Friday, April 19, 2013

BUNGE LA TANZANIA LIMEANZA ZAMANI,ILA KIANCHOTOKEA SASA NI CHA AIBU

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilianza siku nyingi,lakini halikuwa na vituko vinavyo tokea sasa ndani ya Bunge.
Kauli hiyo imetolewa na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi wakati akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Jana.Na kwamba kumekuwa hakuna nidhamu ndani ya Bunge hilo.
Aidha kuhusu sakata la kuchinja Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alisema watanzania waache malumbano kuhusu nani kachinja,kwani toka awali kahukuwa na sakata hili.Alisema kama kuna dharura waislamu wacha wachije kwa shughuli zao,na alisema kila mtua anaweza kuchinja kwa matumizi yake.

Wednesday, April 17, 2013

MANISPAA YA SONGEA MCHELE WA MAUKANI KUTOKA MASHINENI UMESHUKA KUTOKA SHILINGI 2,400/= HADI SHILINGI 1,600/=,LAKINI HALI FEDHA NI MBAYA SANA

Bei ya mchele katika maduka ya Manispaa ya Songea imeshuka kutoka sh.2,400/= hadi sh.1.600/= na 1.400/= kwa kilo moja ,hiyo imebainika katika duka moja la Matarawe Manispaa ya Songea lijulikanalo kana duka la Moyo kuwa wanauza mchele huo kwa bei aliyoitangaza Waziri Mkuu kwa wafanya biashara wa vyakula Jijini Dar es Salaam  wauze mchele kwa bei ya sh.1,600/= wakati akipokea tani kadhaa za mchele kutoka nje.

Bw.Moyo alisema mchele unaokobolewa mashineni ni wa  Tunduru,ambao bei yake ni nafuu ukilinganisha na mchele kutoka Kyela Mbeya bei yake imebakia palepale ya sh.2,400/=,2,500/= kwa ajili ya gharama za usafirishaji kutoka Kyela Mbeya hadi Songea.

Monday, April 15, 2013

WANAHABARI KUAANZISHA TUZO YA KUTUKUKA YA DAUDI MWANGOSI

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bwana Abubakar Karsan ,amesema wanahabari wanaanzisha TUZO iliyotukuka ya Daudi Mwangosi.
Bw.Karsan alisema Tuzo hiyo itatolewa kwa Waandishi wa habari,wa magazeti,majarida,wa radio TV na Blogs.
Aidha alisema UTPC ittampa shilingi milioni tano mke wa marehemu Mwangosi ili afanyie shughuli zake za ujasiliamali.

RAI IMETOLEWA KWA WATANZANIA KUACHA SAKATA LA UCHINJAJI WA NYAMA KWA AJILI YA KITOWEO

 Mwenyeliti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,kuhusu tatizo linalojitokeza la kutaka kujua nani mwenye haki ya kuchinja/
Mfano wa sakata la madai ya uchinjaji katika mji mdogo wa Tunduma lilivyojitokeza hivi karibuni kama vurugu hizo zilizojitokeza katika sakata la uchinjaji katika mji huo Mkoani Mbeya.


RAI IMETOLEWA KWA WATANZANIA KUACHA SAKATA LA UCHINJAJI   ZAMANI WALIOKUWA  WAKICHINJA ILITAMBULIKA KUWA NI WAISLAM

IMETOLEWA Rai kwa Wanzania kuacha sakata la uchinjaji wa nyama ambayo hutumika na jamiinzima kwa ajili ya kitoweo,ambapo hapo awali waliyokuwa wakichinja nyama kwa ajili ya jamii walikuwa Waislamu.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa tangu zamani uchinjaji ulikuwepo katika jamii ya Tanzania ,lakini hakukuwepo na malumbano haya yanayojitokeza hivi sasa,na kwamba jamii ikuwa ikitabua kuwa Waislamu ndiyo walikuwa wachinjaji wa kitoweo kitakacho tumika katika Jamii nzima.
Aidha alisema hajakataza watu wanaojichinjia kuku,mbuzi wao majumbani kwao kwa ajili ya matumizi ya familia zao,bali ni uchinjaji unao tumika na jamii nzima.

Monday, April 8, 2013

SHEREHE NI PAMOJA KUVYWA NA KULA SASA MAARUSI NA WAHISANI WAO WANAELEKEA MEZA YA CHAKULA FUATILIA PICHA HIZO

 Maharusi wakipata chakula,chipsi kuku,mshikaki,sambusa,kachumbari na mazagazaga mengine ;hivyo hivyo picha zinazofuata.






 Jirani wa Baba mzazi wa Bwana harusi huko Mateka Mhe. Diwani Bibi Mapunda anayecheka.
 Ndugu wa Baba mzazi wa kwanza mzee Simba wa Makambi Manispaa ya Songea
 Wa kulia Mkaguzi wa Shule Binti Chiwangu wa kwanza kulia
Baba Mdogo wa Bwana harusi wa kwanza kushoto

Bwana Franci na Mkewe Bibi Rose Makule wakipeleka keki Ukweni kila mmoja wao

Bibi Rose akiwasha mshumaa maalumu katikati ya keki hiyo 
 Bwana Francis B.Chale na Mkewe wakipeleka keki  kwa wazazi wake
 Bibi Rose Makule akimkabidhi Baba Mkwe wake Mzee Bahati Chale kwa Heshima zote za Kichaga alizo nazo Bibi Harusi huyu
 Bibi Rose akimpa mkonoo wa heri Mama mkwe mdogo
 Mzee bahati Chale akiwonyesha wahisani wake waliyofanikisha sherehe hizo keki aliyo kabidhiwa na mama mkwe wake
 Bibi Rose Makule akimkabidhi Mume wake Keki ili awakabidhi wakweze


Bw. Harusi Francis Bahati Chale akimkabidhi mama mkwe wake keki

 Wasimamizi nao wakionyesha jinsi walivyolishana kike siku ya harusi yao hapo zamani
Baba Mzazi wa Bwana harusi,Ambaye mwanzilishi wa Ukumbi huo wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania tawi la Songea ,lilipo kwisha chini ya usimamizi wake madhubuti kama Mkuu wa chuo hicho Bwana Bahati Chale,alihamishwa na kuletwa mkuu wa chuo hicho mwingine,hiyo ndiyo zawadi ya mtenda kazi bora nchi hii badala ya kuendeleza na kuboresha Chuo hicho alicho anza nacho katika Jengo la kupanga analetwa mtu mwingine. lakini Mungu si Athimani sasa yuko Chuo Kikuu cha Songea Tawi la SAUTI Mkufunzi Hapo.

PINGU ZA MAISHA SHEREHE YA MAHARUSI KATIKA UKUMBI WA CHUO KIKUU HURIA SONGEA KATI YA BWANA FRANCIS BAHATI CHALE WA MATEKA SONGEA RUVUMA NA BIBI ROZI MAKULE WA BOMANG'OMBE HAI KILIMANJARO

 Bw. Francis Bahati Chaele na Bibi Rose wakiingia katika Ukumbi wa Chuo kikuu huria cha Songea Ruvuma siku ya Jumamosi iliyo pita.
 Bwana Harusi Francis B.Chale
 Bibi harusi Rose Makule
 Baba Msimamizi wa harusi Bw.Bosco Haule
 Mama msimamizi wa harusi hiyo Mrs Bosco Haule
 Baba wa Bibi harusi Mzee Makule harusi akisalimia wa wahisani waliyofanikisha harusi hiyo
 Bibi harusi Rose Makule akisalimia wahisani
 Dada wa Bibi harusi
 Mama na ndugu wa Bibi harusi
 Kaka wa Bibi harusi
Wasimamizi wa maharusi Bw. Bosco Haule na Bibi haule wakisalimia wahisani. Inafuatia kuwasha mshumaa na kukata keki