Saturday, November 12, 2011

MADAWA YA KULEVYA YAHARIBU MAISHA YA VIJANA WENGI KAMA UWAONAVYO VIJANA WA KILWA KIVINJE

mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE  KUSINI Bwana Juma Nyumayo  aliyesimama katikati anasuluali nyeusi alikuwa akiongea na vijana wanaotumia madawa ya kulevya Kilwa Kivinje,hao wao hupaita masikani,husemekana kuwa vijana hao hawaogopi serikali wala mtu yeyote.ukiwaushi wanakuchanja na nyembe.
Bw.Nyumayo anaangalia picha ya meli iliyochorwa kwenye kitambaa na vijana hao ambao hujiita wasela,washikaji wa Kilwa Kivinje Mkoa wa Lindi ambapo Blog hii ilikuwa huko kuona maendeleo ya wananchi wa mikoa ya Mtwarana Lindi katika miaka 50 ya UHURU wa Tanzania.ambapo mafaniko yapo,na changamoto zipo nyingi zikiwepo za ukosefu wa ajira kwa vijana hao ambao ni idadi kubwa nchini,kwa kukosa cha kufanya ndipo wanatumia madawa hayo.

Friday, November 11, 2011

PAMOJA NA MAENDELEO YALIYO PATIKANA KATIKA MKOA WA MTWARA BADO WANANCHI WA MKOA HUO WANA SHIDA YA MAJI

 Akina mama na watoto wanatoka majumbani kwao saa 11 usiku kutafuata maji lakini hadi saa 10 jioni hawajapata maji hayo ambayo katika wilaya ya Masasi mkoani mtwara plastiki moja la maji ya baridi au chumvi ni sh.100.
 Na watembeza maji plastiki moja ni sh.1000 kwa maji baridi na sh.500  maji chumvi
Hiyo ni foleni ya maji ambapo akinamama wameweka ndoo zao kuanzia saa 10 lakini hadi blog hii inatia nanga Masasi saa 11 jioni bado walikuwa hawajapata maji.

SAFARI YA MIKOA YA MTWARA NA LINDI KUONA MAENDELEO YALIOFANYIKA MIAKA 50 YA UHURU KUSINI MWA TANZANIA

i
Siku ya kwanza ya kukata tiketi ya kwenda Mtwara na Lindi katika stendi ya Songea
 Bwana Juma Nyumayo Mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI mwenye suluali ya bluu tulikuwa nae kukata tiketi kwenye basi litokalo Songea kwenda Masasi Mkoa wa Mtwara liitwalo New Obama.
 Ndani ya Basi hilo nilikaa jirani na Mzee Mohamedi Gwasa Afisa Elimu mtaafu ,alimpokea Bwana Nyumayo walipokuwa akiripoti akiwa mwalimu katika wilaya ya Tunduru mika ya nyuma.
 Mwl Mohamedi alistaafu kazi miaka ya themanini,huyo mwenye balaghashia alikuwa akienda masasi
Mwl.Mohamedi walipiga picha ya pamoja na kijana wake Bw. Nyumayo ya ukumbusho baada ya kuwasili Mtwara.

Wednesday, November 2, 2011

ELIMU YA WATU WAZIMA KATIKA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

 Mzee Evans  Leonard Kalonga Afisa eilimu ya Watu Wazima Mkoa mstaafu aliyetumikia taifa hili katika wadhifa huo hadi kustaafu anasema elimu ya watu wazima ilichangia kwa kiasi kikubwa kufuta ujinga kwa jamii ya watanzania baada ya uhuru.Mzee kalonga aliwahi kuwa Afisa elimu ya watu wazima Mkoa wa Rukwa na baadaye Mkoa wa Ruvuma hadi kustaafu kwake.

 Bwana Thomas Lipuka Komba yeye amestaafu akiwa Afisa Elimu Vielelezo Wilaya za Lindi na baadaye Songea vjijini yeye alikuwa Afisa Habari katika Idara ya elimu akiwa Ripota wa magazeti ya TUJIFUZNE KUSINI hadi anastaafu.
 Maafisa hao ni hazina tosha ya elimu ya watu wazima ilivyo anza kushamili hadi kupoteza umaarufu wake.
Hapa wakiaandaa MAKALA ya elimu hiyo kwa ajili ya Toleo Maalumu la TUJIFUNZE KUSINI ndani ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hii.

NGOMA ZETU LEO NAWALETEA NGOMA YA KUSINI LIZOMBE AMA KWA JINA LINGINE KITOTO


 kikundi cha Lizombe cha Jakaya Mrisho Kikwete cha Lizaboni Manispaa ya Songea kilicho tumbuiza siku ya wiki la elimu ya watu wazima kiwilaya limefanyika Kata ya Majengo

 Bwana Rabii Mzee mwanakisomo wa Majengo akisoma risala siku ya juma la elimu ya watu wa zima Manispaa ya Songea hivi karibuni
 Waandishi wa habari akisikiliza kwa makini ujumbe unaosomwa na Bwana Rabii Mzee kutoka kwenye risala hiyo.
Baadhi ya walimu waliofika kuhudhuria wiki hilo wakiwa kama watazamaji wasiojua nini kinaendelea kuhusu elimu ya watu wazima.

WANANCHI WAKISHIRIKI KWENYE KISOMO WATALETA UKOMBOZI KATIKA USAFI WA MANISPAA YA SONGEA – MEYA

 Mstahiki Meya Charles Mhagama  akikagua kazi za wanavikundi
 Akikagua moduli za masomo kutoka Taasisi ya elimu ya watu wazima Kituo cha Songea
 Mheshimwa Mhagama wa kwanza mwenye makaratasi  akisikiliza shauri
 Kazi za mikono za wnakikundi cha Majengo
 Asha Tembo na Annamary Komba wakisoma shairi wanakisomo wa kujiendeleza kutoka majengo
Afisa eilu ya watu wazima Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Yonas akisoma taarifa ya elimu ya watu wazima ya manispaa ya Songea.

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Songea Mhe. Charles Mhagama  amesema kuwa wananchi wa Manispaa ya Songea wakishiriki kikamilifu kwenye vikundi vya kisomo vya MUKEJA  na VICOBA watakuwa ukombozi wa mabadiliko ya usafi katika Manispaa yake.
Mheshimiwa Mhagama alisema hayo kwenye hotuba yake ya wiki la elimu ya watu wazima kiwilaya iliyomwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Iddi Abdalah Diwani wa majengo, baada ya kukagua maonyesho kadhaa yaliyo wekwa na vikundi mbalimbali ya kisomo na uzalishaji mali katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Manispaa ya Songea.

Sherehe huzo ziliandamana na Risala,Ngojera,michezo ya kuigiza na ngoma ya Lizombe ya kikundi cha Jakaya Mrisho Kikwete cha Lizaboni kinachoongozwa na Mzee kajogolo.



Thursday, October 27, 2011

BREAKING NEWS ! ! ! GARI LILILOKUWA LIKIPELEKA MITIHANI DAR ES SALAAM KUTOKA RUVUMA SONGEA LA PATA AJALI

Habari zilizopatikana kutokana baadhi ya watu waliyokuwepo kwenye Lori hilo inasema kuwa askari wawili majana yao hayakupatikana mara moja wameumia,na baadhi yao ni wazima.Habari zaidi utazipata kwenye vyombo vya habari.