Wednesday, February 22, 2012

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATOA RAI YA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO NA UONGOZI WA MKOA PANAPOTOKE VITENDO VYA UHALIFU

 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabit Mwambungu aongea na wandishi wa habari ofisni kwake leo kupitia vyombo vya habari,kuwaomba wananchi kuwa na uvumilivu wakati serikali ,inafanya jitihada za kutafuta vyanzo vya matukio ya mauaji yaliyotokea siku tatu mfululizo katika Manispaa ya Songea.
Aidha ameomba ushirikiano wa uongozi wa mkoa na viongozi wa mitaa,kata na tarafa wa kuwa na ulinzi shirikishi,kwa kuwa wahalifu wanaishi nao.

Aidha alisema vifo vingi vinasadikiwa vinatokana na imani za ushirikina na uchawi basi na majambazi waningilia hapohapo katika mauaji ya watu,hivyo matembezi ya usiku kama sio ya lazima yaachwe kupisha polisi na ulinzi shirikishi ufanye kazi yake.Na kwamba indapo mtu asiyejulikana,mara moja itolewe taarifa mapema kabla uhalifu haujatokea.
z
 Waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa,alipokuwa akiwataka wananchi wasubiri serikali ifanye kazi yake kushirikiana na viongozi wa mkoa na wananchi kuhakikisha hali ya utulivu inakuwa kama awali,kufuatia maandamano ya wananchi yaliyozuiwa na polisi kwa kutumia mabomu na silaha za moto kuzuia,ambapo watu wawili wamepoteza uhai wao kutokana na majibishano ya mabomu na mawe yaliyokuwa yanatupwa na wananchi.katika manispaa ya Songea leo.
Ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma akiwa na waandishi wa habari

Sunday, February 19, 2012

JKT MLALE YAINGIA FAINALI KATIKA 9 BORA BAADA YA KUMCHAPA POLISI YA IRINGA GOLI MOJA KWA SIFURI KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA

 Ni hicho kikosi kilicho pata tiketi ya kuingia 9 bora wakishika nafasi ya pili katika kundi lao ,anayeongoza ni Mbeya City.
 Wakitoka kwenye chumba cha mapumziko wakiingia uwanjani kumalizia kipindi cha pili.
 Furaha ilivyo wajaa wajeshi hao walipofika kambini kwao Uwanja wa Sabasaba - Matarawe  Katika Manispaa ya Songea.
Waliondika kwa mtindo huo ,ambapo kila mmoja alicheza alivyofikiri kwakuwa hakukuwa na ngoma.Ila kwa kawaida wajeshi hawahitaji ngoma,maana wanaweza wakacheza kwa mtindo wa kwata.Nakumbuka na mie nilipitia katika Jeshi hilo Ruvu JKT.




TIMU ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT ) Mlale imeingia katika tisa bora katika kundi lao,baada ya kuifunga timu ya Polisi ya Iringa bao moja kwa sefori katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea leo.

JKT Mlale ilipata goli la kwanza katika kipindi cha kwanza kwenye dakika 10 lililofungwa na mchezaji namba 3  Ahamad Kibopile,Polisi walijitahidi kurudisha goli lile lakini bahati haikuwa yao hadi mapumziko ikawa goli moja kwa bila..

Katika kipindi mchezo ukawa wakuvutia lakini JKT wakawa wakicheza mchezo wa kujihami zaidi,Lakini Polisi pamoja na ujanja wao haukuweza kufua dafu mbele ya vjiana wa JKT.Hivyo hadi firimbi ya mwisho goli ni moja kwa sufuri.Na kuwapa tiketi ya kuingia fainali,ambapo Mbeya City ndiyo wa kwanza wakiwa na point 22 wakati JKT wanapoint 16.

TUJIFUNZE KUSINI INAWALETEA UTAMADUNI WA WATU WA KUSINI KATIKA KUBURUDISHA KWA NGOMA ZAO

 Kukiwa na sherehe za Harusi,za dini,serikali ama mapokezi ya viongozi mbalimbali ngoma za Lizombe,Kioda,Ligambusa,Mhambo na Mganda zinatumbuiza.
 Hicho ni kikundi cha Lizombe cha Lizaboni katika Manispaa ya Songea kilihusika na mapokezi ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal  wiki iliyopita.Mkoani Ruvuma.
Hicho nacho ni kikundi cha kioda cha akinamama ambacho kilitoa burdani muruwa siku hiyo ya ugeni mkoani hapa.Siku nyingine nitakuletea kila ngoma na maeneo inakotoka kabila ambalo lenye asili ya ngoma husika.

BREAKING NEWS !!! WANAUME HUKO KENYA ( NYERI ) WANAPATA KIPIGO CHA KUFA MTU TOKA KWA WAKE ZAO WANAPOTOKA KWENYE POMBE

 Tunaposema unyanyasaji wa kijinisia kwa wanawake na watoto kutoka kwa baadhi ya wanaume wenye mfumo dume,kwa upande wangu naona wanaume wanaonewa.Mfano mzuri ni kwa huyo mwanaume mwenzetu mwenyeji wa Nyeri jina lake halikutambulika alivyo fanana.je ndivyo alivyo zaliwa na mama yake hivyo.Basi kazi hiyo ni ya mkewe aliyoifanya kwenye uso na kichwa cha mmewe.kisa ati amerudi usiku,amelewa pombe.kisa hicho si cha huyo mwanaume mwenzetu tu yaliyomkuta wiki iliyopita bali waki wengi wanaume wamefanyiwa unyama huo na wakezo huku Nyeri Nchini Kenya.
Huyo naye ni mwnume aliyepata kisago kutoka kwa mkewe baada ya kurudi nyumbani kalewa pombe,yeye ambaye jina lake wanalo wenyewe Nyeri huko nchini Kenya .alipata dhahama hilo kisogoni,shingoni na kichwani ambapo kichwani alikula nyundo ya kichwa.

Wanawake hao wanasema wanaume wakileta za kuleta wanatandikwa.'Kama analeta fujo anapotoka kwenye pombe zake,nikiwa na chochote nitampiga nacho.Maana wao wanakunywa pombe,sisi ndiyo tunahangaika na watoto,kuchuma kahawa wao wanadai fedha za kunywea bila ya ustaarabu'.alisema mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake.

Wasomaji wa Blog hii,ninani alaumiwe,mke au mme?,lakini kama ndivyo je adhabu hizo walizoziamua kuzitoa kwa wanaume wao huko Nyeri inafanana na kuadhibiwa,au ni uuaji? ( Source K24 )

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA IWE YENYE AMANI NA UTULIVU DUNIANI KOTE

Ni jambo la kumshukuru Mungu ambaye ametufanya tupo hapa leo tunavuta pumzi.Ni matumaini yetu tumshukuru kwa kila jambo ambalo tunalolipata ama tunalolikosa.

Saturday, February 18, 2012

MKOA WA RUVUMA ULIKUWA NA UGENI WA MAKAMU WA RAIS DKT MOHAMED GHARIB BILAL KUKAGUA NA KUONA MIRADI

 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal apokewa viwanja vya Ikuli ndogo Songea.
 Kikundi cha Lizombe cha zawadiwa bahasha na mama Asha Bilal katika viwanja vya Halmashuri ya Manispaa ya Songea
Makamu ahutubia baadhi ya viongozi wa chama na serikali na wananchi wakiyofika kumpokea Ikulu ndogo Songea
 Mkurugenzi matendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea akimkabidhi taarifa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu.
 Kikundi cha lizombe toka Lizaboni Manispaa ya Songea kikitumbuiza
Mama Asha Bilal akiwasalimia wananchi na kuwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozionyesha kwenye Sekta ya kilimo.
 Makamu wa Rais akielezea jinsi serikali inavyo thamini mchango wa wananchi katika kilimo na jinsi inavyoruhusu watu wenye fedha zao wanunue mahindi kwa bei ya shilingi 350 kwa kilo na wao wayauzi kokote ndani na nje ya nchi.wakati akiwa kwenye ghala la hifadhi ya chakula la taifa Ruhuwiko.
Hayo ni mahindi ambayo yamehifadhiwa nje ,baada ya maghala kujaa mahindi,ambayo sasa yanachukuliwa na kusafirishwa.




MAKAMU wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal alikuwa na ziara ya kikazi katika mkoa wa Ruvuma ambako alikagua,kutembelea miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa Uranium Wilayani Namtumbo,Ghala la taifa la kuhifadhi chakula Ruhuwiko Songea na Makaa ya mawe Rwanda Mbinga.
 Ziara ya makamu wa Rais imefanyika kwa mafasniko makubwa ingawa sintofahamu zilijitokeza kwenye mrdi wa Uranium,Makamu hakufikishwa kwenye mgodi ili akague eneo la mradi kama ilivyo onyeshwa kwenye ratiba ya matukio ya ziara hiyo.
Watu wanajiuliza kwanini Dkt hakufikishwa kwenye mradi huo mkubwa amabo bado kuanza kuzalisha,Kama hiyo haitoshi kwanini Wizara ya Nishati na madini isipaleke mwakilishi wake au mataalamu wake, kama waziri wa nishati alikuwa na udhuru?.
Kumbe watu wa chini kabisa ambao hawasikilizwi wasemayo ,kumbe walalamikayo ni sahihi,kuwa kila siku kuna helkopta zinatua huko na kuondoka na madini,na kwamba maeneo mengi huko ni mashimo matupu je zinachimbwa Uranium peke yake au kuna madini mengine ambayo yanaibiwa bila ya kueleweka ? kama ni uongo sasa kwa nini makamu wa Rais hakupelekwe kwenye eneo la mgodi ili ajionee mwenyewe.
Wa- Tanzania tutaibia maliasili zetu mpaka lini na hao wanaoitwa wawekezaji kutoka nje? Lakini hatuwezi kushangaa kama twiga kwenye hifadhi ya taifa waliweza kupitishwa na kusafirishwa nje ya nchi kwenye ndege sembuse,madini ambayo yako mbali na mkoa na wilaya.
Hapo kuna mchezo mchafu unafanyika, na hao waliyowekeza kwenye mradi huo na baadhi ya watendaji katika wizara hiyo,huwenda na wadau wengine,kwa utaratibu huo nani amfunge paka kengele ? ( ama kweli mikataba ya madini itatumaliza ).

Friday, February 17, 2012

SERIKALI IMEWATAKA WAKULIMA WA KOROSHO KUVUTA SUBIRA WAKATI IKITAFUTA UFUMBUZI WA KUPATA BEI ITAKAYO WANUFAISHA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabit Mwambungu

WAKULIMA wa Korosho Nchini wametakiwa kuwa na subira wakati huu mgumu
wakati serikali ikiendelea kutafuta suluhisho la kudunmu la kuwa na soko
la uhakika wa mazao hayo.

Wakati hayo yakiendelea tayari wakulima wa zao hilo wapo katika
mkanganyiko wa sintofahamu juu ya hatima ya soko la mazao yao ambayo
wengine wakiwa wanasubiri malipo ya awamu ya pili huku kukiwa na kundi
kubwa pia la wakulima waliopunjwa nguvu zao na vyama vikuu vya ushirika
kwa matumaini ya kuwalipa baada ya kuuza korosho hizo kwa wanunuzi
wakubwa.

Hayo yamesemwa na imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said
Mwambunmgu wakati akiongea na Madiwanai wa Halmashauri ya Wilaya ya
Tunduru Mkoani humo na kuongeza kuwa hali hiliyo imetokana na Serikali
kubaini tatizo la ubabaishaji wa Soko la Mazao hayo katika msimu wa
Mwaka 2011/2012 hali inayo tishia wakulima kuapata malipo ya pili.

Sambamba  na ahadi hiyo pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Ruvuma amewaahidi
wakulima wa mazo hayo kuwa kauli ya serikali juu ya Suluhisho la
kupatikana kwa Soko la uhakika litatolewa katika kikao kitakachoketi
February 2 Mwaka huu Mjini Dodoma  na kuwahushisha Wakuu wa Mikoa
Mitano inayao lima Korosho nchini.

Akifafanua taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa kikao hicho
ambacho Mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Prof.
Jumanne Maghembe, Pia kitaweahusiha Maafisa Kilimo wa Mikoa na Wilaya
husika, wadau na viongozi wa vyama vya Ushirika katika Wilaya na Mikoa
hiyo.

Bw. Mwambungu aliitaja Mikoa itayaohusika katika Mkutano huo kuwa ni
Ruvuma, Mtwara, Lindi,Pwani na Morogoro  ambao alidai kuwa pamoja na
utekelezaji wa majukumu yao ya kawaida pia kwa pamoja wameapa
kutolifumbia macho suala la ubabaishaji wa soko la mazao hayo kutoka
kwa wakulima zikiwa ni juhudi za kuwarudishia ari wakulima baada ya
kuhakikishiwa upatikanaji wa soko la mazao yao ( source Steven  Augustino  Tunduru )