Friday, August 21, 2015
PAMOJA NA USHABIKI KWA WAKEREKETWA ,CHA MSINGI HAPA NI KUWA NA SHAHADA YA KUPIGIA KURA
Ushabiki wa kusindikiza viongozi kwenda kuchukua Fomu na kurudisha Fomu,uwe wa amani na nidhamu bila kujali Itikadi za vyama vyao.
Kinachao takiwa kutolewe elimu kwa mashabiki hao, siku ya kupiga kura wasijae kwenye vituo vya kupigia kura na kudai wanamtaka nani,kelele kibao waache. wawaachie mawakala wafanye kazi yao.
Maana mkono wa Dola ni mrefu kupita kawaida,watapigwa bila faida yoyote kwani huyo watakaye mtaka kuwa Diwani, Mbunge au Rais akichaguliwa au hakuchaguliwa watapa faida gani au hasara gani.
Ushabiki usio na tija hauta saidia,Wananchi wengi wanaomba kwa Mungu kuwepo na Upigaji kura wa Amani,Ili Tanzania Ibakie kuwa kisiwa cha Amani.
Wengine wanasema hata viongozi nao waache lugha za kashfa wakati wa Kampeni zao,Matusi,lugha za kejeli,Ubabe na umwamba kwenye Kampeni hazisidii wananchi,Wananchi wanacho hitaji ni maisha nafuu, kumtoa mtanzania mwenye kipato cha chini na kumpeleka kwenye kipato walau hata cha kati na sio wimbo uliyozoeleka kila Awamu.
Tunawatakia Amani,Utulivu,Upendo na kuhasehimiana wakati wa Kampeni zao kwa kila Chama kilichoingia kwenye kinyang'anyilo cha Udiwani,Ubonge na Urais
Tuesday, August 11, 2015
BAADA YA KUINGIA IKULU MHE. LOWASSA ,BODABODA,MAMA NTILIE, NA MACHINGA WATANUFAUKA IWAPO ATACHAGULIWA
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo { CHADEMA} Mheshimiwa Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake walisindikizwa na wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kwenda kuchukua Fomu za Urais.na kusema, iwapo atachaguliwa kuwa Rais hatawangusha,na ataweka kipaumbele kwa Bodaboda,mama ntilie na Wamachinga
Sunday, July 12, 2015
NITUMENI NITAWATUMIKIA,KWA NGUVU ZOTE,MOYO WOTE - DKT JOHN POMBE MAGUFULI
Hotuba yake Magufuli baada ya kutangazwa
Wajumbe wa Mkutano huo
Wajumbe wa Mkutano huo
Dkt John
Pombe Magufuli alisema hayo baada ya kutangazwa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Aidha alisema
kuwa yuko tayari kunadi Ilani ya CCM, na kwamba wenzake 38 atakuwa nao pamoja
katika kuinadi Ilani ya Chama hadi ushindi unapatikana. Kwani Chama kwanza,CCM
kwanza na Tanzania kwanza,ni lazima kuwa kitu kimoja.
Baadaye
kamtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza,na kuweka Hitoria katika
Ramani ya Dunia kuwa na Mwanamke wa
kwanza Tanzania kuwa mgombea mwenza mwanamke.
Hatimaye saa
10 jioni leo Dkt Magufuli atanadiwa katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma na
Juma nne Dar es Salaam.
HATIMAYE DKT JOHN POMBE MAGUFULI ASHINDA KWA KURA 2,104 NA KUPONGEZWA NA DKT ASHA ROSE MIGIRO BAADA YA KISHINDO CHA USHINDI
Dkt John Pombe Magufuli ndiye aliyepata nafasi kupitia Tiketi Chama chake kuwa mgombea Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM,kwa kupata kura 2,104,ambapo Balozi Amina Said Ally kwa kura 253 na Dkt Asha Rose Migiro kwa kura59.
Wote wapo tayari kambi zao kuwa bega kwa bega na Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha ushindi unapatikana kwa Dkt Magufuli wa kupeperusha Bendera ya CCM.Na mwenye kiti wa Chama hicho.
Wote wapo tayari kambi zao kuwa bega kwa bega na Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha ushindi unapatikana kwa Dkt Magufuli wa kupeperusha Bendera ya CCM.Na mwenye kiti wa Chama hicho.
Wednesday, June 17, 2015
NG,OMBE 94 NA MBUZI 75 WA MFUGAJI MMOJA JINA LAKE HALIJAPATIKANA KATIKA MANISPAA YA DODOMA WAMESHIKWA WAKIWA SAZURULA KATIKA MANISPAA HIYO KUTOKANA NA KUKIUKA AGIZO LA SERIKALI LA KUHAMISHA MIFUGO YOTE KWENDA NJE YA MANISPAA
Uongozi wa Manispaa ya Dodoma ilishatoa agizo kuwa kila mfugaji ahamishe mifugo yake kupeleke nje ya Manispaa,na atakayekiuka agizo hilo ng,ombe akikamatwa atapaswa kumlipia shilingi 20,000 na mbuzi shilingi 10,000.kila mmoja.
Kwa hiyo mfugaji huyo anang,ombe 94 kila mmoja shilingi 20,000 sawa na shilingi 1,880,000 na mbuzi 75 ikiwamo mmoja shilingi 10,000 ,mfugaji huyo italazimu kulipa shilingi 2,630,000 kwa sababu ya kiburi na ujeuri wa kupingana na maagizo yanayotolewa na Serikali.
Mmoja anayeshughulikia mifugo inayo zurula hovyo katika Manispaa hii alisema,mara nyingi wenye mifugo wamelekezwa nini cha kufanya,lakini wanakiuka,nakwamba mjini kuwepo na mifugo inayochungwa haileti picha nzuri ni vyema watoe ushirikiano na mamlaka husika ,kuhamisha mifugo mbali na Mji.
Kwa hiyo mfugaji huyo anang,ombe 94 kila mmoja shilingi 20,000 sawa na shilingi 1,880,000 na mbuzi 75 ikiwamo mmoja shilingi 10,000 ,mfugaji huyo italazimu kulipa shilingi 2,630,000 kwa sababu ya kiburi na ujeuri wa kupingana na maagizo yanayotolewa na Serikali.
Mmoja anayeshughulikia mifugo inayo zurula hovyo katika Manispaa hii alisema,mara nyingi wenye mifugo wamelekezwa nini cha kufanya,lakini wanakiuka,nakwamba mjini kuwepo na mifugo inayochungwa haileti picha nzuri ni vyema watoe ushirikiano na mamlaka husika ,kuhamisha mifugo mbali na Mji.
JAJI MKUU MSTAAFU AGUSTINO STIVIN RAURENCE RAMADHANI ASEMA ANAUWEZO WA KUWA RAIS IWAPO CHAMA CHAKE KITAMPA RIDHAA YA KUONGOZA
Jaji Ramadhani aliwahikuwa askari kwa cheo cha Luteni Usu mwaka 1971 na hatimaye Brigedia Jenerali,vita vya Uganda naye alikuwemo.akaongeza kuwa mwaka 1978 alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Alisema kuwa baadaye aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu Zanzibar na hatimaye Tanzania Bara hadi kustafu kwake,na kwamba hadi sasa ni Jaji Mkuu wa Afrika na ni Mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo, hivyo kutokana nafasi yake aliyokuwa nayo anasema anauzoefu na anauwezo na sifa za kuwa Rais wa Nchi hii.Pia ni msafi hana tuhuma za rushwa.
Kuhusu mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi ,amesema yeye akiwa Rais atahakikisha kunatolewa elimu kwa wananchi kuondoa imani potofu ya kuwa viungo vya Albino vinampa mtu utajiri au cheo nasio mwili mzima.na kwamba serikali iliyoko madarakani imeshaanza kuchukua hatua kali kwa wale waliobainika wamefanya mauaji kwa walemavu wa ngozi hao.
Aidha akiwajibu waandishi wa habari kuhusu kuwa na wafuasi wengi wakati wa kuchukua fomu, alisema .sipendi makeke wakati wa kuchukua fomu,asema kibaya chajitembeza na kizuri chajiuza.
Jaji Ramadhan amekabidhiwa fomu kadhaa zikiwemo za kupeleka mikoani kuomba wadhamini,na kisha kuzirudisha kwenye ofisi za Chama hicho Mjini hapa.
Subscribe to:
Posts (Atom)





