Monday, September 9, 2013

SERIKALI YAAGIZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IRUIDISHWE ILI WENGINE

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa akiongea na wahitimu wa Stashahada na Shahada ya Kompyuta Sayansi katika chuo cha St,Joseph Songea leo wanachuo 96 wamehitimu mafunzo hayo.




 Picha ya pamoja ya wahitimu wa Shahada ya kwanza katika Kompyuta Sayansi
 Picha ya pamoja ya wahitimu wa Stashahada
Picha ya pamoja ya wahitimu wa Stashahada

 Wahitimu wakila kiapo kabla hawajatunukiwa Stashahada na Shahada zao.
Mawaziri wakimsikiliza mtoa maelezo kwenye chumba cha Kompyuta sayansi



SERIKALI imewataka wanafunzi wa elimu ya juu ambao wanakopeshwa fedha na Bodi ya mikopo nchini kuirejesha mikopo hiyo,mara tu  wanapo malize elimu yao na kufanikiwa kupata ajira, kwa kulipa mikopo hiyo kuitafanya serikali kuweze kuwakopesha wanachuo wengine.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika St, Joseph  College of Information Technology Ruhuwiko nje kidogo ya Mji wa Songea leo.
Alisema serikali inahitaji kutoa elimu ya juu kwa wanachuo wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu nchini,na itajitahidi kutoa mikopo kwa kadiri ya uwezo wake ingawa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa ni wengi,kwa hiyo waliyo kopeshwa wakirejesha mikopo hiyo wanachuo wenye kuhitaji mikopo hiyo watapata.
Aidha ameto rai kwa waajiri kuonyeshe ushirikiano wao na serikali  katika kukusanya fedha hizo kwa wahitimu ambao wamewaajiri, kurejesha mikopo hiyo kwenye bodi ya mikopo.na wasipo fanya hivyo hatua kadhaa zitachukuliwa zidi yao.
Alisema serikali imetengenga shilingi trioni 1.45 kwa wanafunzi wa elimu ya juu,Wizara kupitia elimu ya juu na bodi ya mikopo imeamua kuongeza kiwango cha mkopo kwa mwanafunzi wa elimu ya hiyo.
Katika mahafali hayo wanachuo 96 wamehitimu mafunzo yao na kutunukiwa Stashahada kwa wanachuo 39  katika Fani ya Uhandisi wa Sayansi ya Kompyuta na 58 shahada ya kwanza katika Uhandisi wa Sayansi ya Kompyuta.

Sunday, August 25, 2013

TAFRIJA YA BWANA NA BIBI DICKSON D. NACHENGA ILIENDELEA KWA KEKI KUKATA NA KULISHANA NA SHUGHULI NYINGINE






















BWANA DICKSON D.NACHENGA AAMUA KUACHANA NA UKAPERA BAADA YA KUMPATA WITNESS JUMA TAFRIJA ILIKUWA HIVYOOOOOOOOOO

 Bwana Dickson D.Nachenga na Mkewe Bibi Witness Juma wakiwa wakitambulisha wazazi wa Mke
 Utambulisho uliendelea
Maharusi wakisalimia wahisani waliosababisha tafrija ifane
 Familia upande wa bwana harusi
 Wahisani wakienda kuwatakia heri
 kwa  upole Bibi Witness akimwegemea mmewe

 Ni ishara ya busu hili lakini mie sikulionna


 Maharusi kwenye chakula



 Wazazi kwenye chakula
Baadhi ya wahisani wakishudia tafrija hiyo ya kufana

TAFRIJA YA BWANA NA BIBI HARUSI DICKSON D.NACHINGA NA WITNESS JUMA ,KATIKA UKUMBI WA FAMILIA TAKATIFU BOMBAMBILI MJINI SONGEA












Thursday, August 22, 2013

ZIMBABWE, RAIS ROBERT MUGABE AAPISHWA KWA AWAMU YA 7 SASA , KULIONGOZA TAIFA HILO .

RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe aapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo kwa awamu ya 7,mbele ya halaiki ya wananchi wa nchi hiyo pamoja na Baadhi ya Viongozi kutoka mataifa ya Afrika.
Sherehe hizo zimefanyika Mjini Harare ambao watu 60 elfu walishuhudia shughuli hizo,ambazo zimewafahya washiriki wa vyama vya upinzani wakikosa raha kwa madai uchaguzi haukuwa wa haki.Lakini mataifa yamekubaliana na matokeo hayo na kuapishwa kwa Mugabe ni kwa halali.Na ndiyo maana ameahidi kuwa atakuwa mwamifu katika kulitumikia Taifa la Zimbabwe.
Lakini Wapinzani wanguwa wanatambua kuwa anayemchagua kiongozi ni mwananchi mwenyewe, mtu akipata kura nyingi inamaana wapiga kura ndiyo wamempenda aliye mpenda.Na kama hukuchaguliwa basi wananchi hawana imani na wewe,kwa nini useme haiwezekani kura zimeibiwa, je una uhakika gani kama kura zimeibiwa? kwani wakati wakupiga kura ulikuwepo kwa kila mpiga kura ukaona wamekuchagua ambapo ilikuwa ni siri yao.na wakati wa kuhesabu zikiwa zimepungua hapo utakuwa na haki ya madai hayo.