Saturday, July 9, 2011

JUMA MOSI YA LEO NA HARAKATI ZA WANANCHI WA SONGEA MANISPAA

 Mji wa Songea Mkoani Ruvuma kama unavyo onekana katika picha Jumamosi ya leo na harakati za kujenga taifa kila mmoja kwa stahili yake mradi anahudumia familia yake.
 Manispaa ya Songea leo
Ilikuwa ni mida ya mchana ambapo Blog hii ilipoipata picha ya Manispaa hii ya Songea wakati Manispaa hiyo imaeamua kufukuza akina mama ntilie waliekuwa wakiuza chai na vyakula katika Stendi kuu ya Manispaa ya songea na kuiacha stendi na abiria na magari.

Friday, July 8, 2011

kuharibika kwa Teller za kuchukulia fedha nje ya benki ya NMB tawi la Songea kwa sababisha msongamano benki

Kuharibika kwa visanduku vya kutolea fedha Tellers  katika tawi la NMB mjini Songea kumesababisha msongamano wa wateja  kujazana ndani ya benki hiyo leo kuchukua na kuweka fedha.
Blog hii leo imeshuhudia jinsi watu wanavyo laumu huduma mbovu katika benki hiyo.Wanajiuliza kama ma-teller hayo yameharibika kwanini wasingetengeneza na huduma ikaendelea kama juzi,Hivyo hawaoni karaha kuona umati wa watu ulivyo jazana ndani ya benki kwa muda mrefu.
Pamoja na NMB inawateja wengi lakini pia waliyopewa dhamana ya kuhudumia watu hawako makoni katika utendaji wao wa kazi.
Lakini kingine kinachochangia kwa hapa Songea ni kuwa na teller katika jengo la benki hiyo tu,badala ya kuweka katika vituo vya mafuta kama walivyofanya NBC tawi la Songea.

Wednesday, July 6, 2011

KERO KUBWA LA MLUNDIKANO WA TAKA KATIKA SOKO KUU LA MANISPAA YA SONGEA ULIYOSHUHUDIWA NA BLOG HII LEO

Huo ni mrundikano wa taka katika soko kuu la Manispaa ya Halmasuri ya Songea ambao unasababisha haruru mbaya kwa wafanya biashara katika soko hilo,pia kwa wanunuzi wanaopita katibu na juba lililosheheni taka bila kuzolewa ndani ya soko hilo.

Barabara nyembamba katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea unasababisha foleni ya magari na pikipiki masipo sababu.

 Huo ndiyo msongamano au Foleni ya magari unaosababishwa na barabara nyembamba katika halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Ni eneo la Manzese Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma barabara itokayo Mji Mwema kuelekea Mjini Songea.

BREAKING NEWS SUDAN KUSIN KUWA JAMHURI MPYA JULAI 9 2011

 Sudan ofisi za serikali
 Raman ya Sudan na Picha ya Rais wa nchi hiyo Omar al - bashir na Ramani Sudan Kusini
 Mji wa Sudan Kusini ulivyo chukuliwa kwa juu
Sudan kusini inakabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo, uhaba wa maji wanachi wananunua maji yanayopelekwa kwenye matanki,umeme siyo wa uhakika,huduma ya afya si wa kuridhisha.
 Mji wa Juba nchini Sudan Kusini

Daraja katika mto Nile na Noel Mwakalindile TBC alivyo tembelea Mji wa Juba nchini Sudan hivi karibuni katika mchakato wa upigaji wa kura za maoni na kuhoji wananchi kuhusu kujitenga na Sudan ya Bashir.

Ambapo asilimia 98 ya wananchi wamechagua kujitenga ,Takribani wananchi milioni 4 sehemu mbalimbali nchini humo katika nchi 8 za nje.na askari 60 elfu walihusika na ulinzi na usalama katika uchaguzi huo,ambapo waangalizi  zaidi ya 10 elfu wan chi hiyo na wakimataifa 1,500 walikuwa waangalizi wa upigaji kura za maoni nchini humo.
Sudan  Kusini itakuwa Jamhuri mpya tarehe 9 Julai 2011 na hatimaye kujiunga na Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki. ( Source Urary 95 )

Saturday, July 2, 2011

LORI LA JERUHI 3 WAPELKWA HOSPITALI YA MKOA SONGEA BAADA YA KUTUMBUKIA DARAJANI MATARAWE LEO

 Watu watatu  ( 3 ) wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Songea leo asubuhi  baada ya lori walilo kuwa wakipeleka maturubai  SAMCO kutoka Ruhuwiko kwenye ghala la kuhifadhia chakula mkoa wa Ruvuma baada ya lori hilo kutumbukia kwenye daraja la Matarawe Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Watu kadhaa waliyo shuhudia ajali hiyo wamasema kuwa lori hilo lilikuwa limejaza maturubai,likiwa na matindo 32,hivyo lilivyovuka daraja na kupandisha mlima, lori hilo lilimshinda dereva na kurudi kisha kutumbukia darajani,kuona hivyo wote waliruka.ndipo watatu kati yao waliruka vibaya na kupata majeraha wote walikimbizwa hosipitali.
 Baadhi ya matingo waliyosalimika katika ajali hiyo wakiyavuta maturubai yaliyo mwagikia darajani,na mengine kutupwa ng'ambo ya daraja hilo dogo la Manispaa ya Songea lililoko Matarawe,ili kupakia kwenye lori lingine lililopelekwa katika tukio hilo.

Friday, July 1, 2011

Waliyofanya vizuri katika masomo ya sayansi kidato cha sita watunukiwa vyeti na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni Dodoma leo

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda amkabidhi cheti mwanafunzi Francis John aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi Bungeni Dodoma leo.
Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe akimpongeza mwanafunzi Agapi Chacha aliyefanya maajabu katika masomo ya sayansi mtihani wa Taifa mwaka 2011 ndani ya Bunge leo mjini Dodoma masaa machache yaliyo pita.
 Mhe.Waziri mkuu akiwapongeza wanafunzi 20 kati yao wanafunzi 7 wanatoka katika sekondari za kata nchini
Mhe.Prf.Shukuru Kawambwa akitoa taarifa kwa Waheshimiwa wabunge kuwa wanafunzi na walimu wanafundisha katika shule ambazo wanafunzi hutokea kufanya vizuri zaidi ya wengine katika masomo ya sayansi ambayo wengi wao huyaona na magumu lazima watapongezwa na kupewa zawadi.



WAZIRI mkuu  Mizengo Pinda amewazawadia wanafunzi 20 Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2011.

Wanafunzi hao 10 ni wavulana na 10 ni wasichana  waliyopewa vyeti baada ya kufanya maajabu katika masomo ya sayansi,zaidi ya hapo kati ya wanafunzi hao 20 kati yao wanafunzi 7 wametoka katika sekondari za kata ambazo wengi wanazidharau na kusema hazina maana.

Alisema serilikali inaona mbali katika kuanzisha Programu za kuboresha elimu nchini kama ilivyo katika MMEM na baadaye MMES ambayo ndiyo matunda ya shule za sekondari za kata nchini na matokeo yake yanaanza kuonekana kutokea wanafunzi waliyofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi kama wale wa shule za serikali kongwe.

Aidha Mhe.Pinda amewaasa wanafunzi hao kuwa waepukane na migomo isiyo na tija wakati wa kuendelea na masomo ya elimu ya juu,alisema kuwa wasifuate makundi ambayo kwa namna moja au nyingine wanawaingiza hata wanafunzi ambao hawapo katika matarajio ya kufanya maadamano.

Amezitaja sekondari zilizotoa wanafunzi hao waliofanya vizuri wa kidato cha 6  kuwa ni pamoja na :-Kibaha,Mzumbe,D’salaam,Tabora Boys,Tabora Girls,Benjamini William Mkapa,Tanga,Kiloka,Arusha,Kilimanjaro , Mbeya na Kilakala Morogoro.