Monday, July 30, 2012

MWALIMU APEWA MKONG’OTO NA WANAFUNZI WAKE KWA KUFUNDISHA SIKU YA MGOMO WA WALIMU SONGEA



BADHI ya wanafunzi wa shule ya msingi Kambarage Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamempatia mkong’oto mwalimu   aliyejulikana kwa jina la Kahimba kwa madai ya kuwa na kuherehere cha kufundisha wakati walimu wengine wapo kwenye mgomo ulifanyika nchi nzima,wakidai kuwa mwalimu huyo amewasaliti walimu wenzake na viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania.
   Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambarage Bibi Adolophine Ndunguru katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea alithibitisha tulio hilo kuwa lilitokea majira ya asubuhi.
    Aidha Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Luya Ngonyani,alisema kuwa Mgomo wa Walimu ni halali umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004.
     Alisema kuwa hatua ya kwanza ya Chama Cha Walimu  (CWT ) imetekeleza kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu namba 1 kwa lengo la kudai  maslahi yao.
    Wakati Uongozi wa Manispaa ya Halmashauri ya Songea wakitaka kuitisha mkutano wa Waratibu Elimu Kata na Walimu wakuu wa shule wa Manispaa hiyo leo katika shule ya msingi Mfaranyaki uligonga mwamba baadaya wa Waratibu na walimu wakuu hao kuacha kwenda kwenye mkutano huo.
  Serikali isifanyie mzaha kuhusu tukio hilo,sio suala la kusema shauri lipo mahakamani ,walimu warudi shuleni kufundisha,Sekta ya Elimu ni Sekta nyeti si ya kuichezea chazea kama wengine wanavyo dhani,Mwalimu anaweza akapindisha Mtaala wa Elimu akafanya kinyume na Sera ya nchi kwa muda mfupi sana.Lakini watu hawaoni hayo." kilio cha walimu ni kurudishiwa Teaching allowance".

Saturday, July 21, 2012

WAFANYA BIASHARA WASISABISHE MWEZI RAMADHANI KUWA MWEZI WA MAJONZI NA MAJUTO BADALA YA FARAJA KWA WANAO FUNGA -SHEKHE JONGO

Shekhe Himidi Jongo akielezea umuhimu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo leo ni mfungo mosi.Aidha na kuwaomba wafanya biashara nchini kuacha kupandisha bidhaa bei.


Wafanya biashara wameshauriwa kuacha kupandisha vitu bei kwa sababu ya mfungo wa Ramadhani,Shekhe Hamidi Jongo wa Dar es Salaam alisema hayo kwenye kipindi maalumu cha TBC jana wakati akielezea umuhimu wa kufunga kwa waumini wa Dini ya Kiislam.
Alisema Mungu alihalalisha biashara kufanyika na aliharamisha riba katika biashara,hivyo kufanya bishara siyo dhambi  bali kupandisha vyakula wakati huu wa mwezi Mtukufu wa ramadhani ni dhambi kwani bei ya jana kabla ya mfungo kwa nazi,mhogo,mchele kwanini leo siku ya mfungo mosi ipande? ‘Wasifanye mwezi Ramadhani uwe ni mwezi wa Majonzi na majuto badala ya faraja kwa wanaofunga’ alisema Shekhe Jongo.
Aidha alisema kwa mfanya biashara wa Kiislamu awe mkweli kwa wateja wake wakifika kununua mchele au maharage asema kweli kuwa maharage yake yanaiva haraka au yanachelewa kuliko kusema maharage yake ni maji mara moja kumbe uongo.Mtu kama huyo asifunge maana atakuwa anapoteza muda wake bure.
Tuungane na Shekhe  Jongo kuwahasa wafanya biashara wa mhogo,maharage,nazi,tambi,tende wauze bidhaa hizo kwa bei ya halali,wasipandishe bidha hizo muhimu kwani kufanya hivyo ni kuwakomoa  wenzetu watakaojaliwa kufunga,kwani mwezi huu ni mwezi  Mtukufu kwa waumini wa Kiislamu.

Thursday, July 19, 2012

NI JAMBO LA KUFURAHISHA LA KUKUTANA NA BLOGGER MKUBWA NA KUCHATI NAE INAPENDEZA KWELI SI MWINGINE PROFESA MBELE - SONGEA LEO

 Baada ya mapumziko ya safari ya basi kutoka Dar es Salaam kuja hapa Songea Profesa Mbela mwenye shati la mistari pamoja na ndugu zake picha ya pamoja katika ukumbi wa Serengeti ,maarufu sana hapo Songea kwa kupata moja baridi na moto pia,
Hapa Prf.Mbele anajikumbusha kivywaji cha nchi yake almaarufu Kili- manjaro akiwa na Dada Sia  katika ukumbi wa Serengeti Manispaa ya Songea,Prf.Mbele pamoja na kuishi nchini Marekani kikazi,lakini hukumbuka kurudi nchini kwakwe na hasa mkoani kwake na wilayani kwake Mbinga.
Profesa Mbele anaamini kuwa usomi haupungui iwapo msomi akijichanganya na watu wa kawaida,na wala akiwa akiongea na vijana wa vijiweni,Hawampunguzii Uprofesa wake,maana kazi ya Mungu ni kubwa kwa kuwa siyoyote yanayo zungumzwa na watu wa kawaida ni vya upuuzi la,ila kuna mengine yana maana huenda hata alipokuwepo chuoni hakuwahi kusikia.
Mie na mpongeza sana Profesa huyo,kwa kuwa anatambua kuwa kila mmoja na mchango wake katika jamii kulingana na kiwango chake cha elimu au cha uelewa wake kasoma au hapana,endelea hivyo profesa Mbele kwa mtindo huo utachota mambo mengi yanayoizunguka dunia hii.

TUJIFUNZE KUSINI INATOA POLE KWA FAMILIA ZILIZO POTELEWA NA JAMAA ZAO KATIKA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR

TUJIFUNZE Kusini pamoja na timu nzima ya TUJIFUNZE  ikopamoja katika majonzi ya wananchi wa Tanzania Visiwani pamoja na wananchi wa Visiwani ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika ajali nyingine ya meli.Tunatoa pole kwa familia zilizofikwa na msiba huo.
Katika matukio kama haya wananchi tuwe na subira na uvumilivu kwa kuwa yote yanayotokea ni matakwa ya Muweza wetu.Na mara nyingi kunapotokea matatizo watu lazima watu watatupiana lawama.Cha msingi nikumuomba Mungu atuepushie jali za mara kwa mara,hasa zinazotokana na uzembe.

Tuesday, July 17, 2012

MATUKIO MJI WA SONGEA

Watu wawili wanao sadikiwa kuwa ni wazazi wa mtoto anyekaa katika maeneo ya Matogoro Manispaa ya Songea wametuhumiwa kumnyonga mtoto wao ambeya alianza kukaa,kwa mijbu wa kikosi cha jeshi la polisi mkoani hapa wazazi hao wanashikiliwa na polisi.
Tukio lingine Kijana ( 25 ) mwendesha pikipiki almaarufu yeboyebo mjini hapa amekutwa amekufa katika nyumba moja maeneo ya Bombambili Manispaa ya songea ,baada ya kutoonenaka kwa tajiri yake kwa siku tatu.inasadikiwa kuuawa na watu wasiyojulikana hadi sasa.
Tukio lingine ni la lori lililobeba mahindi kutumbukia katika daraja la Matarawe barabara ya kuelekea Mji mwema Manispaa ya Songea,Chanzo cha ajali hiyo bado kueleweka vyema hadi tunaenda mitamboni,hiyo ndiyo habari.

Saturday, July 14, 2012

WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA MAKARANI WA SENSA SIKU YA TAREHE 25 /8/2012 SIKU YA KUHESABIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda alisema kuwa siku ya tarehe 25 mwezi wa nane mwaka huu makarani wa sensa watapita katika kaya za watu kuhesabu,kuelewa siku ya kuamkia tarehe 25 ni watu wangapi wamelala katika nyumba ile.
Aidha Mhe.Pinda alisema kuwa wananchi wajitokeze kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya siku Tume ya Katiba ikifika katika maeneo yao.
Mhe.Pinda alisema hayo siku akizindua mradi wa matrekta katika uwanja wa Zimani moto katika Manispaa ya Songea hivi karibuni,siku ya pili ya ziara yake ya siku mbili ya kikazi Mkoani Ruvuma.

Sunday, July 8, 2012

CHUO KIKUU CHA SAUT SONGEA KUANZISHA EVINING CLASS KUANZIA MWEZI WA 9 MWAKA HUU

               CHUO KIKUU CHA SAUT SONGEA KUONGEZA VITIVO

MSHAURI wa wanachuo ( Dean of Student ) Michael Sinienga alisema hayo hivi karibuni kwa waandhishi wa habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Kanda ya Kusini walipotembelea chuo hicho kwa lengo la kupata taarifa za mafanikio na changamoto kadhaa tangu chuo hicho kianze kudahili wanachuo wake.
     Bwana Sinienga alitaja vitivo vitakavyo ongezeka kuwa ni pamoja na ‘Business Administration, Law, Medicine, Mass Communication  and Education’ ambayo ndiyo iliyoanza.
   Matarajio mengine ya chuo hicho ni kutoa kozi fupifupi za ujasiliamali, kozi za jioni ‘Evening classes’  kwa watumishi na watu wengine wenye kutaka kusomea shahada wakiwa kazini.
    Matarajio mengine ni kutoa huduma kwa shule za sekondari ambazo zitakuwa na uhaba walimu na zikipenda kupata huduma hiyo kutoka katika Chuo Kikuu hicho, Pia kuwaandaa vijana kujiamini na kujitambua na maadili kuwekewa kipaumbele.