Tuesday, November 30, 2010

IKIWA LEO NI MAADHIMISHO YA UKIMWI DUNIANI LAKINI UKIMWI BADO NI TATIZO KATIKA JAMII ZETU,KILA MMOJA WETU ACHUKUE TAHADHARI - MNJAGILA

Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmii Bwana Salum Mnjagila akitia saini kitabu cha wageni katika ofisi ya Afisa Elimu Wa Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma mwaka huu wakati wa ziara ya kukagua vituo vya MUKEJA na VICOBA  Simanjiro,Njombe,Songea,Na Mahenge.( picha na Christian Sikapundwa )

Bwana Mnjagila pamoja na kukagua maendeleo ya vituo hivyo lakini hakusita kutoa tahadhari yuu ya VVU na UKIMWI katika jamii za watanzania.Alisema wanapojifunza jinsi ya kuzalisha mali katika ufugaji,ususi biashara ndogondogo na uwekaji wa akiba benki ,lakini pia wajifunze namna ya kuacha mambo yanayochangia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa kuwa na mpenzi mmoja,kauacha mambo hayo au kutumia kinga.Hata kusikiliza ushauri wa wataalamu wa afya na ushauri wa viongozi wa Dini.

wakati leo ni maadhimisho ya UKIMWI Duniani Ruvuma wapo chini ya 33% ya upimaji wa hiyari


KAIMU Mratibu wa UKIMWI Mkoani Ruvuma Dkt Luitrid Komba asema changa moto bado ni kubwa kwa watu kujitokeza kupima afya zao kwa hiyari mkoani Ruvuma.Atoa wito kuwa watu wakapime afya zao,dawa za kurefusha maisha zinapatikana katika vituo vinavyo husika.

Wakati leo ni siku ya maazimisho ya UKIMWI Duniani mkoa wa Ruvuma ina asilimia 6.3 kutokana na taarifa ya watu waliojitokeza kupima afya zao Januari hadi Septemba mwaka huu.

Kaimu Mratibu wa UKIMWI mkoa wa Ruvuma Dkt.Luitfrid Komba alitoa taarifa hizo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa RCC kilichofanyika Songea Club Novemba mwaka huu.

Dkt Komba alisema upimaji wa hiyari UKIMWI ni asilimia chini ya asilimia 33 kimkoa na kiwango cha watoto walioambukizwa ni asilimia 4.6.Aidha vituo 90 vinatoa huduma ya mama na mtoto ya kinga ya maambukizi ya UKIMWI.
 

Monday, November 29, 2010

Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya akemea vitendeo vya Wizi wa Ruzuku za Pembejeo

'Sikubali wala sinataruhusu Ruzuku za pembejeo zilizotolewa na serikali kuliwa na wajanja wachache wenye lengo la kuchukua vocha za mbolea na mbegu wakati mashamba hawana ili wakauze wapate fedha,sintavumilia kwa vitendo vya kuhujumu fedha za serikali.' Alisisitiza mkuu wa wilaya huyo kwenye kikao cha  maendeleo cha mkoa ( RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Songea club.




Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya ambaye ni mwenye kiti wa Pembejeo za Ruzuku wilaya  ya Songea,ndiye aliyeanzisha utaratibu wa barua za utambulisho wa shamba kwa wakazi wa mjini ili kulinda fedha za Serikali zisiliwe na wajanja wachache ambao hujifanya wana mashamba kumbe wanalengo la kuiba fedha za serikali kupitia Ruzuku za pembejeo,kitendo ambacho kinamkera Mkuu wa wilaya hiyo.

Aidha Bw.Sabaya amekemea kwa nguvu zote vitendo vivyosadikiwa vinafanywa na baadhi ya Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa vijijini na Vitongoji kutoza fedha kati  ya shilingi 1,000/= hadi 5,000/= ili kuwapitishia barua hizo kuwa ni kero na ni dalili za rushwa na wakibainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu,(Source Juma Nyumayo)

PONGEZI

Mwenye kiti wa Ruvuma Press Bwana Juma Nyumayo kulia aliyevaa vuti akiwa na Makamu wake wa Press hiyo Bwana Mhidini Ndolanga aliyevaatai na Mjumbe wa Press hiyo Bi.Editha Karlo  wa katikati akiwa akipata chai siku ya kikao cha kamati ya Maendeleo ya mkoa wa Ruvuma hivi karibuni Songea Club ( Picha Na Christian Sikapundwa )


Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma (RPC) kinawapongeza viongozi waliochaguliwa  wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro ( MECK ) kwa kuaminika na wanachama wao na kuwapa ofisi yao ambayo ni mdau mkubwa wa maendeleo.

Mwenyekiti wa Ruvuma press club Bwana Juma Nyumayo,amesema kamati ya muda chini ya uongozi wa mwenyekiti Josephine Sanga,ilifanya kazi nzuri na kuweka misingi imara kufikia uchaguzi wa Kidemokrasia uliowachagua viongozi wapya.

Hongera sana endeleeni kushirikiana kwa maendeleo ya Kilimanjaro,Kanda ya Kaskazini na Taifa zima kwa ujumla ( Source Juma Nyumayo ).

HICHO NDICHO KILICHO PIGIWA KELELE NA WAJUMBE WA BOARD YA BARABARA MKOANI RUVUMA KWA MKUU WA MKOA DKT CHRISTINE ISHENGOMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt  Ishengoma allisema fedha za serikali za ujenzi wa barabara zitumike kwa kujenga barabara zenye viwango vilivyo bora katika kikao cha bodi ya barabara kilicho fanyika katika ukumbi wa Songea Club,Alikuwa sahihi.Je hiyo barabara ya kiwango cha lami katikati mji wa Manispaa ya Songea itokayo CCM Wilaya kuelekea kanisa la Anglikana ilijengwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa ? .( picha na Christian Sikapundwa )

FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA ZITUMIKE KWA UJENZI ULIO BORA WA BARABARA ZETU - DKT ISHENGOMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt Christine Ishengoma katika kikao cha Board ya barabara Songea Club tarehe 26/11/2010

MKUU wa mkoa wa Ruvuma  Dkt Christine Ishengoma amekemea tabia ya baadhi ya Halmashauri mkoani hapa kutumia fedha za ujenzi wa barabara visivyo hasa kujenga vipande virefu bila ubora. ‘Afadhali mjenge barabara km  moja ( 1 ) yenye ubora kuliko km 4 kwa fedha hiyo bila ubora.’Alishauri Dkt Ishengoma.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara mkoani Ruvuma kilichoketi tarehe 26/11/2010 Songea Club walipeleka masikitiko yao makubwa kwa halmashauri ya Manispaa  ya Songea. Kwa ujenzi wa barabara na matengenezo bila viwango.

Hata  hivyo waliipongeza,Halmashauri ya Mbinga katika ujenzi wa barabara za kiwango cha lami pia wakala wa Barabara mkoani TANROADs kusimamia vyema mitandao na kujenga barabara na madaraja.( Source Juma Nyumayo )

Sunday, November 28, 2010

Siku 16 za kupinga ukatili za kijinsia Tanzania,wanaharakati,jamii isilifumie macho jambo hilo

Siku 16 za maandalizi ya kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwa watanzani,unafanyika kikanda kama ilivyo ainishwa na wanaharakati wa kupinga unyanyasaji wa kijinsia katika jamii zetu za kitanzania.Hasa kufuatia mila na desturi za kiafrika kuwa na mfumo dume,mfumo boss,na hata mfumo jike.Dkt Judith Tudunga alisema kupitia vyombo vya habari kuwa ukatili wa kijinsia umetawala sana katika jamii zetu.

Wito wake kwa watanzania kuwa wakisikia jirani anapigwa ama kufanyiwa vitendo ambavyo vinamdharirisha wajitokeze kwenda kutoa msaada.Alisema unyanyasaji na ukatili wanaofanyiwa baadhi ya tanzania unasaidia kurudisha nyuma maendeleo ya ,mtu binafsi na hata Taifa zima kwa ujumla.