Tuesday, March 12, 2013

BREAKING NEWS VATCAN CITY TODAY ,INDIVIDUAL OATH EACH CARDNAL AT SISTEN CHAPE ( KATIKA MCHAKATO WA KUMCHAGUA PAPA MPYA)L

Individual prayer  by  each Cardinal to day at Vatican City.,and the election of new Pope is going on.let us pray so that to get better Pope that can Serve the church all around the World.
 Sala zinazoendelea za Makadinal Vatican na kumchagua Papa mpya,sala za waumini nazo zitasaidia kumpata Papa Mpya.wamesimama katika mstari kwenda kusali zala hiyo kwenye kitabu kitakatifu 'ambapo atataja jina lake na anakotoka ,kisha akiendelea maandiko matakatifu yaliyoandkiwa ,na kila Cardinal kafanya hivyo leo.Tunawatakia utulivu na amani Roho mtakatifu awaongoze Macardinal hao wapate Papa mpya.







Monday, March 11, 2013

HALI YA HEWA KATIKA MANISPAA YA SONGEA NA VITONGOJI VYAKE KULIKUWA NA MVUA ZA RASHARASHA ZA HAPA NA PALE

 Baada ya mvua kukatika mpiga picha wetu alikutana na lori ambalo lilikuwa na sheheni ya mzigo,kuwa ni dalili ya wananchi kupata mavuno ya kutosha kwa kuwa pembe jeo zinaletwa.
k
Na lori hilo lilikuwa likielekea ghala ya taifa ya Ruhuwiko kuliko hifadhiwa chakula kwa ajili ya tahadhali.

Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA AWASHUKURU WA KENYA KWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

 Uhuru Muigai Kenyatta ashinda kiti cha urais kwa kupata kura 6,173,433 sawa na asilimia 50.07% na kukabidhiwa cheti cha ushindi wa Urais  na mwenye kiti wa Tume ya uchaguzi IEBC Mhe.Issack Hassan,na ataapishwa baada ya siku 14 kulingana na Katiba mpya ya Kenya ya mwaka 2010.
Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe.Uhuru Muigai Kenyatta,amekabidhiwa cheti cha ushidi wa Urais kufuatia ushindi aliyoupata kwa kura 6,173,433 sawa na asilimia 50.07%  na kumwacha kwa mbali Bw.Raila Odinga kwa kura 5,340,536


RAIS mteule wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Muigai Kenyatta, amewashukuru wakenya wote kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa kwanza wa kihistoria ambao umechukua muda mrefu chini ya  Katiba mpya  ya mwaka 2010.
Mheshimiwa Kenyatta alisema hayo leo katika ukumbi wa chuo kikuu cha kikatoliki cha Afrika mashariki baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi  wa kiti cha Urais kwa kura 6,173,433 sawa na asilimia 50.07% na mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi IEBC Bw.Issack Hassan.kwamba wamevumilia jua, wametumia muda mwingi hadi kufikia nia yao ya kuwapata viongozi wa kuiongoza Kenya.na kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura.
Aidha alisema ushindi uliopatikana siyo wa Jubilee peke yake bali ni kwa wakenya wote,na kwamba ushirikiano wao ndiyo  utaofanya serikali ya Kenya ipige hatua katika maendeleo,pia kudumisha amani na utulivu uliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa viongozi waliowachagua wenyewe.
Alimewashukuru Tume ya uchaguzi IEBC,wachunguzi wa nje na ndani ya nchi,vyombo vya habari kwa kazi kubwa waliofanya tangu siku ya kupiga kura,kuhesabu hadi kutangazwa kwa matokeo.
Alisema katika chaguzi za nyuma vyombo vya habari viliwajengea wananchi chuki tofauti na uchaguzi huo,ambao unaingia katika kitabu cha kihistoria ya Kenya kufanya uchaguzi wa amani na utulivu ambapo Dunia ilikuwa na wasiwasi wa kutokea machafuko wakati wa upigaji wa kura,kuhesabu hadi kutangazwa kwa matokeo.
Uhuru Kenyatta amewahakikishia wakenya kuwa atatimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni zake,katika kuinua uchumi,amani na utulivu miongoni mwa wakenya milioni 40,na kwamba amemshukuru Mungu katika kufanikisha uchaguzi huo kwa kufanyika kwa amani na utulivu.

Sunday, March 3, 2013

CHUO CHA USHIRIKA MOSHI TAWI LA RUVUMA KINATOA ELIMU YA USHIRIKA

Hiki ni Chuo cha Ushirika Tawi la Ruvuma  katika manispaa ya Songea ,kinatoa mafunzo ya Elimu ya Ushirika kwenye vikundi vya ushirika wa SACCOS.

ULIKUWA MWEZI,ZIKAWA SIKU ,NA SASA NI MASAA TU KWA TAIFA LA KENYA LENYA ZAIDI YA WATU MILIONI 13 KUPATA VIONGOZI WAO

Kesho wananchi zaidi ya milioni 13 watajitokeza kupiga kura katika vituo 33,000 vya kupiga kura katika nchi hiyo.Aidha vituo vitafunguliwa kuanzia saa 12.30 hadi saa 11 jioni, Vituo ambavyo vitachelewa kufungua  vitaongezewa muda wa kupiga kura.

Saturday, March 2, 2013

WATOTO NA WAJUKUU WA MZEE NCHIMBI WA MSAMALA WANAWASHUKURU WATU WOTE WALIOKWENDA KUMHIFADHI BABA YAO MPENDWA GALUS ALFONS NCHIMBI

 Mzee Galus Alfonsi Nchimbi alizaliwa mwaka 1935 Mashangano katika Manispaa ya Songea , katika uhai wake alikuwa fundi mjenzi wa majumba.na t 2013 tarehe 28/2/2013 alifariki na tarehe 2/3/2013 alizikwa kwenye makaburi ya Mshangano.Mungu ailaze mahali pema peponi Amina, nahivyo ndinyo ilivyokuwa katika mazishi yake.








Friday, March 1, 2013

FAMILI YA WENA WA MABATINI SONGEA INAWASHUKURU WOTE WALIYO TOA MICHANGO YAO KWA KIJANA WA MPENDWA MAREHEMU FRANCES GELBERT WANA TANGU AKIWA MGONJWA HADI KUMPELEKA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE

 Marehemu Francis Gilbert Wana wa Mabatini Songea amezikwa katika maburi ya Mfaranyaki,picha ya chini ni mama mzazi wa Francis.
 Shemeji wa Frances na Mkewe wanaweka mashada kwenye kaburi lake
 Mama mzazi wa Frances anaweka shada juu ya kaburi la mwanae
 Baba zake wanaweka mashada juu ya kaburi la kijana wao.
 Watoto wote  wanaweka mashada juu ya kaburi
Mama huyo anaweka shada juu ya kaburi