimepungua hapo utakuwa na haki ya madai hayo.


Thursday, July 25, 2013

TUNAJIFUNZA STORI YA USTAARABU WA PWANI KWA KUTEMBELEA MAENDOA YA KISTORIA NA KUONA JINSI MABABUZETU WALIVYO FANYISHWA KAZI NA WAGENI WALIYOINGIA PWANI YA AFRIKA MASHARIKI KATIKA MJI WA BAGAMOYO

 Ukristo ulivyo ingia Bagamoyo,wamisionari walijenga jengo hilo kuwa la mapadre.
 Lakini pia walivyoingia Waarabu Bagamoyo wakafika na Ustaarabu wao wa kiislamu ambapo walikuwa wafanya biashara kwenda bara kutafuta pembe za ndovu na watumwa.jengo hilo ndilo lilikuwa la matajiri  wa kiarabu wafanya biashara jengo lililojengwa matumbawe.
 Hilo ni handaki ambalo lilijengwa na wamisionari kwa ajili ya kujihami na maadui ,hilo handaki limeenda kadi kanisani,nyumba za mapadre chini kwa chini.ambapo sasa halitumiki limewekewa mifuniko kwa ajili ya ukumbusho na watalli kwenda kuona mji Mkongwe wa kihistoria Bagamoyo.


Friday, July 19, 2013

MABOMBA YA GESI ASILIA YAPAKULIWA KATIKA BANDARI YA MTWARA WAZIRI MKUU WA MIZENGO PINDA ASHUHUDIA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw.Simba Kalia walishuhudia shehena ya mabomba ya kupitishia Gesi yakipakulia kutoka katika meli.
Baada ya ushuhuda huo Waziri Mkuu amarejea Mkoani Ruvuma kuendelea na Ziara yake ambapo leo amefanya ziara Muhukuru na kwenye daraja la Umoja wa Tanzania na Msumbiji.

VIONGOZI WA WATENDAJI WA TUJIFUNZE KUSINI JANA WALIUNGANA NA WANANCHI WA AFRIKA KUSINI KUMPONGEZA NA KUMTAKIA AFYA NJEAMA MWANAHARAKATI RAIS WA ZAMANI MZEE NELSON MANDELA MADIBA KWA KUTIMIZA MIAKA 95 YA KUZALIWA

VIONGOZI na watendaji wa TUJIFUNZE KUSINI jana walijumuika na wananchi wa Afrika Kusini katika maazimisho ya miaka 95 yakuzaliwa  mwanaharakati wa nchi hiyo aliyopinga ubaguzi wa rangi hadi kwenda jela kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa nchi hiyo,na hatimaye akawa Rais ,na sasa Rais mstaafu mzee Nelson Mandela.
Tunamuombea Mungu ampunguzie makali ya kuugua kwake ,na apate afya njema kwani bado mchango wake  unahitajika.
Ambapo Mkewe alisema hali ya mzee huyo kwa sasa inatia matumaini,anaendelea vizuri,kwa hiyo Mungu ataendelea kumpa nguvu na kuwa na afya njema.Tunazidi kumuombea kwa Mungu afya yake irejee kama awali.

Wednesday, July 17, 2013

WANAHABARI WALIYORIPOTI AJALI ILIYOTOKEA KWENYE MSAFALA WA WAZIRI MKUU JANA ENEO LA NAMTUMBO WATIMULIWA KWENYE MSAFARA HUO, NA AJALI NYINGINE YATOKEA MBINGA GARI LA POLISI

WAKATI mwandishi wa Waziri Mkuu kuwatoa waandishi wawili wa mkoani Ruvuma  kwa kuripoti ajali iliyotokea kwenye msafara wa Waziri Mkuu jana katika eneo la Nantumbo , leo tena ajali nyingine imetokea kwenye ziara ya wilaya Mpya ya Nyasa na Mbinga ya gari la polisi.Hakuna aliyetangaza hiyo.

Kumbe ajali Zinapotokea za Waziri Mkuu hazitakiwi kutangazwa, Na waandishi wa habari ambao si wa Waziri Mkuu? Na waandishi wa Mawaziri wakuu wamepata mafunzo ya kuwakataza waandishi wengine wasitangaze matukio yanayotokeayawe  mazuri au mabaya katika Ziara ya Waziri Mkuu,na watangaze wao na wasipo tangaza basi, sasa nini maana ya uandishi wa habari?

Monday, July 15, 2013

WAZIRI MKUU WA JAMHURU YA MUUNGANO WA TANZANIA MIZENGO KAYANZA PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI LA CHUO CHA UALIMU KIUMA BONITE TUNDURU

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Kayanza Pinda


WARIZRI Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ameweka jiwe la msingi chuo cha Ualimu Kiuma Bonite Tunduru ,Chuo  kinacho milikiwa na Mkurugenzi Dkt.Matomola,ikiwa ni Taasisi kubwa inayo unganisha Chuo cha Waganga,shule msingi na  sekondari na shughuli nyingine za maendeleo.
Mhe.Pinda alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa shirika hilo la Bonite ambalo linaliletea maendeli wananchi wa Tunduru, Mkoa wa Ruvuma na majirani pamoja na Taifa kwa ujumla.na kwamba alimshukuru sana Dkt Matomola kwa moyo wake wa uzalendo wa kuanzisha taasisi kubwa kama ile kwa manufaa ya taifa, badala ya kujinufaisha mwenyewe.
Aidha mhe.Pinda katika mkutano na  wananchi mjini Tunduru leo, alisema ushururu kwa watu wadogo wadogo usitozwe, maana unaleta kero kwa wananchi wa hali ya chini.
Kuhusu maendeleo ya elimu wilayani humo, Mhe. Pinda amemwambia Mkuu wa mkoa kuwa asili 30 ya watoto wote waliyo faulu kuingia Kidato cha kwanza, ambao hawaja ripoti waende shule mara moja.
Ambapo kuhusu ujenzi kwa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Namtumbo hadi Tunduru utaendelea kujengwa baada ya wakandarasi wa  awali kufukuzwa kwa kushinda kukamilisha katika muda waliyo pangiwa.
Waziri Mkuu amesikia kilio cha watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambao wamekaa  kwa miaka mingi bila kupata uhamisho kama vile ndiyo wamehamia, amewaambia mara baada ya kufika Songea ataangalia nini cha kufanya. ( Na. Juma Nyumayo katika Msafara wa Waziri Mkuu mkoani Ruvuma )