Dereva huyo wa kampuni ya Saibaba yatokayo Dar es salaam kwenda Arusha ,aliye kataa kutaja jina lake alipokuwa akihojiwa na Polisi Kibaha alisema yeye alikuwa hajalewa ila alikunywa kiroba kimoja tu.Aliendelea kukataa na kuwatishia wasafiri wake wachukue swichi waendeshe wao.
Wasafiri wali mgundua alipoanza safari Terminal Dar es salaam,mwendo kasi alivyo fika Kibaha alitaka avamie nguzo ya umeme.Hongera wasafiri kama nyie na wengine wafuate nyayo za wasafiri wa Arusha.kukeme amadereva walevi anapo wagundua.
Makamu wa Rais Dkt Bilali apewa maelezo kuwa mabomu yameteketeza maghala 4 yaliyo hifadhi nguo na vitu kadhaa,aidha maghala ya silaha 23 lakini maghala 22 ndiyo yaliyo lipuka na kuleta madhara makubwa.
Hali ilikuwa hivyo askari huyo akiwa na baadhi ya silaha hizo ambazo zilileta balaa usiku wa jana.
Rais Jakaya Kikwete apata maelezo juu ya majeruhi wa mlipuko wa mabomu Gongo la Mbopto kutoka kwa mganga wa hospitali ya Amana.Aidha Rais amewataka wananchi walio kimbia makazi yao warudi kwenye makazi yao kwani Serikali imedhibiti hali hiyo.na hali ni salama.
Huyo ni mama aliyejeruhiwa na bomu ambalo lili mkata mkono wakati akikimbia milipuko ilipozagaa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bibi Blandina Nyoni akitoa maelezo kwa waandish wa habari hapo Amana alipo kwenda kuoana hali halisi ya huduma katika Hospitali hiyo.
Kufuatia mlipuko ya mabomu leo usiku Gongo la Mboto Dar es salaam watu 20 wamepoteza maisha na 184 majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali za Amana. Temeke,kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi ASP Advera Sensor alisema hali ni shuali wananchi watulie hali haiwezi kurudia tena ,alisema wasisikie uvumi wa watu ambao hauna ukweli.Ametahadharisha iwapo mtu ataona kitu ambacho si cha waida watoe taarifa polisi.
Alitaja Mawasiliano ni Namba za simu za,0783-260334 au 0774- 039020 au 0755 -756410.maana kuna uwezekano wa baadhi ya mabaki ya mabomu hayo hivyo wawe waangalifu.
Mmoja wa wafanya kazi wa Red Cross akimpeleka majeruhi kupata huduma ya kwanza katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam ambako wamewahifadhi wahanga hao.
Huyu ni mfadhili mmoja kutoka kiwanda kimoja wapo cha magodoro amefika kiwanjanai hapo kutoa msaada wa magoro 300 yanye thamani ya shilingi 10,000,000/=.
Huyo ni Mtoa huduma wa RedCross toka jana usiku yuko kiwanjani hapo akitoa msaada wa chakula na matibabu kwa wahanga,alisema watoto 179 wamepotelewa na wazazi wao.
Wahanga wa mlipuko wa mabomu Gongo la Mboto wapo Uwanja wa Uhuru hawajui nini cha kufanya kufuatia hali ilivyo wakuta usiku huo wa balaa.
Hawa ni baadhi ya waumini wa dini za kihindu wametumwa na mkubwa wao huko India kuja kutoa huduma za kibinadamu kwa wahanga hao.
Hawa ni wahanga wako kwenye viti vya uwanja huo sio wanatazama mpira bali ni machungu tu yamewakuta kufikishwa hapo walipo.Jumuiya ya TUJIFUNZE KUSINI inato pole kwa wote waliopoteza ndugu zao,waliopata majeruhi kadhaa Mungu awape unafuu mapema warejee kujenga taifa letu.
Masultani na Machifu bado wapo katika wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ,hapo ni kundi la masultani wakiwa katika Taasisi ya KIUMA inayo endeshwa na Daktari Matomora.aliye amua kuanzisha Taasisi hiyo kwa lengo la kuondoa ujinga wilayani humo.
Sultani Mpelembe ni Myao wa Malambo - baba yake wa kwanza aliitwa Chuma - Chekulungu ( maana yake ni chuma kikubwa).Kupitia masultani hawa hapo zamani biashara ya watumwa ilishamiri sana uyaoni,ikiwa ni pamoja na pembe za ndovu kwa kufanya misafara mirefu kati yao na Kilwa Karne ya 19.Livingstone alishuhudia wayao wakiteka watumwa nchini malawi katika mto Shire mwaka 1859.
Alipitia machifu kadhaa walioshughulika na biashara hiyo,na kujenga utawala wa kichifu karne ya 19 lakini haukudumu.Bishara hiyo ilidumu kwakuwa walikuwa na ushirika na watu wa pwani ,Kilwa na Afrika ya Kati.
Kijiji cha Wayao na jinsi wanavyo karimu wageni wakiwatembelea nyumbani kwao,ngoma ,vyakula vitaandaliwa,utamaduni wa kiyao ni wa Kibantu kwa ukarimu,Ila biashara ya kuuza binadamu na kufuata mila na desturi za kiarabu na ufuasi wa kiisalamu ndipo kulikorudisha nyuma maendeleo ya elimu Wilayani humo.
Watoto wilayani Tunduru,wameathirika kwa kiasi kikubwa katika elimu inayochangiwa na wazazi wao ambao wanaona elimu sio kitu cha kuwasaidia katika maisha,utoro,mimba,biashara ndogondogo ndizo zilizotawala miongoni mwa watoto hawa.
Huu ni kati ya misikiti mikongwe Duniani kati ya 695 - 705 BK Msikiti wa Umawiya Mjini dameski katika Syria.
Blogu ya TUJIFUNZE Kusini inawataki heri na fanaka kwa kusherehekea Mulidi Duniani kote,tunaungana nao katika kuomba, maana Sala ya Maulidi imesaliwa katika maeneo mbalimbali duniani kwa lengo la kumuomba Allah aishushie amani,upendo na mshikamano kwenye nchi ambazo amani imepotea. Amani na mshikamano ni muhimu kwa madhehebu yote Duniani,hasa katika nchi yetu ya Tanzania.
Sehemu ya jengo ambalo lilikuwa na ukumbi mkubwa wa kunadi bidhaa zikiwemo watumwa,pembe za ndovu,simbi,mbao na vyombo vya kufinyangwa kutoka bara la Arabu na Ghuba ya uajemi,kisha kuingiza kwenye ngarawa tayari kwa kusafirisha.
Hicho ni kiberenge kilitumiwa na mmoja wa mwanaakolojia ambaye akikuwa akichimba ili aone masalia ya vyombo vilivyo kuwa zikitumika wakati huo na washirazi kisiwani hao wakati huo.aliyeshika kiberenge ni Bw.samweli mtembeza wattalii.
Hapo si kiwanja ila ni ukumbi amabo mnada ulikuwa ukifanyika,au sherehe zao watawala hao wa kiarabu walikuwa wakifanyia humo,kwa mbele kuna maji ni bahari ambapo kuna ngazi za kuteremshia bidhaa kuingiza kwenye ngarawa zao.fika ukajionee ni utalii nafuu zana wa kuona kisiwa cha kihistoria Tanzania.
Pwani ya kusini mwa Tanzania Mafia na kilwa ilikuwa ni miji
ya biashara katika karne ya kumi na moja,pia biashara ilishamiri Mogadisho
nchini Somalia.Ngarawa zilipeleka pembe za ndovu,dhahabu kutoka
Msumbiji,watumwa na bidhaa kadhaa kutoka pande nyingine za pwani kwa ajili ya
kuwauzia warabu wakati wa msimu wa biashara.
Aidha Kilwa kutokana na wanaisimu wanasema historia ya Kiswahili
imeanzia miji ya pwani ya Afrika Mashariki,na Kilwa ni mmoja wapo.warabu
waliingia kiujanja ujanja kufundisha dini ya kiislamu ambapo shehe wa kwanza alikuwa
mshirazi Muhammad mtoto wa Ali bin Hasan.
Alikuwa mwanzilishi wa utawala wa Kilwa na kukutwa na
Wareno,na ndiye aliyekuwa wa kwanza katika mlolongo wa Waarabu kutoka Bara la
Arabu na Ghuba ya Uajemi.Ili kujua tamaduni na asili ya waswahili katika pwani
hizo wanaakolojia wanachambua kwa makini ambapo wanaantropojia nao walifanya
tafiti zao za kuchunguza mabaki katika miji na vijiji katika Pwani hiyo.
Mapema katika milenia ya kwanza kabla ya Kristo ngarawa
zilikuwa zikisafiri kutoka Bara la Arabu na Ghuba ya Uajemi zikipeperushwa na
pepo za kaskazi,kuleta vyombo vilivyofinyangwa,nguo na vyombo vya chuma vilivyo
badilishwa na pembe za ndovu,watumwa,mbao,simbi na rangi na kurudi kwao na pepo
za kusi.
Kwa wale wanaochukua shahada ya kwanza ya Kiswahili ningewashauri
wafanye ziara kwenda maeneo yenye chimbuko la historia ya Kiswahili waone eneo
warabu walopokuwa wakipakizia bidhaa zao kwenye majahazi wakiwemo binadamu
maarufu watumwa kupelekwa bara Arabu na Ghuba ya Uajemi.
Ukifika utapata kuelewa mamwinyi na umarufu wao,kuliko
kusoma tu kwenye vitabu,ustarabu na utamaduni wa kiafrka wa pwani hiyo na
washirzi noa kuwepo kwa lugha ya Kiswahili,pia kuondoa dhana potofu ya kuwa
asili ya Kiswahili ni kiarabu au kibantu kwa kuangalia lahaja zilizokuwa
zikitumika pwani na wenzao wa bara.
Na kuyaona magofu yaliyojengwa kwa mawe matumbawe,yanye
asili ya majengo ya kishirazi.yalikuwa majengo imara hadi leo ushahidi
unaonekana,lakini kustawi kwa Kilwa Kisiwani kutakuwepo iwapo atapatikana
mwekezaji wa kujenga hotel ya kitalii kwenye kisiwa hicho cha
kihistoria,kilicho nunuliwa kwa kipande cha nguo kukizunguuka.