Thursday, April 25, 2013

SHULE YA KWANZA KATIKA KUFAULISHA KATIKA MANISPAA YA SONGEA IMEPATA KIKOMBE NA YA MWISHO IMEPATA NGAO

 Naibu Meya Wilon Kapinga akimkabidhi mwakilishi wa shule ya msingi Mfaranyaki zawadi ya Kikombea
Mwakilishi wa shule ya msingi lupapila wamepata ngao kwa kuwa wa mwisho kufaulisha katika shule za msingi za Manispaa hiyo.

HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA KULIPIA ADA YA MWAKA MOJA KWA WANAFUNZI WATATU WALOFANYA VIZURI MITIHANI YAO MWAKA JANA DARASA LA ZABA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Songea Bw.Nachoa Zatcharia  akielezea hali ya elimu ilivyo katika manispaa hiyo kwenye kikao cha Tathimini ya elimu mwaka 2013 ,kilicho fanyika katika ukumbi wa Songea Club leo.
Amesema kuwa pamoja na kuongoza kwenye matokeo kimkoa lakini bado changamoto bado zipo ni lazima zijadiliwe kwa makini na wadau wa elimu ili kuinua taaluma katika manispaa hiyo,Na kwamba wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi ,Manispaa hiyo itawalipia ada ya bweni ya sh.70,000/= kila mmoja kwa mwaka mmoja,
Wanafunzi hao ni pamoja na Sunday Msinza kutoka shule ya msingi Majimaji aliyepata alama 215 kuchaguliwa Mzumbe wa pili ni Ayoub Cosmas Ilomo aliyepata alama 213 na kwenda Kibaha na watatu Msichana Genoveva  Ndunguru  aliyepata alama 202 na kwenda Msalato.
 Afisa elimu Taaluma wa manispaa hiyo Bi.Consesa Mbena Kisoma taarifa ya elimu ya Manispaa hiyo
 Baadhi ya wadau wa elimu
Afiesa Elimu wa Manispaa hiyo Bi.Edith Matata Kagomba

MKUU WA WILAYA YA SONGEA AWATAKA WENYE MADARAKA KUFANYA KAZI ZAO KWA UFASAHA,WALIMU WAFANYE KAZI ZAO WAKIZINGATIA KANUNI,ILI KUINUA TAALUMA

 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Joseph Joseph Mkirikiti aliyekuwa Megeni rasmi katika kutathimini elimu katika Manispaa ya Songea leo.Bw.Mkirikiti alisema kila mmoja aliyepewa mamlaka katika Manispaa hiyo lazima atekeleze wajibu wake ipasavyo.
Aidha alisema kuwa kwenye mambo magumu wasifanye kuwa rahisi hasa katika kuinua taaluma katika Manispaa hiyo.Walimu wawajibike ipasavyo katika kufundisha,wasimamie watoto,wafundishe kwa upendo.
Kamati za shule na Bodi za shule ziwajibike kwa wanafunzi na wazazi katika uhamasishaji wa maendeleo ya elimu.
Alisema kuwa madiwani wote wafanye kazi kwa bidii bila kujali itikadi zao,kwa hiyo kamati za shule,bodi za shule wenyeviti wa serikali za mitaa na walimu wakifanya kazi zao kwa ufanisi matokeo mazuri yataonekana.
h
 Afisaelimu wa sekondari Manispaa ya Songea Bw.Leo L. Mapunda

 Mkuu wa Wilaya Bw.Joseph Joseph Mkirikiti kulia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Bw.Nachoa Zacharia
 Waheshimiwa madiwani
 Baadhi ya wadau wa elimu
 Waheshimiwa madiwani
Naibu Mstahiki Meya Wilon Kapinga akifunga mkutano huo,na kuagiza kwa wadau wa elimu kwenda kuyafanyia kazi maazimio yote yaliyo jadiliwa katika tathimini hiyo.Na kwamba kila mtu akatekeleze majukumu yake katika eneo lake la kazi.

Wednesday, April 24, 2013

BREAKING NEWSSSSSSSSSS,CHUO KIKUU KIMOJA NCHINI UINGEREZA KIBUNI MBINU YA KUPUNGUZA WIZI WA BAISKELI KWA ASILIMI 62,IKIWA MBINU YA PICHA YA MACHO WAILI

 Picha hiyo iliyo na ujumbe usemao ( We are watching You ) imebuniwa na chuo kikuu kimoja Nchini Uingereza,kwa lengo la kupunguza wizi wa Baiskeli nchini humo.Kwa taarifa ya usalama nchini humo inasema wizi wa baiskeli umeshamili kwa asilimia 63%.
Lakini kutokana na picha hiyo kuwepo,imesaidia kupunguza  wizi huo kwa asilimia 62%, Lakini ukiangalia kwa makoni macho hayo yalivyo pamoja na ujumbe wake kweili unaweza kumsuta mwizi , kujikuta anaonekana na watu hivyo anaacha kuiba Baiskeli.
Ukiitazama picha hiyo utakuta macho hayo yameelekeza kwenye baiskeli zilizowekwa,na yamekazia hasa kwenye baiskeli hizo.

Tuesday, April 23, 2013

RAIS UHURU KENYATTA ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI LENYE MAWAZIRI 18, KATI YA HAO AMETANGAZA WANNE NA WENGINE WATAENDELEA KUTANGAZWA.

 Rais Uhuru Kenyatta ametangaza Baraza la mawaziri lenye Wizaza 18.Ameanza kutangaza Wizara nne,ambapo amemtangaza Dkt.Fredy Matiang'a.Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ( ITC) Ministry of Information ,Communication and Technology, aliye simama kulia kwake.
 Wapili ni Bw. Henry Rotich waziri wa Fedha (Ministry of National Treasury )
 Watatu alikuwa Bw.James Wainaina Masharia Waziri wa Afya ,( Ministry of Health}
 Na wanne alikuwa Balozi Amina Mohamedi Mwanasheria  Ministry of Foreign Affairs
 Waandishi wa habari ambao walikuwa wakirusha kipindi hicho live ni Source wa Blog hii
Ni waandishi wa kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu ya Kenya wakati Baraza la mawaziri likitangazwa.


RAIS Uhuru Kenyatta na Makamu wake Willium Rutto leo wametangaza Baraza jipya la Mawaziri,Lakini kati ya hao, Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mawaziri wanne ambao si wanasiasa.Ni tukio la kistoria kufanyika nchini Kenya.

Rais aliwataja Mawaziri hao kuwa ni pamoja na :-
  • Dkt. Fredy Okengo Matiangi Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ( ITC ).Ministry of  Information, Communication and Technology ( ITC )
  • Henry Rotich Waziri wa Fedha ( Ministry of National Treasury )
  •  James Wainaina Masharia  Waziri wa Afya ( Ministry of Health )
  • Balozi Amina Mohamed Ministry of Foreign Affairs

Alisema majina mengine yataendelea kutangazwa ,na kwamba kazi itaanza mara moja kuaznia kesho.Alisema Kenya ina wasomi wengi na wataalamu wengi lakini Katiba ya Jubilee imeweka kikomo cha kuchagua baraza la mawaziri kwa lengo la kupata baraza dogo ,ambalo lilisizidi wizara 22.
Kwa kutokana na wizara nne zilizotangazwa kutabakia na wizara 14 ambazo zitaendelea kueleweka hapo baadaye.
Kamati ya Bunge itawachunguza mawaziri hao na wengine kuona kwamba watalisaidia taifa la Kenya na watu wake katika kusukuma mbele maendeleo.
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wa kwake Willium Rutto walifika mbele ya waandishi wa habari bila Wapambe wao wakiwa  wamevalia mashati meupe na tai nyekundu bila makoti

Monday, April 22, 2013

BEAKING NEWSSSSSSSSSSSS: KUFUKUZWA BUNGENI NA KUJIUZURU KWA WAZIRI WA ELIMU KUNA UHUSIANO GANI ? BAADHI YA WABUNGE WALIYOFUKUZWA BUNGENI KWA UTOVU WA NIDHAMU WANADAI KWANINI WAZIRI WA ELIMU HAJIUZURU.

Watanzania tufike mahali tuseme, kuwa kuwepo na vigezo ambavyo vitasaidia kumpata mwakilishi wa jimbo lao Bungeni ambaye ni mwadilifu, sio tu anajua kuwashawishi wapiga kura wake na kisha akachaguliwa baadaye akawa kituko Bungeni.

Kuna msemo kuwa zamani watu walikuwa wakishindwa kuhoji mambo na wasomi walikuwa wachache na wale wachache walishindwa kuhoji kwa kuwa waliogopa kutia kitumbua chao mchanga,ni hoja yenye maantiki,Je sasa wasomi wengi wanye kisomo cha juu na wenye kujua kuhoji, kumekuwa na tofauti gani ya mwanzo wasomi wachache na waliogopa kuhoji na sasa wasomi wengi wanahoji mambo mengi kimaendeleo na heshima Bungeni?.

Utovu wa nidhamu ndani ya Bunge letu kumefanya baadhi ya Waheshimiwa wa bunge wakae nje ya Bunge kwa siku kadhaa.sasa cha ajabu wabunge hao wanamadi mengi kimsingi hayana uhusiano na kufukuzwa kwao.

Mf.Mbunge mmoja anadai kwanini waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt Shukuru kawambwa hajiuzuru,hivyo Waziri huyo ndiyo aliyewaambia wakosenidhamu wakati wa majadiliaano ndani ya Bunge.Mbona wanapenda kumwandama waziri huyo bila sababu.

Hivyo Waziri huyo ndiyo alikuwa na wanafunzi siku ya kufanya mitihani na kuwaambia wachore picha kwenye karatasi za majibu au kutukana matusi ama kuandika  mistari ya Rap kiasi cha Album nzima,chonde tumrudie Mungu.

Dkt Kawambwa wakati shule utitiri za Sekondari za Kata zikijengwa nchini ndiye alikuwa Waziri wa Wizara hiyo, kwa nini  wasiwahoji waliyokuwa katika Wizara hiyo kuwa kwanini walianzisha sekondari zisizo na walimu, maabara, nyumba za walimu, majengo ya utwawala, vitabu vya kufundishia na kujifunzia na kama yote hayatoshi, Madai ya walimu yalianza kipindi hicho hicho  na yeye amekabidhiwa tu.

Chamsingi hapa tujitafiti tuone tumekosea wapi katika Elimu Nchini na siyo kujiudhuru  kwa Waziri Kawambwa ,kwa mtindo huo watajiuzuru wengi katika Wizara hiyo maana inachangamoto kibao,kisha ni kubwa mmno.

Saturday, April 20, 2013

MKUU WA WILYA YA NACHINGWEA BI. REGINA CHONJO AAGIZA WAENDESHA BODABODA KUPATA LISENI YA UDEREVA WA PIKIPIKI

Mkuu wa Wilaya ya Nachingewa Mkoani Lindi Bi.Regina Chonjo amewaagiza waendesha bodaboda wa Wilaya hiyo kupata liseni ya kuendesha pikipiki,ili kupunguza ajali zinazotokea wanapowakimbia askari wa usalama barabarani kwa kuwa hawana liseni.
Bi.Chonjo alisema bodaboda ni kazi,hiyo ili wafanye kazi hiyo kwa umakini ni lazima kila mmoja wao apate liseni.
Alisema hayo wakati akiongea na waendesha bodaboda hizo mjini Nachingwea,na kwamba waendesha bodaboda hao wameshapata mafunzo ya usalama barabarani na hivyo itakuwa ni rahisi kwao kupewa liseni.( Source ITV )