Friday, September 12, 2014

MWENYEKITI WA TCD MHE. MOMOSE CHEYO ASEMA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIKUTANA NA TCD NA SIYO ALIKUTANA NA UKAWA MJINI DODOMA

Hayo yalisemwa na mwenyekiti huyo kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 kuwa hakupenda vichwa vya baadhi ya magazeti kuandika " Kikwete akutana na UKAWA Mjini Dodoma" bali ilitakiwa iwe Kikwete akutana na TCD Mjini Dodoma.

Aidha alisema kuwa mazungumzo yao na Rais yakifikia makubaliano,lakini cha ajabu bado kuna baadhi yao wamekuwa wagumu kurudi Bungeni kuendelea na majadiliano ya Rasim ya Katiba.

Alisema Bunge maalumu la Katiba lipo kisheria hivyo haliwezi kuvunjwa kwa ajili ya watu wachache walioko nje ya Bunge, bali litaendelea hadi tarehe 4/10/2014.na kwamba amewasihi wananchi kuwa waulivu kazi waliyo watuma inaendelea vizuri.

Na hakuna chama kinacho taka nchi iingie kwenye vurugu,aidha vijana wasichochewe na wachache hao kwa madai ya kuingia barabarani,kwani watakao pata madhara wao wenyewe watakuwa mbali hiyo ndiyo sifa ya wachochezi.

Saturday, September 6, 2014

MABADILIKO YA HALI YA HEWA KATIKA MANISPAA YA DODOMA KWA SIKU NNE MFULULIZO ,BARIDI,UPEPO NA MAWINGU UTAZANI TUKO NYANDA ZA JUU KUSINI

 Hiyo ndiyo Dodoma picha hizo zimepigwa baada ya kajua kujitokeza  kidogo lakini baridi ni palepale,mchana na usiku. Mzunguko wa Stendi kuu ya Mkoa wa Dodoma
 Kushoto kwako ni barabara kutokea Bungeni kuelekea mjini,na Kulia kwako ni barabara kutoka mjini kuelekea Bungeni au Morogoro.
 Barabara ya kuelekea Dodoma Sekondari
Kituo cha Bodaboda  Bohari jirani na Muungano Club na Dispensary ya Makole mkabala na maktaba ya Mkoa wa Dodoma

Friday, September 5, 2014

ZIARA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOANI DODOMA ILIFANA KATIKA UZINDUZI WA MIRADI KADHAA YA MAENDELEO KATIKA AWAMU YAKE YA NNE KISHA KUZUNGUMZA NA WAZEE WA DODOMA

 Katika baadhi ya miradi ya Maendeleo iliyofanyiwa uzinduzi katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ni nyumba za Shirika la nyumba la Taifa Medeli katika Manispaa ya Dodoma.
 Nyumba hizo zinapangishwa na kuuwa kwa wananchi.Mwananchi yeyote anaweza akanunua kwakupitia mikopo katika Taasisi za fedha.
 Ukiwa nauweo unanunua nyumba katika Shirika la nyumba la Taifa
Mwenye macho hambiwi tazama Jinsi Serikali ya Awamu ya Nne ilivyo jitahidi kutimia ahadi zake wakati wa uchaguzi,Hiyo ni moja ya shughuli  za Serikali hii,bado miundo Mbinu ya Barabara,Reli Viwanja vya ndega pamoja na huduma mbalimbali za Jamii.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA MHE.GOFREY ZAMBI AWAPONGEZA WATOTO WADOGO WANACHAMA WA VICOBA DODOMA WAKATI AKIZINDUA VIKOBA ENDELEVU MKOANI DODOMA HIVI KARIBUNI

 Naibu Waziri wa Kilimo chakula na Ushirika Mhe.Godfrey Zambi akiwasalimia watoto wanachama waVIBOBA kabla hajafanya uzinduzi wa VICOBA endelevu mkoani Dodoma hivi karibuni.
 Mhe.Zambi akwasalimia watoto wa VICOBA na ni  wanachama waVicoba Mkoani Dodoma
 Akikagua bidhaa mbalimbali kutoka  VIKOBA
 Wkiwa tayari kupokea maandamano ya wanacha wa VICOBA katika viwanja vya Mwl. Nyerere Mjini Dodoma Hivi karibuni.
 Mh . Zambi akiangalia shati la kitenge kikundi cha VICOBA wakati akitembelea miradi ya wanavicoba kabla ya uzinduzi wa VICOBA Mjini Dodoma hivi karibuni.
 Maandamano ya wanachama wa VICOBA yakiingia katika viwanja vya Nyerere Square katika Manispaa ya Dodoma wakati Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe.Godfrey Zambi akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa VICOBA Mkoani Dodoma hivi karibuni.
 Rais wa VICOBA Nchini Mhe. Devota Likokola Mkuwa kwenye nguo iliyoandikwa VICOBA akimweleza Mgeni rasmi umuhimu wa kuweka akiba kwa kutumia kitabu cha kuweka akiba.
 Mhe. Likokola akipokea maelezo kutoka LAPF Jinsi mfuko huo unavyo wasaidia wananchi waliosataafu na wale wanaopenda kujiunga ili wapatiwe mikopo hasa ya ujasiliamali.
 Rais wa VICOBA Mhe. Devota Likokola Mkuwa akitoa utambulisho kwa wanachama na wageni mbalimbali waalikwa katika uzinduzi huo Mkoani Dodoma hivi karibuni.
Mlezi wa VICOBA Mkoani Dodoma  Bw.Anthon Mavunde.kijana aliyeaminiwa,pia ni mwanasheria

Tuesday, July 8, 2014

BRAZIL WAISHANGAZA DUNIA KWA KUKUBALI KUFUNGWA MAGOLI MENGI YA MFULULIZO KWAO,NA KUWAFANYA UJERUMANI IANDIKE HISTORIA YA MVUA YA MAGOLI KATIKA KOMBE LA DUNIA

Haijawahi kutokea katika mashindano ya kombe la Dunia na kama ilitokea basi ni miaka kadhaa ya nyuma huko timu kufungwa magoli mengi ya mfulululizo na kufanya timu nyingine wachanganyikiwe uwanjani kama ilivyo tokea Jana kwenye uwanja wa Estadio Minarao ulioko Beto Horizente mechi kati ya Brazil na Ujerumani ,wakati Ujerumani ilivyo ifunga Brazil magoli 7 - 1 yaliyosababisha vilio uwanjani humo.

Pamoja na Jitihada za goli kipa wa Brazil Julio Cesar kudaka mashuti makali kiasi kile lakini hazikuzaa matunda anabakia akidaka hewa kama unavyoona pichani.

 Jitihada za Julio Casar jana haziku zaa matunda pale alipo zitiwa na mashuti ya Ujerumani katika uwanja wa Estadio Minarao jana.
 Hizo ndizo heka heka za mvua za magoli kwa wanasoka hao wakongwe Duniani,walio waacha wapenzi wa wanasoka hoa midomo wazi.Na mbaya zaidi mvua hiyo ya magoli imewanyeshea kwao na sio ugenini ambako wangeweza kuficha aibu hizo.
 Baadhi ya wachezaji wa Brazil wakiteta jambo na Kocha wao lakini wapi, mwaka wa balaa ni wa balaa tu.Ukipanda mchicha zinaota mbigili.
Ni siku ya uzinduzi wa Kombe la Dunia Brazil,ambapo Timu hiyo ilisimama kwa stahili hiyo mbele ya macho ya umati wa watazamaji uwanjani humo siku hiyo.Lakini hatima yake na shamrashamra zote zimeishia mabao 7 - 1.

Monday, July 7, 2014

MAAJABU YA TANZANIA NI VIVUTIO KWA WATALII

 Mbuga za wanyama nchini ni muhimu kwa kuingiza Taifa mapato yake ,ili kinacho sababisha vivutio hivyo visichangie kwa kiwango kikubwa ni ujangili unaofanyika katika hifadhi hizo za Taifa.
Kuna watu wanaotaka utajiri wa harakaharaka wanaoingia katika mbuga hizo ka kuanza kuwa ua tembo kwa lengo la kupata pembe za wanyama hao kitendo ambacho kinasababisha wanyama hao kupungua kwa kiwango kikubwa.
Lakini je Serikali na wananchi wanaoishi katika maeneo ya mbuga hizo wanasaidiaje kupunguza uhalifu huo ili idadi ya tembo isizidi kutokomea.Ni vizuri kila mmoja awe askari wa kuzuia ujangili nchini.

SABABA MJINI DODOMA WANANCHI WASHEHEREKEA KWA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI

Wakati siku za nyuma siku kama ya leo ya sikukuu ya sabasaba ilikuwa ikionekana kuwa kweli sikukuu ya sabasaba.Lakini kwa kipindi  hiki sikukuu hiyo inafanikwa sana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya maonyesho ya Biashara kuanzia tarehe moja hadi tarehe saba.

 kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho  ya biashara, wananchi wakitembelea mabanda  na kununua bidhaa mbalimbali, Ambapo mikoani maonesho kama hayo hayapo,na hakuna ndoto ya kufanyika maonesho hayo katika mikoa yote ili wananchi wa mikoa hiyo nao wanufauke na bidhaa hizo.