Dokta Emanuel Nchimbi atetea kiti chake cha Ubunge katika jimbo lake la Songea Mjini baada ya kumshinda mpinzani wake Advocate Mbogolo wa CHADEMA aliyewania nafasi hiyo kwa mara nne sasa na kuambulia patupu,asikate tamaa ipo siku ndoto yake itakamilika ya kuingia Jengo la Bunge la Jamhuri ya Tanzania ( Picha na Christian Sikapundwa)
Friday, November 5, 2010
Thursday, November 4, 2010
LEONI LEO KIKWETE,LIPUMBA AU SLAA !! KUKAMILISHA NDOTO YA KUINGIA IKULU BAADAYE LEO IJUMAA YA TAREHE 5 NOVEMBA 2010 KUWA RAIS WA TANZANIA KWA MIAKA MITANO IJAYO
Pamoja na kumaliza hekaheka za kampeni za Urais Ubunge na Udiwani ikaingia ngwe nyingine ya upigaji wa kura tarehe 31.10.31 2010 ulikamilika kwa Amani na Utulivu mkubwa,wananchi walitimiza haki yao ya msingi kumchagua kiongozi wanaye mtaka.
Ikaingia hatua ya mwisho ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo,ambapo vyama vyilivyo ng'ara kwenye majimbo mengi katika nafasi za Ubunge na Udiwani vimeibuka kuwa washindi ,na matokeo ya nafasi ya Urais yameendelea kutangazwa na leo ndiyo atangazwa mshindi kwa nafasi ya Urais kulingana na uwingi wa majimbo aliyopata ushindi na kujumuisha matoke.Na kuibuka kidedea leo.
Vyama vilivyoingia katika kinyang'anyiro vilivyo shindwa vikubali matokeo,kukataa matokeo bila kufanya utafiti wa kutosha kwa wapiga kura wako,ni kushangaza watu.kushinda au kushindwa ni katokeo ya idadi ya wapiga kura waliyo kukubali au kukukataa.Na si rahisi kung'amua ni nani aliye nikubali au kukukataa kwa kuwa ilikuwa ni siri ya mpiga kura kwenye visanduku.
Lakini pia kushinda au kushndwa kusichukulie uwingi wa watu waliyojitokeza siku mgombea alipokwenda kunadi sera za chama chake,watu wanaweza wakawa wengi lakini siku ya kupiga kura wasiwe wengi au wakawa wengi lakini hawa kuwa na shahada ama walikuwa na shahada hawa kwenda kupiga kura yote yanawezekana kwa Binadamu.
Aidha cha msingi Tume ya Uchaguzi irekebishe utaratibu wa kuchelewesha kutangaza matokeo,ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo kuna sababisha maswali mengi kwa wapiga kura wenyewe,wanacha wa vyama mbalimbali na wagombea wenyewe,kwanini yanacheleweshwa.Matokeo yakitangazwa mapema yatapunguza malalamiko ya wapigiwa kura ya kuchakachuliwa kura zake.
Thursday, October 28, 2010
IKIWA ZIMEBAKI SIKU MBILI WATAZANIA WAINGIE KWENYE UCHAGUZI MKUU KIKWETE AJA NA CCM NI CHAMA KUBWA KUBWA LA MBEGU NDICHO KIME ZAA CHADEMA,NCCR,CUF,TLP NA VYAMA VYOTE VYA UPINZANI NI NINI KAMA CCM
Zikiwa zimebakia siku mbili kuelekea kwenye uchaguzi mkuu tarehe 31 /10/2010,mgombea Urais kupitia CCM Dkt Jakaya kikwete aseama CCM ni Chama Kubwa tena dume la mbegu iliyozaa,akina CHADEMA,NCCR,TLP CUF navingine ambavyo havijulikani sawasawa.( Source Christian Sikapundwa)
Dar es salaam awambia tatizo la maji litakuwa ndoto kwao wakazi wa jiji hilo,kama Ilani ya CCM inavyoeleza.Mikoa ya Lindi waambiwa kuwa ruzuku ya dawa za korosho itaongezwa,na kuimarisha soko la uhakika lenye tija kwa mkulima wa zao hilo.
Saturday, October 23, 2010
THE MAJI MAJI NATURAL HISTORICAL OF NGONI MUSEUM AT SONGEA MUNICIPALITY
HISTORICALLY the Ngoni people were situated as the Bantu speakers had settled in Southern Africa in groups such as Sotho –Tswana the Ngoni Shone and the Tsonga Ngoni who became dominant and also the Xhosa were the one of the branch of Ngoni.
Due to the historical background shows that the Ngoni people were escaped the ruling power of Shaka Zulu,when the Mzilikazi in 1823 decided to run away Northwards to the Shonaland and modern Zimbabwe . Because Shaka was an autocrat person.
Shaka became a supreme autocrat controlling everything in Zululand . he made himself as spiritual and judicial leader, had no children for fear they would turn against him when they grew up, therefore he was a killer he slaughtered thousand of people when his mother died.
Politically the Ngoni people were organized into numerous but small hereditary chiefdoms, in average Ngoni chiefdom consisted of four to five villages with the chief called the Nkosi. But among the ngoni were chosen from the royal clan, the heir to the throne son was in principle the eldest son of the senior wife of the chief.
The ngoni chiefdoms were temporal and spiritual leaders, they were responsible for administration of the chiefdoms and for the dispensation of justice, they presided over social and religious ceremonies.
In other hand the chief did not enjoy his power, because the chief’s power were checked by his own privy council, is also his power was also often challenged by his brothers or even his sons therefore the chief had to attract and retain supporters in order to maintain their power.
Economically the ngoni people were subsistence economies which encompassed the cultivation of crops, animal husbandry ,crafts, mining ,metallurgy and barter trade which the structure and composition of these economies varied from community to community and were conditioned by environmental factors. such as distribution of water and rainfall, soil fertility and natural resource endowment.
Finally we welcomed you to the Majimaji National Historical museum of Songea the place Chiefs were buried among of them were Nkonsi Gama, Songea Mbano,Chandamali,and also the Memorial of majimaji war of July 1905 to August 1907 which started at Nandele village Kilwa District Lindi Region.
When you face majimaji National museum Songea Municipality
This is the attractive place of majimaji National Museum of Songea Municipality,where you can enjoy your self by observing traditional historical things of the Ngoni people and the place were chiefs buried,Welcome Songea,Welcome Majimaji Museum. ( Photo by Christian Sikapundwa )
Thursday, October 21, 2010
MBIO ZA ELIMU YA SEKONDARI KWA KIDATO CHA KWANZA ZINAISHIA KIDATO CHA NNE UKIKIMBIA VIZURI UTASHINDA NA VIBAYA UTASHINDWA BWANA EMANUEL C.SIKAPUNDWA NI MIONGONI MWA WALIOANZA MBIO HIZO.
Emanuel C.Sikapundwa mwenye miwani ni mwanafunzi wa Msamala Muslim Seminari Songea amehitimu elimu ya sekondari kidato cha nne (IV ) mwaka huu,baada ya kutunukiwa cheti cha kumaliza elimu hiyo,Dada na ndugu zake walimkabidhi zawadi mbalimbali kama ishara ya upendo na hungera kwa huhimili mikikimikiki ndini ya maisha ya shule kwa miaka yote akiwa shuleni.
Lakini kabla ya sherehe hizo kuanza huko shuleni kwao,Nyumbani kwa Emanuel Ndani ya uwanja wa Sabasaba Matarawe Manispaa ya Songea wameonekana akina mama wakiamwandalia chakula yeye na wapambe wake,ndugu na jirani,Sherehe ni kula (.Source Christian Sikapundwa )
Akina mama hao walianadaa wali mweupe na mwingine Pilau,unajua wasahili husema mchele ni mmoja lakini mapishi mbalimbali.watu wa pwani wana ujua zaidi mchele na aina mbalimbali za mapishi yake,mimi si mwanataaluma wa mapishi hayo.Na kwenye miti hakuna wajenzi,inamaana kule wanako ulima mpunga inawezekana hakuna mbwembwe nyingi za kuupika mchele huo.Je wewe wasemaje ? fuatilia ...............
Wednesday, October 20, 2010
VIJANA BAADA YA KUGUNDUA KUWA AJIRA IMEKUWA NI MAZUNGUMZO MAJUKWAANI KARIBU NCHI NYINGI DUNIANI,KUNA BAADHI YA VIJANA WAGUNDUA AJIRA YA CHAPCHAP HUKO NCHINI KENYE AJIRA GANI HIYO ENDELEA NA ‘FILER’ HAPO CHINI
BAADHI ya vijana nchini Kenya wamebuni ajira ya harakaharaka baada ya kuona ajira imekuwa wimbo wa majukwaani hasa kipindi cha chaguzi mbalimbali za uongozi duniani.
Kwa taarifa ya Wanyama Kibusire wa Kenya zinasema amekutana na vijana hao wakiwa katika ajira hiyo ambayo wanasema inawapa Dollar 7 za Kimarekani baada ya kumaliza kazi ambayo wamepangiwa na mwajiri wao,Siku hiyo hiyo.
Alisema vijana hao na wananchi wa Kenya wamoena njia rahisi ya kuemboleza msiba ndugu yao akifariki na kuajiri vijana kufika kuwalilia kuanzia chumba cha maiti,hadi nyumbani kwa mfiwa,walilia vijana hao wa ufundi mkubwa wakati wengine wakiomboleza kwa nyimbo za sala kama watakuwapo.
Ingawa baadhi ya madhehebu ya dini yamekipinga sana kitendo hicho,lakini vijana hao walisema ajira hakuna,kama kuna watu ambao hawana uwezo wa kuomboleza kwa kulia kwanini wao wasifanye kazi hiyo ambayo inawapa ujira.
Lakini kama kuna ajira ya kutengeneza masanduku ya kuzikia watu ambapo watu wenyewe hawajulikani watakufa lini na kifo kipi na wapi wameruhusiwa kufanya hivyo sasa kwanini vjiana mabingwa wa kulia kwenye msiba wasiajiriwe?.Kazi ni kazi tusije tukadharau kazi za watu tutakuwa hatuwatendei haki.
Tuesday, October 19, 2010
WAKAZI WA MJI WA SONGEA HAWAPO NYUMA KWA KUJICHANA KWA VINYWAJI BARIDI,KUNA USEMI USEMA UKITAKA KUJUA NGUVU ZA MLEVI UMWAGE POMBE YAKE,SASA UKITAKA KUZIJUA NGUVU ZA MNYWA SODA UFANYE NINI?
Jumanne ya leo nilipo shuhudia Lori lililojazwa makasha matupu ya vinywaji baridi aina ya Coca Cola ,liloshambuliwa na wauzaji wa vinywaji hivyo katika mji wa Songea,karibu na baa za vinywaji vikali maarufu kwa jina la bia maeneo ya Standi ya mabasi yaendayo nje ya mkoa wa Ruvuma ,vijana wakitupia na makasha hayo kama mpira wa kikapu bila kuangusha.
Ilikuwa inafurahisha lakini wao ni ajira wala siyo mchezo,mwingine kajaribu kama hukupata kesi na mwenye kampuni ya soda au utozwe faini.Kazi ni kazi bwana usidharau kazi za watu ndizo zinazo wapa umaarufu.Hata hao wanao dai kuwa wakichaguliwa watatoa ajira,hazitakuwa tofauti sana na hizo.kwa hiyo tuheshimu ajira za watu.
Lakini kando kulikuweko na wateja wengine wakijiburudisha kwa soda,kutokana na jua kali liwakalo katika mji wa Songea lakini hautoki jasho,matokeo yake unazidi kuwa mweusi,lakini Dar,joto na jasho mtindo mmoja, mambo haya jamani yanafurahisha kweli.
Ilikuwa inafurahisha lakini wao ni ajira wala siyo mchezo,mwingine kajaribu kama hukupata kesi na mwenye kampuni ya soda au utozwe faini.Kazi ni kazi bwana usidharau kazi za watu ndizo zinazo wapa umaarufu.Hata hao wanao dai kuwa wakichaguliwa watatoa ajira,hazitakuwa tofauti sana na hizo.kwa hiyo tuheshimu ajira za watu.
Lakini kando kulikuweko na wateja wengine wakijiburudisha kwa soda,kutokana na jua kali liwakalo katika mji wa Songea lakini hautoki jasho,matokeo yake unazidi kuwa mweusi,lakini Dar,joto na jasho mtindo mmoja, mambo haya jamani yanafurahisha kweli.
Subscribe to:
Posts (Atom)