Thursday, May 31, 2012

MTOTO ACHOMWA MIKONO YAKE MOTO NA MAMA YAKE WILAYANI KILWA KWA WIZI WA BOGA,MAMA AONYA WANAWAKE WENZAKE WASIWE WAKATILI KAMA ALIVYO MFANYIA MTOTO WAKE

Mtoto huyo ambaye jina lake halikupatikana katika Blog hii kama anavyoonekana kwenye picha hafifu lakini mikono yake inaonekana ilivyo fungwa bandeji,ni mkasa aliyoupata kutokana na kuiba boga aliloliweka mama yake mzazi kuliiba ndipo alipochomwa moto mikono yake.Mama yake akamficha ndani huko wilayani Kilwa Mkoani Lindi.
Ni ukatili wa aina yake wa kumchoma mtoto mikono kwa moto ati kaiba boga kweli huo ni uungwana ? kwa wanawake ambao ni mama zetu ?.Kilema ambacho hata kisahau cha kuchomwa na mama yake moto eti kaiba boga,itamwingia akilini kweli.Sasa wana Blog wenzangu hebu tulipembue kwa undani tukio hilo.



MAPENZI YA SABABISHA MTOTO MLEMAVU KUAWA NA KUTUPWA MTONI SONGEA

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma ( RPC ) Michael Kamuhanda anayehamia Mkoa wa Iringa baada ya kuongea na waandishi wa habari mkoani hapa leo katika kumtambulishi Kamanda mgeni wa mkoa huo ( RPC ) aliyehamishiwa hivi karibuni ACP Deusdedit Nsemike hayupo pichani..

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu auawa na bwana wa mama mwenye mtoto Rebeka Cheni na kutupwa mtoni,Kamanda wa Mkoa wa Ruvuma anaehamia mkoa wa Iringa  Michael Kamuhanda leo amewaambia waandihi wa habari kuwa chanzo ya mauaji ya mtoto huyo ni mapenzi.
Alisema kuwa inasemekana kuwa mama wa mtoto huyo aliambiwa na bwana ambaye hakuzaa naye mtoto huyo kuwa wamuue ili waendelee na mapenzi yao kwa raha kwani mtoto huyo alikuwa mlemavu wa akili Tahira,ndipo mama huyo alivyo toka nje na kumwacha mwanae ndani,muda huo bwana huyo mkatili alivyo pata mwanya wa kummaliza mtoto Rebeka.
 Alisema baada ya kufanya kitendo hicho watuhumiwa walichukua mwili wa mtoto huyo na kuitupa mtoni,wasamaria weme walivyo kundua hilo waliitaarifu polisi.Na kwamba wote wako mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea.

KAMANDA WA POLISI ( RPC ) MGENI ACP DEUSDEDITH NSEMIKE MKOANI RUVUMA ATABULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO.NA AKAMANDA WA ZAMANI ANAYE HAMISHIWA MKOANI INGA MICHAEL KAMUHANDA

 Kamanda mgeni wa polisi RPC Mkoani Ruvuma ACP  Deusdedit Nsemike  baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma leo

 picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Ruvuma leo baada ya utambulisho wa RPC Mgeni nje ya jengo la polisi mkoa mjini Songea Kamanda mgeni  Deusdedit Nsemike wa tatu kutoka kushoto.

Bwana Juma Nyuamayo wakizungumza na rpc Michael Kamuhanda leo.
.
KAMANDA wa Polisi (RPC) Mgeni ACP Deusdedith Nsemike Leo ametambuliwa kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa Jengo la Polisi mkoani na Kamanda Michael Kamuhanda anaye hamishiwa mkoa wa Iringa.
  Kamanda Nsemike alisema kuwa atakuwa tayari kufanya kazi na waandishi wa habari,kwani nimuwazi,na kwamba anaomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa waandishi hao japo watapata jambo ambalo ni la uhalifu.
  Aidha alisema kuwa atahitaji utii  wa sheria bila masharti,Mahusiano pamoja na Idara nyingine zikiwemo za Ustawi wa jamii,Elimu,Afya ,michezo na Halmashauri za Wilaya.
  Vilevile alisema kuwa atahitaji ushirikiano na viongozi wa ulinzi na usalama ili kuhakikisha Falsafa ya Polisi Jamii inatekelezwa kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia sheria za nchi.
   Alisema kuwa iwapo wananchi watapata taarifa za fujo,ujambazi,zitaarifiwe mapema katika vyombo vinavyohusika kabla hakujatokea madhara makubwa.
Awali kamanda Michael Kamuhanda aliwaonba waandishi wa habari hao kuwa na ushirikiano wa karibu na Kamanda Nsemike kama vile alivyopata ushirikiano yeye katika kufanikisha shughuli zake za ulinzi na usalama katika Mkoa wa Ruvuma.
Pia akamweleza Kamanda huyo mgeni Mkoani hapa kuwa asiwe na mashaka na waandishi wa mkoa huo katika utendaji wao wa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma Michael Kamuhanda amepata uhamisho kwenda Mkoa wa Iringa, Ni matumaini ya waandishi wa Mkoa wa Iringa watampa ushirikiano wa kutosha Kamuhanda katika shughuli zake,kwani wanahabari ni kioo cha Jamii

Tuesday, May 29, 2012

MADWA YA KULEVYWA NAYO NI HATARIII,BW,JUMA NYUMAYO ANAWAHOJI VIJANA WANAOTUMIA MADAWA HAYO KILWA KIVINJE

Hao vijana walioketi wanatumia madawa ya kulevywa wa Kilwa Kivinje lugha wanayozungumza ni ya ina yake .Mhariri  Msaidizi wa magazeti ya Kisomo vjijini Kanda ya Kusini Bw. Juma Nyumayo  mwenye suluali nyeusi anawahoji vijana hao,kwa nini wanatumia madawa hayo.wanadai kuwa hawana kazi ya kufanya,hivyo wakiyatumia madawa hayo wanakuwa bomba.
   Hivyo kwa hali hiyo tutawafikisha wapi vijana wetu ? ukweli ukiwaona vijana hao utawahurumia,wamekuwa kama mazezeta,tahira hivi.maana wanamawazo ya mbali sana,kwamba meli wana uwezo nazo katika kuzamia.

KILWA KISIWANI NA SONGOMNARA IMEWEKWA KWENYE URITHI WA DUNIA,BW.JUMA NYUMAYO MWANDISHI WA HABARI NA MHARIRI WA MAGAZETI YA KANDA TUJIFUNZE KUSINI ANASOMA KIVUKONI KWENDA KISIWANI

Bw.Juma Nyumayo aliyeshika kibao kilicho andikwa UNESCO- HIFADHI YA URITHI WA DUNIA,Kilwa Kisiwani na Songo Mnara,kibao kilichowekwa kabla ya kupanda maboti kwenda Kilwa Kisiwani ambako kuna majengo ya kihistoria na ustaarabu wa Kiarabu na Masultani na Ngome ya Wareno.
 Huyo ni mfanya kazi katika kivuko hicho ambaye kazi yake ni kutambulisha wageni/watalii wanaokwenda Kisiwani huko kuona mabaki ya majengo misikiti iliyojengwa enzi za biashara za waarabu zikiwemo za watumwa,pembe za ndovu.
UNESCO ndiyo wanaosaidia kufanya majengo yaliyoachwa yawe katika hali ya kuvutia na kupendeza .Tuna vivutio vingi pwani ya kusini mwa Tanzania.

Monday, May 28, 2012

Haya bado hayaja malizika kusombwa kwenye ghala la chakula la Taifa Ruhuwiko Songea ,na mengine yanavunwa sasa.kazi kwa walaji.

Shehena ya magunia ya mahindi ya zamani ambayo bado yanasombwa ,lakini pia wakulima wameanza kuvuna mahindi mapya katika Mkoa huo wa Ruvuma.Ni kazi kweli kwa walaji.