Thursday, February 14, 2013

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AKERWA NA WATU WAZIMA WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu.akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake leo.

Afisa Eilimu Mkoa wa Ruvuma

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu ametoa siku kumi na nne kwa wazazi na walezi ambo hawaja wapeleka shule za sekondari watoto wao ambao wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka huu.
Pia kuwatahadharisha watu wanaofanya mapenzi na wanafunzi ambao ni watoto wadogo,amesema watu wazima kufanya mapenzi na watoto ni dhambi pia ni kosa la jinai,matokeo yake wanawapa  mimba na kuwakana kwamba hawahusiki.  Atakaebainika atachukuliwa hatua.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo katika ofisi yake leo alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu tatizo hilo la watoto wengi ambao wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani humo lakini hadi tarehe 14/2/2013 hawaja pelekwa shule.
Ameagiza wakuu wa wilaya,wakurugenzi,mkatibu tarafa ,na watendaji  wa vijiji na mitaa ambao wanaishi wa wazazi na walezi wa watoto hao kuwahimiza kuwapeleke shule kabla ya tarehe 01/03/2013 kwa hiyari yao, na kwamba baada ya tarehe hiyo kupita wazazi na walezi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha Bw.Mwambungu amesema tatizo hapa sio ada bali ni miundombinu ya wazazi na walezi wa watoto hao kuwa mibaya.Kwa kuwa ada ya  shule ni shilingi 20,000 kwa mwaka,muhula wa kwanza shilingi 10,000 na muhula wa pili shilingi elfu kumi.
Aidha alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani humo mwaka huu ni 16,578 lakini walioripoti ni 9,388 tu, na wanafunzi 7,190 hawajaripoti katika shule za sekondari walizopangiwa.
Pia amesema kuwa waandishi wa habari wananchi na viongozi wa ngazi zote mkoani watoe taarifa za haraka kwa uongozi wa wilaya na mkoa kwa watu wazima wanaojihusisha kufanya mapenzi na wanafunzi ambao ni watoto wadogo,na kuwasababishia mimba.
Amesema tatizo la mimba kwa wanafunzi ni kubwa mmno kwa sababu ya kulindana na wale wanaowapa mimba wanafunzi.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID THABITI MWAMBUNGU AMETOA SIKU 14 KWA WAZAZI NA WALEZI AMBAO WATOTO WAO HAWAJA RIPOTI SEKONDARI KIDATO CHA KWANZA , BAADA YA ZIARA YA KUSHITUKIZA KATIKA SHULE 5 KWA KILA WILAYA

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake leo.
 Mkuu wa Wilaya Songea Bw.Joseph Joseph Mkirikiti
 Afisa Elimu Mkoa ( REO ) Ruvuma.
Baadhi ya waandishi wa habari.wakimsikiliza mkuu wa mkoa.

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu ametoa siku kumi na nne kwa wazazi na walezi ambo hawaja wapeleka shule za sekondari watoto wao ambao wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka huu.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo katika ofisi yake leo alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu tatizo hilo la watoto wengi ambao wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani humo lakini hadi tarehe 14/2/2013 hawaja pelekwa shule.
Ameagiza wakuu wa wilaya,wakurugenzi,mkatibu tarafa ,na watendaji  wa vijiji na mitaa ambao wanaishi wa wazazi na walezi wa watoto hao kuwahimiza kuwapeleke shule kabla ya tarehe 01/03/2013 kwa hiyari yao, na kwamba baada ya tarehe hiyo kupita wazazi na walezi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha Bw.Mwambungu amesema tatizo hapa sio ada bali ni miundombinu ya wazazi na walezi wa watoto hao kuwa mibaya.Kwa kuwa ada ya  shule ni shilingi 20,000 kwa mwaka,muhula wa kwanza shilingi 10,000 na muhula wa pili shilingi elfu kumi.
Aidha alisema kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mkoani humo mwaka huu ni 16,578 lakini walioripoti ni 9,388 tu, na wanafunzi 7,190 hawajaripoti katika shule za sekondari walizopangiwa.

Tuesday, February 12, 2013

MAZINGIRA MAZURI YA KUFUNDISHIA NI PAMOJA NA VIFAA KATIKA SHULE ,MKUU WA SHULE KALEMBO SEKONDARI BW.HAULE ANATHIBITISHA UKWELI HUO

 Mkuu wa Shule ya sekondari Kalembo iliyoko katika Manispaa ya Songea Bwana Bosco Haule alithibitisha usemi huo katika ofisi za TUJIFUNZE wakati alipofika kuchukua maandalio ya masomo kwa walimu wake ambavyo alivichapisha. Bwana Haule ni yule aliyevaa kaumda suti ya buluu nyepesi pamoja na mhariri wa Ttujifunze  Ofisini kwake hivi karibuni.

Bw.Haule ameshika maandalio ya masomo kwa ajili ya walimu wake ,ambayo atayagawa kwa walimu ili kupunguza ghasia ya kuandalia kwenye karatasi.

POPE BENEDICT XVI ANNOUNCES HIS RESIGNATION IN A SURPRISE STATEMENT

Pope Benedict XVI is to resign at the end of this month after nearly eight years as the head of the Catholic Church, saying he is too old to continue at the age of 85. That is a  strong  courageous step his resignation, actually  ages matters to a very important position of a Pope has , I support his decision.

Analysts say Europeans - and Italian-speakers specifically - are still among the favorites, but strong candidates could emerge from Africa and Latin America, which both have very large Catholic populations. There for we pray to God to get another Pope any were from the World, if from Africa it will be better.

The miracle from God will happen at the end of this month at Vatican after prayers from Cardinals to find out new Pope.

KWA NINI BINADAMU TUNASHINDWA KUWA WAVUMILIVU KATIKA MAISHA YETU ? KWA NINI WATU WAPIGANE HADI KUPOTEZEANA NAISHA KWA AJILI YA NANI KACHINJA NYAMA?

Jambo la wananchi kuchukua jukumu la kupigana hadi kutoana maisha kwa ajili ya nani kachinja ng'ombe au mbuzi.Imani hizi zitatupotezea heshima ya Taifa letu ambalo linajulikana kama kisiwa cha Amani.Kila mtu anahaki ya kuwa na imadi yake ya kuabudu ila inapofikia kwenye uhalali wa uchinjaji ikibainika kwa nini waumini hao wasiache kwenda kununua nyama ambayo haikufuata taratibu ya uchinjaji hadi imalizike buchani.
Ni jambo la kusikitisha sana,Serikali isilifumbie jicho tukio hilo lilotokea hivi katibuni za waumini wa Kikristo na Kiislamu kupigana,kuchoma bucha na hata kupoteza uhai wa watu,lisitokee tena sehemu nyingine busara haitaji kwenda shule.Wote ni ndugu moja.

UAMUZI WA KUJIUZURU UPAPA ,PAPA BENEDICT KWA UMRI WA MIAKA 85 NI WA BUSARA SANA KWA KANISA NA KWA WAUMINI WAKE

Uamuzi wa Papa kutangaza kwake kutaka kujiuzuru ifikapo saa sita usiku wa tarehe 28 mwaka huu ni wa busara sana kwa Kanisa na kwa waumini wa kanisa hilo.
Papa amesema kuwa umri wa miaka 85 aliyokuwa nayo inatosha katika kutoa huduma kwa kanisa hilo,ameona ni vyema aachie ngazi apishe mwingine aendeleze Utume huo ambaye atakuwa na nguvu na afya ya kutosha katika Utume huo.
Wapembuzi wa mambo wanajaribu kuangalia nani atakuwa mrithi wake,kutoka Barani Ulaya,Marekani ya Kaskazini au barani Afrika.
Uwezekano ukawepo Bara la Amerika na Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya waumini wa Kanisa hilo la Roman Catholic.Yote tuna mwachia Mungu kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu kwa Makadlnali watako kutana kwa kazi hiyo.

Ambapo ishara ya moshi huo wa kuonyesha sala  na maombi ya kumpata Papa mpya yamekubalika,Sala na maombezi ya waumini hao Duniani kutasaidia kazi hiyo kuwa nyepesi.

Sunday, February 10, 2013

MANISPAA YA SONGEA JUMAPILI

 Leo pitapita zangu katika mitaa ya Manispaa ya Songea
Na kwa mbali ni soko kuu la Manispaa ya Songea